Serikali imesitisha uzalishaji wa pombe ya Banana kwa kutokidhi viwango vya ubora

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Siku chache zilizopita, mdau wa JF aligusia juu ya Pombe hii kuwa hatarishi kwa wananchi. Serikali imechukua hatua mapema ili kuwalinda wananchi.

Hoja ya mdau inapatikana hapa Unywaji wa pombe aina ya Banana inaathiri nguvu kubwa sana ya vijana

==========

Serikali imesitisha uzalishaji wa pombe aina ya Banana inayozalishwa na kiwanda cha Tanbasi Investment kilichoko Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro baada ya kubainika kushindwa kukidhi viwango vya ubora.

Jana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, alitangaza kufungwa kwa kiwanda hicho kutokana na ripoti ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kagaigai alifikia uamuzi huo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu wa TBS.

“Ripoti ya TBS inaonyesha kuwa sampuli za pombe hiyo zilizopelekwa huko hazifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuongezwa kiwango kikubwa cha kemikali ya Asetic Acid.

“Nilivyokuja Kilimanjaro, niliambiwa na viongozi wa dini kwamba Rombo kuna viwanda vingi vya kutengeneza pombe, ambazo hazina ubora na zinaleta madhara kwa binadamu.

“Nikaelezwa zipo zilizosababisha baadhi yao kupoteza maisha ndio maana nikafanya ziara maalum huko ya kutembelea viwanda hivyo na nilipochukua sampuli katika moja ya viwanda, hayo ndio majibu yake," alisema.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa, mara nyingi imekuwa vigumu kubaini pombe ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na udanganyifu unaotumiwa na baadhi ya watendaji wasio waaminifu.

Alisema wilaya hiyo imekuwa na matumizi makubwa ya pombe zisizo rasmi ambazo zinachangia kupoteza nguvu kazi ya taifa, ongezeko la matukio ya kihalifu na migogoro ya ndoa.

Akizungumzia zaidi madhara ya pombe hiyo, Meneja wa TBS Kanda ya Kaskazini, Happy Kanyeka, alisema sampuli waliyopokea kutoka kwenye kiwanda hicho imeonyesha pombe hiyo haikidhi kiwango cha ubora.

“Pombe hiyo aina ya Banana inayozalisha kiwandani hapo haitauzwa mpaka pale TBS itakapofanya uchunguzi wa kina, tutaangalia mchakato mzima wa uzalishaji, tutachukua sampuli nyingine tena na kiwanda hicho kitakuja kufunguliwa baada ya kujiridhisha na ubora wake.

“Pia tumekubaliana tutapitia viwanda vyote vinavyozalisha pombe aina hiyo katika mkoa wa Kilimanjaro na mikoa jirani kuangalia kama vinakidhi viwango.

"Ingawa tulifanya ukaguzi Septemba mwaka huu, tutarudia hasa kwenye viwanda vya Banana, tutafanya utafiti kuona madhara yanayowakumba watu wa wilaya ya Rombo yanatokana na nini kinachowekwa kwenye pombe hiyo," alifafanua.

Alisema katika sampuli iliyochukuliwa awali imeonyesha uwapo wa (Asetic Acid) nyingi hali inayopelekea kushindwa kukaa kwa muda uliokusudia.

Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo waliozungumza na Nipashe, akiwamo Deogratus Tarimo, walisema hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuchukua sampuli katika viwanda kutasaidia kuleta mabadiliko.

“Kwa sasa hatuna vijana, wengi wamejiingiza kwenye pombe, matukio ya uhalifu na mauaji yamekithiri na migogoro ya kifamilia imeongezeka.

"Tunaomba serikali ifungie viwanda vyote ambavyo havikidhi matakwa ya kitaalamu na kisha wafanyabiashara wawekewe utaratibu maalum wa kuomba vibali ili kufungua biashara hizo upya,” alisema.

Chanzo: NIPASHE
 
Kiwanda si kina formula ya kutengeneza pombe?

Means kiwanda cha Banana cha Rombo mtaa A kinatumia same formula na kiwanda cha Banana cha Rombo mtaa C.

Means kama umekuta hitilafu katika bidhaa ya kiwanda A ambayo siyo hitilafu ya kibinadamu ni ya kiformula basi product ya kutokea kiwanda chochote haiwezi kua sawa.

Unless kama zinajitegemea kiformula which is highly unlikely.

So hapo ilitakiwa vyote vifungwe na siyo kusema utaenda kukagua na chingine wakati vyote vinatumia formula moja kuzalisha same product.
 
Kongole mh kigaigai law nnijuavyo Rombo,Marangu vujana wakiamka alfajiri tuu jana kalala na njaa ila anakuambia nakwenda kutoa lock
Mashavu yamewaning'inia utadhani wazee wa miaka 80 vile kumbe ni kijana wa miaka 26 tuu
 
Tunamshukuru sana Mkuu wa mkoa kwa umakini aliouonesha katika jambo hili hususani bidhaa hii ya banana Wine, kwani ameonesha kuijali afya ya wananchi wa Kilimanjaro huku akishirikiana na TBS...

LAKINI, mm ningependa kulitazama swala hili kwa upande wa pili..
Banana wine ni mvinyo ambao umeonekana kutengenezwa sana na wajasiriamali mbalimbali hususani miaka ya hivi karibuni, si Tanzania tu hata mataifa mengine muamko wa kutengeneza wine kwa kutumia Banana umeongezeka pia.

Kwa upande wa maendeleo ya viwanda, serikali na taasisi kama TBS zikishirikiana na hawa wazalishaji basi tutakuza uchumi wa nchi maradufu kama viwanda vingine vikubwa like TBL na SERENGETI..

Ninachokiona mm katika taarifa hio ni KUUA Viwanda hivi vyote vidogo vidogo vinavyotengeneza Banana wine, kwani taarifa hii ni silaha tosha katika kupoteza soko na wateja wa bidhaa hii.

Kama shida ni acetic acid, hii lazima iwepo tu kulingana na specifications zilizotolewa na TBS wenyewe (Angalia attachment hapo chini). Na kama imetokea kiwango hicho specified kimezidi, kuna corrective actions ambazo TBS hua wanashirikiana na Viwanda ili kutatua shida iliyojitokeza, SIO kwenda kwenye media na kusema bidhaa fulani ni mbaya na haifai kwa Jamii,Theres always a chance to correct the mistakes!
Kwan bidhaa ngapi zinakutwa na TBS ziko nje ya specifications na Hazitangazwi???

Na kama shida ni vijana kutelekeza familia, hio ni tabia tu ya mtu. na kama tabia hii inaletwa na pombe, Basi pombe zote zifungiwe,
Why BANANA WINE pekee???

There is something i don't understand kwenye hili sakata! AHSANTENI.
 
Screenshot_20211201-203533.png
 
Back
Top Bottom