Serikali iingilie kati juu ya Ubakaji unaoendelea Coco Beach jijini Dar!

Kodisha mabinti wazuri (blackbelts and above/special unit etc). Waende coco kukodisha maboya. Wakifika maji marefu, jamaa akianza purukushani iki abake, binti karateka amsulubu mbakaji. Fungulia mbakaji mashtaka. Fanya hivi kila wikiendi kwa mwezi mmoja, baada ya hapo fanya randomly kwa mwaka mzima.
Kama nakuelewa hivi
 
Hebu toa mawazo yako ili tutokemeze hili janga. Kumbuka hata mwanao pia yanaweza kumkuta. Upo mkoani ndiyo ila ukumbuke dunia ni uwanja wa fujo. Kesho na keshokutwa mwanao kapangiwa chuo dar, kwahiyo tutafakari jinsi tutakavyoweza kuwakomboa hawa wanawake
Ndio maana nasema we waache tu waje kuhara humu. Siwaombei mabaya, ila kwenye issue zinazogusa jamaa directly kama hivi, tena hasa mabinti na dada zetu wadogo ambao ndio tunawaita taifa la kesho, halafu mtu anakuja kuleta masihara humu. Wanadhani ukiishi mkoani hayakukuti. Vipi kama una mke/dada/gf aliyebahatika kutembelea beach yoyote kwa safari ya kikazi, missionary au masomo, yakamkuta, halafu akakuletea maradhi nyumbani huko ambako unaamini hayatakukuta? Tafakari
 
Hii kitu ni mbaya sana,ila ushauri wangu ni kuwa kuwepo na wadada ambao watajifunza nao kuogelea iwe msaada kwa wadada au wanawake ambao watahitaji kufundishwa kuogelea,ikumbukwe hao watu wanaofundisha watu sio professional na anefundishwa kwa mila zetu ni kama yuko nusu uchi au uchi kabisa sasa matamanio hufikia mahali yanavuka mipaka na shetani nae anautumia huo mwanya na hatimaye mambo hufikia huko,haya mambo tuwaachie wazungu sisi huku kwetu bado sana..
Watasagana
 
Kwenye post yangu nimejikita kwa mabinti(ambao bado wako chini ya maamuzi na uangalizi wa wazazi), hawa ni hatari sana kupotezewa ndoto zao kama mleta mada alivyotanabaisha mfano wa aliyefanyiwa vile alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Huo ndio ulikuwa msisitizo wangu na nikasema anayestahili kuwajibishwa wa kwanza ni mlezi/mzazi wa huyo binti husika.

Kwa wale ambao wana maamuzi yao binafsi ni suala lingine pia.
Lakini dada anazungumzia ubakaji unaoendelea Coco. Maradhi na mimba zisizotarajiwa hazichagui umri wa mwanamke atakayekuwa majini. Binti anaweza kupewa ruhusa na mzazi ya kuenda beach, kuogelea na mengineyo yako chini ya binti mwenyewe anapokuwa eneo la tukio. So, hawa beach boys huchukua advantage hii kufanya ushenzi wao. Inaumiza sana, tena hasa pale unapokuwa na binti or dada anayesoma halafu yakamkuta
 
Hili eneo yusuf manji alitaka kuwekeza pesa za maana pangekuwa kama mamtoni, yaani kama miami beach,

machadema na Lissu wao wakaleta mtimanyongo, haya sasa yanawakuta,
 
Kwa kuwa hizo "sehemu kibao" hazina maboya au watu wa hivyo? Nenda Kawe Beach ndio utaelewa
za free ndio utakutana na huo ushenzi, kwanza beach zenyewe hakuna anayezijali zimejaa miba, nenda mbalamwezi uone kama utabakwa.
 
Unasema serikali haiumii? Hivi unadhani unapokuwa na nguvu kazi ya taifa (vijana) inayoongezeka maradhi, mimba za utotoni (wanafunzi ambao wengi wamesomeshwa na serikali kupitia kodi unayolipa n.k) unazungumza kwa mrengo upi? Hivi huwa mnawaza nini kabla ya kuandika? Nnda China uone wanavyolia na ageing population, wanahitaji vijana (labor force) kwa udi na uvumba ili kuijenga nchi, halafu wewe unakuja kusema serikali haiumii
Serikali haumii, ingekuwa inaumia wala ''isingefuta ajira za walimu wa arts''
Unakumbuka suala la Kagera? Kwann serikali ilichukua hela za wahanga wa tetemeko?
Ingekuwa inaumia, ingekaa kimya kuhusu suala la coco beach? Issue ya cocobeach ni muda mrefu sana.
Serikali inayoumia ni ya watu weupe tu lkn hii ya kiafrika wala haina shida na ww kbsa.
Ingekuwa inaumia ingekuwa inapiga wananchi wake mpaka kufa? Unakumbuka marehemu Mwangosi nafikiri yule mwandishi wa habari wa kujitegemea wa channel 10? Alipigwa na polisi mpaka kufa.
N.B
Serikali inayoumia ni ya watu weupe ambapo mwananchi wake hupata haki zote na siyo ya kiafrika.
Nenda ukamuulize tena aliyefuta ajira za walimu wa arts kama ameumia na vijana kuwa jobless. Kisha rudi uandike tena.
 
Kawaida polisi na vyombo vingine huchukua maamuzi pale ambapo majanga huripotiwa kama wanaliwa na hawatoi taarifa sasa jeshi litabunije kukamata watu bila uhakika, Na kwa nini watu wanalalamika haya mambo na bado mnaenda huko ?
So kama kuna janga na bado halijaripotiwa, na vyomba husika vinalifahamu, linatakiwa lisifanyie kazi tu kwa sababu halijaripotiwa rasmi. Kwani nini maana ya usalama na intelijensia? Hekima ituongoze jamani
 
za free ndio utakutana na huo ushenzi, kwanza beach zenyewe hakuna anayezijali zimejaa miba, nenda mbalamwezi uone kama utabakwa.
Sasa unadhani ni kila mtu ana uwezo wa kulipia huko unapopataja? Kumbuka mtu anakwenda kwa dhumuni la kuogelea mpaka yanapomkuta ndio anajua madhara yake. Hutegemei mtu unayemlipa kukodisha boya akakugeuka mnapokuwa majini. Tupunguze lawama kwa hawa wadada
 
Serikali haumii, ingekuwa inaumia wala ''isingefuta ajira za walimu wa arts''
Unakumbuka suala la Kagera? Kwann serikali ilichukua hela za wahanga wa tetemeko?
Ingekuwa inaumia, ingekaa kimya kuhusu suala la coco beach? Issue ya cocobeach ni muda mrefu sana.
Serikali inayoumia ni ya watu weupe tu lkn hii ya kiafrika wala haina shida na ww kbsa.
Ingekuwa inaumia ingekuwa inapiga wananchi wake mpaka kufa? Unakumbuka marehemu Ulimboka nafikiri yule mwandishi wa habari wa kujitegemea wa channel 10? Alipigwa na polisi mpaka kufa.
N.B
Serikali inayoumia ni ya watu weupe ambapo mwananchi wake hupata haki zote na siyo ya kiafrika.
Nenda ukamuulize tena aliyefuta ajira za walimu wa arts kama ameumia na vijana kuwa jobless. Kisha rudi uandike tena.
Ndugu safari itakuwia ndefu sana kama utachanganya siasa na facts. I was talking from the economic perspective. Hii ya ya kula pesa, sijui kupiga watu n.k hakuna nchi ambayo hayo mambo hayapo. tena hata hapa kwetu ni machache na kumetulia sana
NB: Ulimboka nadhani yuko hai, au ulikuwa unamtaja Mwangosi mkuu?
 
Hili sio Coco tu, ni kwenye beach zote mabo ni hayo hayo hata baadhi ya swimming pool.
hawa vijana wanongoza kwa magonjwa ya zinaa na ukimwi pia.
 
