Serikali "imewachakachua" wazee wasaafu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali "imewachakachua" wazee wasaafu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mbwigule, Feb 2, 2012.

 1. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Majuzi serikali imewalipa wastaafu waliokuwa wakilipwa kila baada ya miezi sita pensheni ya miezi mitatu badala ya sita waliyoisubiria kwa kipindi hicho. Mara ya mwisho wazee hawa walilipwa mwezi Julai mwaka jana yaani miezi sita iliyopita. Hakuna anayepinga mpango wa serikali kubadili ulipwaji huo kufanyika miezi mitatu mitatu badala ya sita ya awali, lakini swali ni kwa nini mabadiliko hayo yaanze kwa wazee hao kudhulumiwa malipo yao ya miezi mitatu? Wengi walifikiri serikali ingelipa kwanza malipo yao ya kawaida ya miezi sita yaani Julai hadi Januari kisha kuendelea na utaratibu wao mpya wa miezi mitatu mitatu.

  Izingatiwe wengi wa wazee hawa wanalipwa kiwango kidogo cha pensheni na pengine cha kudhalilisha, sasa kuwadhulumu kama ilivyofanyika si kujitakia laana ya bure? Hivi kwa nini serikali hii ya awamu ya nne inahaha kujitafutia migogoro kila kukicha hata kutoka kwa watu walioonekana kuuvumilia udhaifu wao?
   
 2. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii ndiyo serikali ya CCM; ya Tumethubutu, Tumewaweza na Tunasonga mbele ! Nadhani sasa wazee wataelewa kwa nini vijana wanataka mabadiliko maana wengi tu walikuwa watetezi wa vibaka hawa. Hivi hii serikali mbofu mbofu ya CCM haioni hata huruma kwa watu hawa ambao maisha yao ya kujinyima na uadilifu walipokuwa kazini ndicho kilichofanikisha wao kuwepo walipo sasa? Shame on them!
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sawa. Waliopo makazini wanaidai areas za toka July 2011 hadi Jan 2012.

  Jamani, hivi Kikwete ukiamua kufuta safari zako 2 za nje ya nchi pande za Ulaya na Marekani na tatu za misibani hawa wazee si watapata fedha yao?
   
 4. Michael Pima

  Michael Pima Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inasikitisha sana maana kwa umri wao hawa ni dhahiri ni wale waliotumikia Taifa hili kwa kujituma. kujitolea, moyo safi bila kufisidi Taifa. Ama kweli mvumilivu hula mbovu Tanzania.
   
 5. M

  Mr Mayunga JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Rekebisha kichwa cha habari.
   
 6. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwani nini kimetokea kwa wazee??
   
 7. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Na wewe huna dogo? ni wastaafu na hiyo ni typing error. Nashukuru wengi wameelewa nina maana gani. Lakini asante kwa kunishtua.
   
 8. M

  MINAKI Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nilikuwa naongea na mzee wangu ambaye ni mstaafu, akanambia morogoro kuna mstaafu alizimia baada ya kuona pesa aliyolipwa haitoshi hata nauli. Yaani ni udhalilishaji wa hali ya juu ambao hastahili kuendelea
   
Loading...