Serikali iingilie kati juu ya Ubakaji unaoendelea Coco Beach jijini Dar!

Hahahahah....wewe Wacha kuwatisha wenzako.
Sidhani kama jamaa anatishia mtu. Kwani ha bb si watu tunaoishi nao mitaani, au wanatoka sayari gani? Watu wanawafahamu ns ndio maana wanasema. Watu mnatahadharishwa na bado mnaleta masihara na kufanya mioyo kuwa migumu. Ashupazaye shingo..............!!!
 
Hapo sawa lakini kuhusu serikali kuzuia ubakaji hiyo naona tunaitwisha tu mzigo. Kuwa ya kulipia naona ni wazo zuri
Hivi kulipia na uhalifu vina uhusiano gani. Mhalifu atashindwa kulipa kiingilio anapokuwa ana dhamira yake ovu? Kama ni kuingizia serikali mapato tu nitawaelewa, ila kwa issue ya usalama si kweli. coz sidhani kama kuna beach yoyote hapa TZ ina askari wengi kama Coco na bado uhalifu unaendelea. Sasa hapo tatizo ni wananchi au hivyo vyombo vya usalama?
 
Naachilia laana juu ya wabakaji, moto uwe juu yao, tauni iharibu miili yao na mauti iwe malipo yao,
 
Hili eneo yusuf manji alitaka kuwekeza pesa za maana pangekuwa kama mamtoni, yaani kama miami beach,

machadema na Lissu wao wakaleta mtimanyongo, haya sasa yanawakuta,
So, yanawakuta waathirika ni chadema au watanzania?
 
Hahaha huyo binti na wengine wanafurahia kujamihiana(sex) huwezi kuniambia eti wanaenda cocobeach kijifunza kuogelea, huo ni uongo. Wanajifunza kuogelea siku moja tu tena cocobeach?! Ili iweje kwani wanaishi mto msimbazi kwamba wanajiandaa kwa mafuriko?!
Kuna wasichana siku za sikukuu husafiri kutoka mwanza,musoma, na bukoba kuja Dar nao wanaenda cocobeach kujifunza kuogelea hahaha.
Kuna mabinti huenda kwenye matamasha cocobeach na kutaka mafunzo ya kuogelea siku hiyo hiyo hahaha.
Wanajifunza kuogelea cocobeach ili waende wapi?! Kwenye olympic au ili iweje?!
Mleta mada angeomba watoa mafunzo ya uogeleaji cocobeach wawe na condom za kutosha. Binti mwenyewe aliuchuna wao kufukunyua mambo ya watu tu.
 
Kuna watu humu wanamuhusudu sana makonda kua ndio solution ya hilo
"Eti makonda akiskia atawanyorosha" unazani hafahamu lolote hiyo situation hawezi kuizuia huyo bwana maana wale jamaa ni competent vibaya mno

Wapuuzi ni wanawake acha waendelee kufanywa
 
Nikiwa kama mdada mwenye uchungu na suala la kufanya mapenzi na mtu usietegemea nimeona nililete hili suala hapa.

Kule Coco Beach kuna wakaka huwa wanakodisha maboya ya kuogelea. Ukienda kukodi wanakuambia tukufundishe kuogelea, ukikubali wanakupeleka katikati ya kina cha maji ambapo unakuwa huwezi kukataa jambo lolote maana hujui kuogelea na akikuachia huwezi kumudu hayo mawimbi ya maji, basi hukulazimisha kufanya mapenzi bila hiari yako.

Unafanya naye mapenzi na kama tunavyojua kubakwa ni kitendo cha aibu huwezi kusema kokote zaidi ya kuugulia maumivu moyoni. Mbaya zaidi huwa hawavai mpira wanakufanya kavu kitendo ambacho kupata mimba au UKIMWI ni rahisi. Ni kitendo cha dakika tano lakini kinaweza kikakugharimu maisha yako yoote.

