Serikali imetangaza kuwa mfanyakazi ambaye hatawasilisha namba ya mlipa kodi (TIN number) hadi Desemba 31, mwaka huu hatalipwa mshahara wa Januari

kodi zinazidi kuongezeka
Mkuu unaonaje ukikaa kimya ukasoma michango ya wadau? Hapa hakuna kodi mpya, ni kuweka utaratibu mzuri ili kodi zote ziende kwenye mfumo rasmi na sio holela shangwe kama ilivyokuwa. Lipa Kodi Kwa Maendeleo ya Taifa! Tunataka bwawa la JKN likamilike pia SGR!
MAendeleo hayana Chama!
 
Hivi Kayombo ndo paymaster wa serikali na private...mkurugenzi wa mamlaka anawezaje kutoa kauli ya serikali utafikiri wao ndo wanalipa mishahara
 
Kwa kuzingatia maana ya TIN ( Taxpayer Identification Number), anayelipa kodi ni mtumishi/muajiriwa na si muajiri na TIN hutolewa baada ya maombi toka kwa mlipa kodi, hivyo ni wewe ndio unayeomba na si vinginevyo.
Niwasilishe nini mkuu?
Nimekuelewa kuwa mwajiri wangu ndie anapaswa kushughulika na tiaraei.
Details zangu anazo zote
 
Kwa kuzingatia maana ya TIN ( Taxpayer Identification Number), anayelipa kodi ni mtumishi/muajiriwa na si muajiri na TIN hutolewa baada ya maombi toka kwa mlipa kodi, hivyo ni wewe ndio unayeomba na si vinginevyo.
Ahsante
 
Safi Sana endeleeni kiwakamua mpaka warudishe akili zao. Mi walimu siwapendi kabisa ndo wameshiriki kuiba kura sasa wakamuliww tu hakuna namna.
 
Hivi Kayombo ndo paymaster wa serikali na private...mkurugenzi wa mamlaka anawezaje kutoa kauli ya serikali utafikiri wao ndo wanalipa mishahara
Kwa serikali hii ni kawaida, hukumsikia SACP Mambosasa alipozungumzia kuhusu uhaba wa cement juzi kati hapo.
 
Mpaka sasa hivi waajiri wapo kimya hawazungumzi lolote.
Hata TRA na kusitisha mishahara wapi na wapi?Kwanini wao wasiwachukulie hatua waajiri ambao hawajawasilisha hizo TIN za waaajiriwa wao coz swala la mshahara ni mimi na mwajiri wangu kama mimi sijawasilisha hiyo TIN basi wao waanze na mwajiri wangu ambaye ndio wakala wao.
 
Mie binafs nafkiri ni wakati wa serikali na TRA kuangalia upya mfumo wa kodi wanayokata kwa watumishi wa serikali, kama vipi na wao walipe kwa miezi 3, 3 au miezi 6 au kwa mwaka na malipo yawe ni mara moja tu na sio kukata kila mwezi maana hata mfanyabiashara mkubwa halipi kodi kila mwezi bali kwa mwaka au nusu mwaka, inakuwaje wafanyakazi wetu wawe wanatozwa kila mwezi??

Kama sababu ni kulipwa mshahara kila mwezi kwani wafanyabiashara wanaolipa mara moja kwa mwaka/miezi 6/miezi 3 si nao wanafanya biashara kila mwezi??

Hapa naona wafanyakazi wamebebeshwa zigo kubwa maana ukipiga hesabu ya mfanyakazi anayepokea mshahara wa ngazi ya daraja D kodi yake anayolipa kwa mwaka mzima ni zaidi ya 1.5 miln!

ni uonevu na wizi mkubwa sana kwa wafanyakazi
 
Safi Sana endeleeni kiwakamua mpaka warudishe akili zao. Mi walimu siwapendi kabisa ndo wameshiriki kuiba kura sasa wakamuliww tu hakuna namna.
WALIMU WA SEREKALI HILI HALIWAHUSU KWASABABU HAO SIKU NYINGI TANGU WALIPOAJIRIWA WALIKUA WANAKATWA. YANI KIUFUPI WADANYAKAZI WA SEREKALI WENGI WAO WALISHAANZA HUU UTARATIBU.
 
Mfanyakazi wa Tz ni kama mtumwa, mshahara ukatwe kodi, bado bidhaa zote anazonunua nazo akatwe kodi, asomeshe, kuuguza, na kuitibu familia, umeme, maji, hili ni balaa.
Mitano Tena 🖐️
 
Hapo kwenye Tin upande wa sekta binafsi Kuna pesa nyingi sana zinapotea Sasa sijui JPM Kama wasaidizi wake wataweza kusimamia hapo hasa TRA na rushwa, wafanyakazi wa binafsi kwenye makampuni wanalipwa nusu mshahara ili wasikatwe Kodi kubwa na nssf pia, na wengine wengi wanajifanya kulipwa Kama vibarua Sasa hao vibarua ndo wengi sana napendekeza pia wapewe Tin au kitambulisho Cha mjasiriamali yaani mbona barabara zitafika vijijini wakiwa serious kweli kwenda mguu kwa mguu Kwenye makampuni Kama wanavyokuja kwenye maduka ghafla, wakifika tu waanzie ofisi za uhasibu zote kuomba idadi ya wafanyakazi then wahamie HR ghafla, alafu Waite wafanyakazi wote watoe Tin namba walinganishe na idadi, yaani Kuna pesa nyingi zinapotea. Ila waanze serikalini kwa mawaziri na wabunge kutuonyesha mfano kwa kupewa hizo Tin namba. Hapa nasubiri barabara kijijini kwangu hizi pesa zikikusanywa.
 
Mkuu unaonaje ukikaa kimya ukasoma michango ya wadau? Hapa hakuna kodi mpya, ni kuweka utaratibu mzuri ili kodi zote ziende kwenye mfumo rasmi na sio holela shangwe kama ilivyokuwa. Lipa Kodi Kwa Maendeleo ya Taifa! Tunataka bwawa la JKN likamilike pia SGR!
MAendeleo hayana Chama!
Mi nawashangaa hawa watanzania wengine,,yaani mnataka kuishi bure bure tu,,lipeni kodi,huo ndo uzalendo,,hakuna kuishi bure hapa...hutaki,,nenda Qatar
 
Back
Top Bottom