Mpalakugenda
JF-Expert Member
- Jun 2, 2015
- 2,155
- 1,429
Ungeenda kwa Makonda tu kama hukuviona vituo vya polisi.Nikiwa kama mdada mwenye uchungu na suala la kufanya mapenzi na mtu usietegemea nimeona nililete hili suala hapa.
Kule Coco Beach kuna wakaka huwa wanakodisha maboya ya kuogelea. Ukienda kukodi wanakuambia tukufundishe kuogelea, ukikubali wanakupeleka katikati ya kina cha maji ambapo unakuwa huwezi kukataa jambo lolote maana hujui kuogelea na akikuachia huwezi kumudu hayo mawimbi ya maji, basi hukulazimisha kufanya mapenzi bila hiari yako.
Unafanya naye mapenzi na kama tunavyojua kubakwa ni kitendo cha aibu huwezi kusema kokote zaidi ya kuugulia maumivu moyoni. Mbaya zaidi huwa hawavai mpira wanakufanya kavu kitendo ambacho kupata mimba au UKIMWI ni rahisi. Ni kitendo cha dakika tano lakini kinaweza kikakugharimu maisha yako yoote.
Jumamosi moja jirani yetu aligundua binti yake ana dalili za kuumwa, akampeleka hospitali akagundua ana ugonjwa wa zinaa. Jirani yule aliumia saana akaamua kuniita ili nimsaidie kumhoji binti yule kuwa imekuwaje kapata huo ugonjwa wa zinaa na binti ni mdogo yuko form three tuu shule moja hivi naihifadhi, ndipo akatupa mkasa uliompata kuwa ni vijana wanaokodisha matairi kuwa ndio waliomfanyia unyama huo.
Na mimi nikaona kabla sijaandika humu nikaona ni bora nikashuhudie nikaenda pale nikakodi mpira kijana akanisihi anifundishe ili nijue kuogelea. Tukaanza safari ya kuogelea kufika sehemu penye maji mengi nikaona yule kaka macho yameanza kuwa mekundu, mdudu ushaanza kusimama na ananilazimisha kunipeleka mbaali. Nikaanza kuvutana naye kwamba siwezi kuendelea mbele hapa pametosha. Kwa kuwa hakukuwa mbali saana na watu wako karibu na mimi ninaongea kwa sauti kubwa ndipo akaamua kunirudisha kwa kudai kuwa ni muoga tuu na siwezi kuyazoea maji.
Ombi langu kwa serikali: Kuna haja ya kuwasaidia wadada juu ya kadhia hii maana wengine hawawezi kusema na ni wake za watu wanaishia tuu kunyamaza na maumivu makali.