Jumamosi moja jirani yetu aligundua binti yake ana dalili za kuumwa, akampeleka hospitali akagundua ana ugonjwa wa zinaa. Jirani yule aliumia saana akaamua kuniita ili nimsaidie kumhoji binti yule kuwa imekuwaje kapata huo ugonjwa wa zinaa na binti ni mdogo yuko form three tuu shule moja hivi naihifadhi, ndipo akatupa mkasa uliompata kuwa ni vijana wanaokodisha matairi kuwa ndio waliomfanyia unyama huo.

Na mimi nikaona kabla sijaandika humu nikaona ni bora nikashuhudie nikaenda pale nikakodi mpira kijana akanisihi anifundishe ili nijue kuogelea. Tukaanza safari ya kuogelea kufika sehemu penye maji mengi nikaona yule kaka macho yameanza kuwa mekundu, mdudu ushaanza kusimama na ananilazimisha kunipeleka mbaali. Nikaanza kuvutana naye kwamba siwezi kuendelea mbele hapa pametosha. Kwa kuwa hakukuwa mbali saana na watu wako karibu na mimi ninaongea kwa sauti kubwa ndipo akaamua kunirudisha kwa kudai kuwa ni muoga tuu na siwezi kuyazoea maji.

Ombi langu kwa serikali: Kuna haja ya kuwasaidia wadada juu ya kadhia hii maana wengine hawawezi kusema na ni wake za watu wanaishia tuu kunyamaza na maumivu makali.
Pole sana! Ubakaji ni kosa la jinai na hapa sina nia ya kuwatetea wanaofanya hivyo! Sijui unataka serikali ifanyaje sasa,iwe inaogelea na nyie mnapofundishwa au iwaondoe hao vijana hapo! Kama wataondolewa manake hapatakuwa na watu wa kufundisha kuogelea hapo na kwahiyo itabidi wanaotaka kujifunza watafute namna nyingine salama na inayoeleweka ya kujifunzia. Nadhani inabidi ninyi mnaojipeleka kwa hao vijana mtafute sehemu zingine za kujifunzia tofauti na huko baharini. Vinginevyo kaendeleeni kubakwa tu manake hamna akili
 
Daah!! Pole sana aisee..kwan kuna beach moja tu DSM???
Njoo huku kwetu mbagala kuna beach matope utajua kuogelea bila shida.....
 
Kuna watu humu wanamuhusudu sana makonda kua ndio solution ya hilo
"Eti makonda akiskia atawanyorosha" unazani hafahamu lolote hiyo situation hawezi kuizuia huyo bwana maana wale jamaa ni competent vibaya mno

Wapuuzi ni wanawake acha waendelee kufanywa
Hahaha kufanywa kwao ni kawaida, labda useme hawampendi mfanyaji. Ukiwauliza wao watakwambia ukweli, hapo tatizo ni magonjwa yatokanayo na tendo hilo ila sio tendo.
Wengine wanatoka Dodoma kuja cocobeach wafundishwe kuigelea hahaha. Mafunzo ya siku moja tu hahaha usicheze na hao viumbe.
Anaweza akapiga yowe ukadhani anauwawa ukaenda kutoa msaada, wewe ndio utaonekana mjinga. Acha wapate mafunzo labda tutapata gold medal ya kuogelea next olympic tournament.
 
Hahaha mbona hata vyangudoa hulalamika wanabakwa kisa hakulipwa walivyokubaliana. Mimi hawa wakilalamika huwa naaproach with extrime caution.
 
Nikiwa kama mdada mwenye uchungu na suala la kufanya mapenzi na mtu usietegemea nimeona nililete hili suala hapa.

Kule Coco Beach kuna wakaka huwa wanakodisha maboya ya kuogelea. Ukienda kukodi wanakuambia tukufundishe kuogelea, ukikubali wanakupeleka katikati ya kina cha maji ambapo unakuwa huwezi kukataa jambo lolote maana hujui kuogelea na akikuachia huwezi kumudu hayo mawimbi ya maji, basi hukulazimisha kufanya mapenzi bila hiari yako.

