Serikali imeiuza Kariakoo kwa Wachina

Serikali imeiuza Kariakoo kwa Wachina

Na hii ndio legacy ya ujamaa, kitu pekee mtanzania anaweza ni propaganda. Kwasasa ni muache ulanguzi au mkubali kufa kifo cha mende

Nyuzi nyingi sana humu Jf zipo tangu kitambo mkionywa upumbavu wa kutaka mpaka faida zaidi ya 100% mkapofusha macho na kuziba masikio.

Wakati umewadia kushare kile kikombe mlichokuwa mnatunywesha nacho maji, serikali wasikilizie hata miaka mitano ijayo then wawapige ban wachina maana mpaka wakati huo vichwa vyenu vitakuwa vimerudi kwenye default settings
 
Wachina ni janga kubwa sana Serikali inabidi ichukue hatua haraka sana hasa kokote kule kwenye wachina Kariakoo, pale Ubungo jengo kubwa jipya, hawa wachina ni watu hatari sana na wataua uchumi wa nchi yetu na wananchi kupoteza biashara zao..!! Kuna wachina pia walitoka Mombasa wako Dar, wanajenga majengo, ni hatari sana, pia TIC waangalie wawekezaji wa kichina ni wahuni kwani anakuja mmoja ana dollar say $100,000 anajisajili mmoja kama investor kumbe wako wachina 100 ndio wamejichangisha..

Wachina wachukuliwe ni hatari kubwa kama Corona kwa uchumi wa nchi yetu, wachina wote Serikali iwafuatilie, iwe kama janga la Taifa, hasa Kkoo itapotea kabisa na wananchi wetu watapoteza biashara zote.
 
Haiwezekani Kariakoo wachina wanaishi kama kwao.

Mbaya zaidi hawalipi kodi ipasavyo. TRA haina kanuni za asiye raia kulipa kodi kama mzawa

Hii ni sawa tu na kusema Kariakoo imeuzwa
Wafanya biashara wa kibongo ni wahuni bidhaa ya 12k unauziwa 35k. Risiti hawatoi na hata wakitoa ni za magumashi Acha wachina watupe unafuu ya maisha. Tumechoka na mawinga wa kariakoo
 
Haiwezekani Kariakoo wachina wanaishi kama kwao.

Mbaya zaidi hawalipi kodi ipasavyo. TRA haina kanuni za asiye raia kulipa kodi kama mzawa

Hii ni sawa tu na kusema Kariakoo imeuzwa
Kwani lazima wote mkae kufanya umachinga Kariakoo? Kwanini msiende kulima mabonde na misitu yenye rutuba yako ya kumwaga.

Ila mumeona kukaa Kariakoo na kufanya uwinga ndiyo jambo la maana
 
Wachina ni janga kubwa sana Serikali inabidi ichukue hatua haraka sana hasa kokote kule kwenye wachina Kariakoo, pale Ubungo jengo kubwa jipya, hawa wachina ni watu hatari sana na wataua uchumi wa nchi yetu na wananchi kupoteza biashara zao..!! Kuna wachina pia walitoka Mombasa wako Dar, wanajenga majengo, ni hatari sana, pia TIC waangalie wawekezaji wa kichina ni wahuni kwani anakuja mmoja ana dollar say $100,000 anajisajili mmoja kama investor kumbe wako wachina 100 ndio wamejichangisha..

Wachina wachukuliwe ni hatari kubwa kama Corona kwa uchumi wa nchi yetu, wachina wote Serikali iwafuatilie, iwe kama janga la Taifa, hasa Kkoo itapotea kabisa na wananchi wetu watapoteza biashara zote.
Wacha wivu, shughulisha akili yako ufanye biashara. Kwani kuna kosa gani wachina kumi kuchangia mtaji wa USD 100,000 unaotakiwa na TIC?

Sisi tunachoangalia ni ingizo la USD 100,000 tu, wawe mmoja au wawili au 20 ni immaterial.

Wewe uko mmoja na pumbu zako tu umawachamba wachina 10 walioleta USD 100,000
 
Mleta mada umeandika kishabiki na kibaguzi tu, lakini ulichoandika sio kweli.
Uhalisia ni huu.
1. Hakuna mchina anayeweza kuishi na kufanya biashara au kazi hapa Tanzania bila kibali. Wale jamaa ni smart kwa hilo maana wanajua msingi wa kuishi na kufanya chochote hapa Tz ni kuwa na hivyo vitu.

2. Hakuna mchina asiyelipa kodi TRA ambaye yuko hapo Kariakoo. Kulipa kodi kihalali ndio kinga ya hao wachina.

3. Kwa sababu ya kuongezeka idadi yao huku wakiwa makini, ujanja na uharaka wa kufanya biashara kumewatisha na kuwanyima fursa watanzania hapo Kariakoo hivyo kutaka upendeleo au udhibiti, jambo ambalo sio sahihi kisheria.

Ushauri.
Watanzania tuache kulalamika, tupambane.
 
Kwani lazima wote mkae kufanya umachinga Kariakoo? Kwanini msiende kulima mabonde na misitu yenye rutuba yako ya kumwaga.

Ila mumeona kukaa Kariakoo na kufanya uwinga ndiyo jambo la maana
Mkuu kitu kama hujui ungenyamaza Tu
Hivi bakhresa anaezalisha ngano akianza kuuza chapati nyumba kwa nyumba huoni kuna madhara kwa watu maelfu wanaouza chapati?
Mchina ana kiwanda yeye auze kwa agent .agent auze kwa mtu wa jumla .yaani kinachotakiwa ni biashara ifate mkondo wake.wala winga hausiki hapa
Tatizo huku mna wivu na matajiri WA kariakoo
 
Unaambiwa hakuna Mchina asiye na kigogo kwenye kila idara nyeti hivyo hata ukimshtaki anachomoa
Wachina wako kwenye Cartels😁 yani ukimtingisha ana Godfather wake ambaye ana connection ubalozini.

Kesi ikifika ubalozini kama sio ya msingi inazimwa chap. Mtu anatoka kidogo akirudi anaendelea na mambo yake. Wachina wako smart sana na flexible kwenye ku adopt mazingira halafu pia ni wepesi wa kuhonga kuliko kufata sheria. Hapo ndipo wanapoenda sawa na mamlaka zenu za kimchongo.
 
Mkuu kitu kama hujui ungenyamaza Tu
Hivi bakhresa anaezalisha ngano alianza kuuza chapati nyumba kwa nyumba huoni kuna madhara kwa watu maelfu wanakouza chapati
Mchina ana kiwanda yeye auze kwa agent .agent auze kwa mtu wa jumla .yaani kinachotakiwa ni biashara ifate mkondo wake.wala winga hausiki hapa
Tatizo huku mna wivu na matajiri WA kariakoo
Mawinga ndo wanaumia sahizi wala sio wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa.
 
Back
Top Bottom