Serikali imefilisika?

Mhhh mkuu ajira inahitaji pesa,kumbe kuna walimu wakujitolea,wale wakujitolea inabidi wawe wa kwanza kuajiriwa.
Kama tuko serious na elimu hata elfu 10 ni idadi ndogo haikidhi matakwa ya taifa.Wapo wahitimu walimu zaidi ya laki mmoja wapo mitaani wengine miaka 5.
So?
 
Lengo la serikali kuajiri ni kuondoa tatizo la upungufu wa watumishi na siyo kuhakikisha wahitimu wote wanapata kazi.

Wahitimu watumie elimu na maarifa waliyoyapata ktk masomo yao kujiajiri
Na wanasiasa wasikabe Hadi kufikia hatua kupora uchaguzi ili wabaki na nafasi zao nao wajiajiri
 
Cha kushangaza kuna wahitimu wa fani ya ualimu zaidi ya elfu 90 mtaani! Halafu wanataka kuajiri Walimu elfu 7 pekee! Na kati ya hao 7000 unakuta kuna ndugu zao humo humo, kuna watakao toa rushwa!

Wakati huo huo vyuo vikuu na vile vya kati navyo vinaendelea tu kudahili wanafunzi kutoka familia masikini (maana hakuna mtoto anayetokea familia inayo jiweza, anaye jiunga na chuo kusomea ualimu) kusomea masomo ya ualimu!

Hakika huu ni udhaifu mkubwa sana kwa serikali ya ccm.
Mama anaupiga mwingi
 
Kuna chawa wa mama ndo huwa wanasifia hivyo vitu kwa nguvu,sasa waulize walete majibu nini kilitokea kutoka elfu kumi na kuomba elfu saba.
Wengune tunasubili mzunguko wa fedha ili tuendelee kufanya biashara kama zamani.
JK alikuwa anaajiri Hadi 42,000
 
Hivi walimu na nyie wakulilia ajira kweli wakati mna maarifa tosha mnashindwa kugeuza changamoto kuwa fursa,huku mitaani kuna kundi kubwa la vijana ambao kwa namna moja au nyingine walishindwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani hasa kidato cha nne na sita kweli mnashindwa kujiunga vikundi mkaomba hata madarasa ya shule zetu za umma mkafundisha vijana ili wasonge mbele zaidi,naimani hamuwezi kosa suport ya serikali na wadau mbalimbali wapo wanaopenda elimu isonge mbele.Walimu waliajiriwa miezi michache tu iliyopita walimu elfu 6 baadae elfu sita tena kama sijakosea.
Ndo nini
 
hata mim nimeshabgaa acha kwanza waende hao buku 7.ni weng ogopa sana.hiv unajua bajet ya kuajiri nimkubwa kias kwamba inahitaj umakin.angalia tu bajet ya nyumban kwako ilvo ndio ujue ngumu kias gani kuendesha nchi

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Ugumu kuendesha nchi, Ila kuchoma hela kwa kesi za kijinga ni sawa?
 
Acha kukatisha watu tamaa, wanaanza kuajiliwa waliomaliza zamani, mtiririko utaendelea hadi wote, kumbuka kuna watu wanastaafu kila mwaka, wanakufa, wanaacha kazi n.k Kubwa zaidi watz tunajua kuzaliana, simbilisi haoni ndani!! Kila mwaka mwaka ni kujenga madarasa na kamwe hayatatosha, ajira za waalimu zipo za kutosha, ni muda tu
Vyuo vinamwaga hatari,,,na serikali inachukua wa science Arts wapambane na Hali yao
 
Vipindi vipo vingapi kwa siku..kwa wiki..kwa mwezi..kwa mwaka..

Hujui kuwa kuna walimu wanafundisha masomo zaidi ya mawili na vipindi vinatofautina muda?

Wewe utakua sio mwalimu..na kama ni mwalimu basi ni aibu kwa taaluma kupata kilaza kama wewe.

Watu kama wewe ndio mnafanya elimu ya nchi hii inshuka kila siku.

#MaendeleoHayanaChama
Tulia we Mwalimu wa UPE
 
Mwaka wa fedha 2021/2022 serikali ilipanga kuongeza watumishi idara ya Elimu ili kuinua kiwango Cha Elimu nchini

Mwezi October Ummy Mwalimu alisema serikali itaajiri walimu elfu 10, kabla ya December, mpaka mwaka unaisha hakuna Mwalimu aliyeajiliwa

Leo Waziri Bashungwa kasema wameomba kibari Cha kuajiri walimu elfu7, yaani kwenye bajeti walisema wataajiri elfu 10,, sahivi wanasema ni elfu 7, tumebaki na miezi 5 kumaliza mwaka wa bajeti.

Unajenga madarasa kwa mkopo, yapatayo elfu15 afu unaajiri walimu elfu7, je serikali haina hela za kuajiri walimu wa kufundisha watoto wetu? Kama hela zipo why wapunguze idadi ya kuajiri from elfu 10 to elfu7?

Ebu tujibu nyie watu wa CCM

Laana ya Uvamizi wa Zanzibar Na mauwaji ya watu kwa maelfu Na kuendelea kuuwa kila baada miaka mitano ,itaendelea kuwatafuna mpaka mtapoiachia Na kuomba radhi. Vyenginevyo mtateseka zaidy kila siku zikienda vizazi Na vizazi
 
Vipindi vipo vingapi kwa siku..kwa wiki..kwa mwezi..kwa mwaka..

Hujui kuwa kuna walimu wanafundisha masomo zaidi ya mawili na vipindi vinatofautina muda?

Wewe utakua sio mwalimu..na kama ni mwalimu basi ni aibu kwa taaluma kupata kilaza kama wewe.

Watu kama wewe ndio mnafanya elimu ya nchi hii inshuka kila siku.

#MaendeleoHayanaChama
- Pathetic! Mwalimu anaweza kufundisha vyumba viwili vya darasa kwa wakati mmoja?

- Kufundisha somo zaidi ya moja hakumfanyi mwalimu afundishe madarasa tofauti kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom