Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Serikali imeninyang'anya korosho zangu

Cathelin

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
2,071
Reaction score
3,998
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.

................................................. ..........

UPDATES

Naamini mmejionea wenyewe kupitia ITV asikari polisi wamepora pesa na Korosho za watu, afu wamewapa kipigo.

Nyie mbuzi wa Lumumba mlikuwa mnabisha nini. Jiwe ni laana kwa nchi yetu
 
Duh.. nimesoma hadi nahisi moyo kusimama kwa mdam. Yaani mtu amekuletea ukanunue kwa hiari yake.halafu leo serikali inasema hauna shamba hivyo inachukuwa bila kujua wewe umeipataje.
BASI NA SISI WAUZA MAHINDI NA MCHELE TUJIANDAE MAANA NA SISI TUNASTOCK LAKINI HATUNA MASHAMBA WALA KIBANDA KIJIJINI
Ila nilishawahi kuandika hapa. MABENK YAJIANDAE KUFIRISI WATU BILA HURUMA KWA SABABU YA KOROSHO.
Ukiandai sana utaambiwa nyie ndio mliokuwa mnanyanyasa wakulima na leo ni kisasi chenu
 
Aisee so pain, nalia sijui nianzie wapi.

Baada ya kukaa bila ajira niliamua kujiajiri bihashara ikawa ngumu, ikabidi nibadilishe aina ya bihashara, kutokana na ndugu yangu alifanya biashara ya Korosho na ikamlipa nikaamua na mimi kutafuta riziki kupitia korosho.

Sikua na mtaji mbaba mmoja ni family friend alikuwa amestaafu so pensheni alikuwa nayo basi akanionea huruma na kunikopesha milioni kumi(10m).

Basi nkaenda kusini aise wananchi walikuwa na hali mbaya yaani mtu mwenyewe ndo anakuletea au kukuitia korosho, basi nilinunua tena bila kumlazimisha mkulima, bali mkulima ndo anakuomba ununua maana hata pesa ya sukari anakuwa hana.

Serikali walipokuja kuhakiki wakaniuliza kama nina shamba nkawaambia sina, me nimekuja kufanya bihashara kama mtanzania maana ni haki yangu kuishi popote,

Bila huruma wakataifisha korosho zangu, nilizimia baadae nkazinduka, Baba alipopata tarifa naye alizima gafra.

Mzee aliyenisave hela ananidai na serikali imechukua Korosho zangu.

Basi Baba ameamua kumuuzia shamba letu maana hakuna jinsi ya kulipa deni.

Naichukia sana Tanzania, sahivi naisi kujitoa muhanga.
Baba yangu jee ulikuwa na leseni ya biashara??????????????
Kisheria inawezekana kuwa wewe ni mlanguzi kwa sababu huna shamba wala leseni ya biashara hiyo.
Ninadhani mwisho wa siku mtalipwa ila jamani tujifunze kufuata sheria na taratibu zake.
 
Pole sana Mkuu..ila hiyo uliyokuwa unafanya ndio KANGOMBA..yaani unanunua korosho kwa mkulima kwa shilingi 1000 ili wewe uje kuuza kwa 3300. Japo umesema hukuwa unawalazimisha ila ulitumia shida za wakulima kujinufaisha. Suala lako linafanana na utetezi wa kufanya mapenzi na binti chini ya miaka 18, hata kama ulimtongoza na kukubaliana lakini sheria itakuambia umebaka.
 
Back
Top Bottom