Serikali imeanza ujenzi wa ofisi mpya ya kisasa ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera

Serikali imeanza ujenzi wa ofisi mpya ya kisasa ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
, ambayo itagharimu shilingi bilioni 9 hadi kukamilika kwake.

Katika hafla fupi ya makabidhiano ya eneo la ujenzi na usaini wa mkataba iliyofanyika jana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa, alieleza kuwa jengo hilo litakuwa la kisasa, imara na litaweza kudumu kwa zaidi ya miaka 100 bila kuathiriwa na majanga kama tetemeko la ardhi.

Mwassa, ambaye ndiye mwanzilishi wa wazo hilo, alisema kuwa ofisi ya sasa ya Mkuu wa Mkoa imekuwepo kwa zaidi ya miaka 60 na ubora wake umepungua kwa kiasi kikubwa. Alibainisha kuwa jengo hilo lilipitia tetemeko la ardhi na linaathiriwa na mabadiliko ya mazingira, ikiwemo kusogea kwa Ziwa Victoria ambalo tayari limeharibu baadhi ya nyumba za watumishi

Aidha, alieleza kuwa mkandarasi wa mradi huo tayari amelipwa asilimia 25 ya jumla ya fedha za awamu ya kwanza ya mradi huo, ambazo ni shilingi bilioni 4.6

Kwa upande wake, Mhandisi Raphael Nyatega kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, alisema mradi huo umeanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 na unatarajiwa kukamilika mwaka wa fedha 2025/2026

1752819968100.png


1752820008004.png

Chanzo: Habari leo
 
Back
Top Bottom