Unafanya naye mapenzi na kama tunavyojua kubakwa ni kitendo cha aibu huwezi kusema kokote zaidi ya kuugulia maumivu moyoni. Mbaya zaidi huwa hawavai mpira wanakufanya kavu kitendo ambacho kupata mimba au UKIMWI ni rahisi. Ni kitendo cha dakika tano lakini kinaweza kikakugharimu maisha yako yoote.

Jumamosi moja jirani yetu aligundua binti yake ana dalili za kuumwa, akampeleka hospitali akagundua ana ugonjwa wa zinaa. Jirani yule aliumia saana akaamua kuniita ili nimsaidie kumhoji binti yule kuwa imekuwaje kapata huo ugonjwa wa zinaa na binti ni mdogo yuko form three tuu shule moja hivi naihifadhi, ndipo akatupa mkasa uliompata kuwa ni vijana wanaokodisha matairi kuwa ndio waliomfanyia unyama huo.

Na mimi nikaona kabla sijaandika humu nikaona ni bora nikashuhudie nikaenda pale nikakodi mpira kijana akanisihi anifundishe ili nijue kuogelea. Tukaanza safari ya kuogelea kufika sehemu penye maji mengi nikaona yule kaka macho yameanza kuwa mekundu, mdudu ushaanza kusimama na ananilazimisha kunipeleka mbaali. Nikaanza kuvutana naye kwamba siwezi kuendelea mbele hapa pametosha. Kwa kuwa hakukuwa mbali saana na watu wako karibu na mimi ninaongea kwa sauti kubwa ndipo akaamua kunirudisha kwa kudai kuwa ni muoga tuu na siwezi kuyazoea maji.

Ombi langu kwa serikali: Kuna haja ya kuwasaidia wadada juu ya kadhia hii maana wengine hawawezi kusema na ni wake za watu wanaishia tuu kunyamaza na maumivu makali.

Mwaka mpya nilipitia maeneo ya cocobeach nilivutiwa na wingi wa watu, nikaona hebu niende pamoja na mambo mengine nifanye kautafiti ili kuona kama kweli hivi vitendo vinafanyika au la. Nilifika pale nikajumuika na kuwa miongoni mwa kundi kubwa. Jambo linalowafanya wadada wengi wapateshida ya kurubuniwa na wahuni wa cocobeach kwa utafiti mdogo nilioufanya ni USHAMBA. Dada mmoja ambaye alikuwa amejaliwa mwili alifika eneo hilo na kubadilisha nguo ambapo alibaki na nguo ya ndani. Baada ya muda kidogo alienda kwenye wakodisha maboya na kukodisha kwa sh.1000. Alielekea kwenye maji na boya lake ambapo kijana mmoja ambaye alikuwa amevaa boxer laini alimfuata na kumuelekeza namna ya kuogelea. yule dada alionyesha kukataa ila baada ya muda akawa amekubali na kujaribu kuogelea ila kwa shida maana maji yalikuwa ndiyo yanajaa na mawimbi ni makubwa na kwa kuwa sio mzoefu kila mara alipigwa na wimbi maana hakuwa anajua jinsi ya kuyakwepa. Kijana aliyekuwa anajaribu kumfundisha alikuja na boya pana ambalo kipenyo chake kinaweza kupitisha watu wawili, kijana alijivika huku akijifanya ni msamaria mwema anajaribu kumfundisha, hawakusogea mbali niliona dada yule akijinasua na kwakuwa watu walikuwa karibu ikabidi alazimishe kutoka kwenye maji ina kijana kiungo chache cha uzazi kikiwa kimesisimka sentimita zote loooh. Ila wengi wanaohadaiwa ni washamba!!! kwa dada wa mjini sio rahisi labda apende mwenyewe
 
Mimi nauangalia huu mkasa kama Fursa kwa wadada, Wajitokeze wadada wajasiriamali wanaoweza kuogelea vizuri wafanyie kazi hili tatizo kwa kuleta Maboya yao wenyewe na wawe wanawatu wa kuwatrain wasiojua, hii nadhani itakuwa fursa mojawapo ya kinadada kuongeza kipato na itapelekea kupungua kwa haya majanga.
 
