Serikali ijue ukweli CCM haina 100% ya Watanzania

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,629
8,806
Nimekuwa nikifuatilia serikali hata wakati wa Magufuli . Tatizo moja ni serikali ya Tanzania imejiaminisha kwamba wana support ya 100% ya Watanzania.

Tatizo ni moja tu huwezi kuyeyusha 30%-40% ambayo hao CCM wamesema wapinzani wamepata kura.

Yaani pamoja wa wizi wote wa 2020 hakuna mtu anabisha kura za wapinzani ni zaidi ya 30%. Sasa kama hata hii ni kweli huwezi kusema 30% hawana cha kuongea na ndiyo maana kuna matatizo mengi ya siasa. Pamoja na kwamba CCM imewazidi k

idogo Chadema Watanzania wengi ambao hawana chama hawapendi uonevu na si kweli kwamba wote wanaipenda Chadema.

Hivyo CCM badala ya kujidanganya wajiulize inakuwaje kwa wakati mgumu hivi Chadema wameweza kufikisha wanachama 10M tena wakujiandikisha kabisa! hili ni suala la kujiuliza sana.

Tatizo la binadamu wanabadilika hebu tuangalie mikutano imekatazwa angalieni mitandao inavyoendelea, angalieni kukuwa kwa TV online na kesi kama za Mbowe zinavyofuatiliwa.

Mikutano ya mitandao inafikisha mpaka watu 6,000 live! hili sio suala dogo.

Naunga mkono Rais kukutana na Lissu na umakini mkubwa Samia awe nao kwa wapambe wake.

Hizi ndiyo estimate

CCM : 14,000,000 au 43%
Chadema : 12,000,000 au 37%
Swing voters: 6,500,000 au 20%

Jumla ya wapiga kura 32,500,000




 
Mil 12 ya chadema ni ya miezi 4 iliyopita , taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadokeza kwamba kuna nyongeza ya 3mil mpaka january 31 2022 , hawa ni wa Chadema Digital , mpaka february 5 ccm ilikuwa na 2mil tu , hii ni kwa mujibu wa Chongolo ambaye ni katibu mkuu wa CCM

Akili kichwani mwako
 
Back
Top Bottom