Serikali iliyozidiwa hata na timu

Goheki

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
448
387
Inasikitisha na inaumiza sana kuona serikali yetu isivyo ni mipango madhubuti,yaani timu ya soka ya Tp Mayembe inamiliki ndege mbili.Tz hatuna ndege hata moja,ila tunaambia viwanja vitapanulia.HII NI AIBU KWA TAIFA.
 
Kwani kipimo ni ndege tu mzee au unapimaje uwezo wa serikali yako...tp mazembe inamajukumu gani yanayoifikia serikali ya tanzania..mashulea,hospitals,mabarabara,pension za baba ako, etc acha mawazo ya chadema na cuf embu jivue gamba
 
aibu ya ndege ni ndogo, aibu ya umeme je? ya maji je? ya dawa mahospitalini je? ya wanafunzi kufeli je?

hayo yanahitaji kodi zetu ambazo jk na kundi lake wanzichezea kwenye anasa angalia magari ya kifahari,sherehe kila kukicha kinachonisikitisha hata kupanga miji tu inawashinda ...ukitaka kupimiwa kiwanja upate hati miliki unalipa gharama zote lakini fikiria kwa mwaka watu wanalipwa mishahara ambazo ni kodi zetu lakini hakuna kinacho fanyika,,,bara bara zinajengwa kwa hisani ya watu wa ...soma vibao kwenye ujenzi wa barabara
 
Kwani kipimo ni ndege tu mzee au unapimaje uwezo wa serikali yako...tp mazembe inamajukumu gani yanayoifikia serikali ya tanzania..mashulea,hospitals,mabarabara,pension za baba ako, etc acha mawazo ya chadema na cuf embu jivue gamba

Hilo ni jambo mojawapo la kukuza uchumi,tp mazembe hawakusanyi kodi,ila mikakati imewafanya wafanye maendeleo,sisi tunadanganyana tu,kuna nchi zenye mashirika ya ndege yanayochangia mapato ya nchi kwa kiwango kikubwa,eg.ethiopian air,kenya
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/
 
hata hiyo nayo ni ndogo, aibu ya kuuza rasilimali je na kupitisha barabara na hotel kwenye mbuga na kuingia mikataba feki ambayo hata mlevi wala housegirl hawezi kusaini naona ndio aibu kubwa zaidi
aibu ya ndege ni ndogo, aibu ya umeme je? ya maji je? ya dawa mahospitalini je? ya wanafunzi kufeli je?
 
AIBU KUBWA ZAIDI ni ile kuwa hata kiongozi wa nchi hajui chanzo cha umaskini wa watu wake na yeye anajiuliza tu....hajui kwanini watoto wanafeli na wala hajui kwanini mawaziri wanasaini mikataba feki
 
AIBU KUBWA ZAIDI ni ile kuwa hata kiongozi wa nchi hajui chanzo cha umaskini wa watu wake na yeye anajiuliza tu....hajui kwanini watoto wanafeli na wala hajui kwanini mawaziri wanasaini mikataba feki

Hawezi kujua kwani ahadi hewa ni nyingi mno,reli hadi kigoma/mwanza,barabara za juu dar,machinga complex kila wilaya dar,hospital kila jimbo tena zilizopo ziwe za rufaa wakati hazina huduma zaidi ya majengo.
 
Back
Top Bottom