Ndugu safari itakuwia ndefu sana kama utachanganya siasa na facts. I was talking from the economic perspective. Hii ya ya kula pesa, sijui kupiga watu n.k hakuna nchi ambayo hayo mambo hayapo. tena hata hapa kwetu ni machache na kumetulia sana
NB: Ulimboka nadhani yuko hai, au ulikuwa unamtaja Mwangosi mkuu?
Ndiyo huyo Mwangosi. Unafikiri watu 30,000 wakiwa jobless na watu hao hao wakiwa na kazi unafikir hali ya uchumi inaweza kulingana? Siasa inahusika sana kwa masuala ya serikali. Kabla mtu kuwa raisi lazima uwe mwanasiasa kwanza. Hiyo reality unayoina ni kwasbb ya siasa
"Huwezi kuongelea suala la uchumi bila ya watu kuwa na kazi''
Jobless wakiwa wengi uchumi wa nchi hauwezi kukua.
Hii ya kula pesa, sijui kupiga watu n.k " hii ndiyo ni hatari sana, unafikiri familia ya Mwangosi inasaidiwa na nani kwasasa? Unafikiri angekuwepo Mwangosi unafikiri angekuwa amechangia kiasi gani km kodi au maendeleo ya nchi?
Huwezi kutaja uchumi wa nchi bila ya kuongelea watu na kazi.
 
Matukio haya yako katika Fukwe nyingi tu hapa Dar.

Tembelea fukwe zote maeneo ya Kigamboni mambo haya yanafanyika.

Swali ni je., wazazi wanashindwa kabisa kupambana na swala hili kwa kuwadhibiti, kuwaonya ama kuwatahadharisha watoto wao hadi kutaka Serikali kuingilia kati juu ya hili..!

Naomba wazazi tubebe dhamana..
 
Mbona serikali ilishafanya kamata kamata ya hao beach boys, na hii mada imeshajadiliwa mara lukuki tu humu, labda kama ni mgeni.
Ukiona hivyo, operation either haikukamilika vizuri or ilikamilika lakini beachboys wamerudi. Ila kwa uzoefu wangu wa hapo Coco, hawa boys hawajawahi kuondoka. Wanaendeleza tu ufirauni wao kwa dada na binti zetu
 
Nawe hujui kuogelea kwanini unakubali kupelekwa kwenye maji marefu???? Ya kujitakia hayana majuto, pole sana!!
Si ndio unakwenda kufundishwa? Kwanza wakati huo unakuwa hujui kuwa unapelekwa kwenye maji marefu unajikuta uko huko utafanzaje mkuu? Ni kama uko ndani ya lift unapanda ghorofani ghafla unakuta upelekwa ghorofa ya 77 kuchungulia dirishani unashangaa uko juu ya mawingu halafu aliyekupeleka anakwambia usipompa unyumba anakutosa dirishani utafanzaje?
 
Pole na hongera

Hili tatizo limeisha ongelewa sana na kulalamikiwa. Inasikitisha kwamba mamlaka husika hawachukui hatua.. Coco beach imetoka kuwa beach ya utulivu na amani na kuwa ya ujangili kwa eneo kama lile..

Inasikitisha sana sana kusoma kuwa hii kitu bado inaendelea eneo hilo..

Na humu utakuta watapita tu kusoma na kukaa kimya kama kawa.


Hivi Coco Beach na cocochanel ni ndugu?
 
Hivi Coco Beach kwa Dar unaweza ita beach nayo, waachieni wahindi wale mihogo huko, Kuna Beach nzuri na kali siyo takataka hiyo Coco, Ulizeni muambiwe Beach nzuri zenye kuvutia za kwenda kwa Dar
Acha dharau. Kwa watu wa hali ya chini, hapo ndio mapumziko yao yalipo. Au beach unazotaka kututajia bahari yake ina maji ya mvua? Kwanza mnapotosha mada
 
Back
Top Bottom