Coco beach polisi wamejaa kila kona tatizo mkibakwa hamripoti sasa mnataka serikali iwasaidie vipi?
Ushauri wangu usikubari kuingia kwenye maji na mtu usiyemfahamu na kumwamini maji ni kitu kingine hata akitaka tigo utampa tu nini k!
Tatizo la polisi kanzu wa pale concentration yao sana ipo kwenye magari ya watu binafsi maana wanajua humo ndo watu wanafanya ufuska sana, huko kwengine kama wanapapotezea.
 
Hufundishwi bure. Unalipia boya, then unaulizwa kama unataka kuogelea mwenyewe or usaidiwe. Na kwa vile hujui kuogelea na pia hujui dhamira yao, unawakubalia tu wakusaidie since unahitaji kuogelea. Knachohitajika hapa ni awareness creation na mamlaka zijitambue
Kumbe unatoa helaa ufundishwe ilii upigwe na mkurukumba..!! Ha ha..daah
 
Kifupi kitendo cha kubaka ni kosa la jinai. Tatizo ni nyie kina dada kwa nini msitoe taarifa polisi?? Iliwattuhumiwe wakamatwe? Ushahidi si mnao? Sababu akishafungwa mmoja wao miaka 30 basi watakoma kufanya hivyo. Unaposema hamuwezi kusema kokote zaidi ya kuugulia maumivu moyoni hilo ndilo kosa lenu. Matatizo katika jamii hayawezi kutatuliwa namna hiyo. Kuweni majasiri na hata leo bado mnaweza kuwafungulia mashtaka.
 
Niombe kutoa Taarifa zenye mfanano na hizo
Kwanza Mimi ni m/kiti wa shina no 4
Ilemela Mtaa Igombe B
Mwaka 29
017 ulikuwa Mwaka mgumu kwangu na kiongozi mwenzangu wa shina Jirani ,Huku kwetu kuliibuka Tatizo la Vijana wenye umri 18_24 kuwa na kikundi cha uharifu wa aina mbalimbali ikiwa ubakaji ukwapuaji wa Simu smart phones wizi wa betery za solary na sola zenyewe ,hatukupendezwa na tabia hiyo tulianza harakati za kuhakikisha ysalama wa Jamii tunazoongoza pia kuwashauri Vijana kuepusha na tabia Hizo hatari niliwasilisha majina Polisi walipoazimia kuniangamiza Mimi na familia yangu nilipata Habari kuwa wangetumia kila njia kuniangamiza nikiwa njiani au nyumbani pia nilipata taarifa kuwa kulikuwa na mkakati wa kunichomea Ndani ya nyumba Usiku na familia yangu ,ili fikia hatua mmoja wao kunifuata kwangu saa 7 Usiku kama kujisalimisha alitaja wenzake wengi na akasema walikuwepo baadhi ya Wazazi walikuwa nyuma ya Mpango wa kuniangamiza kutokana na kuwa niliingilia Shughuli inayolisha familia zao ,Kiongozi wa Mtaa Wetu aliita Baadhi ya Vijana walikiri kuwa ni waharifu sugu na wakaahidi kuachana na uharifu na waliahidi kunilinda Mimi na famulia yangu ili Mradi wasipelekwe Polisi na kila kila mmoja alijieleza kwa maandishi aliosaini,unafuu ulikuwe hadi Sikukuu zote leo Jioni Nimepata taarifa kuwa wazazi wameibua hoja ya kunifanyizia tena eti Vijana wao wanasakamwa na Polisi kutokana na Mimi wakati sijakutana na Polisi kwa mwaka huu baadhi ya Wazazi ni watu ambao pia ni Viongozi hivyo naiarfu Polisi hasa kamanda wa Mkoa Mwanza na OCD Ilemela na wote wapendao Amani na wanachukia Uharifu ikitokea ni mashirika au familia yangu ikadhulika Vijana hao na Wazazi wao Ndio wahusika wakiongozwa na Abel Grevaz ,Lutumbi ni wazazi Vijana Baadhi ni Frank Abel,Mabura na Allan na wenzao
Pia naomba Ushauri je niache Uongozi au mnani shaurije wana jf
 
Pole sana dada'ngu. Mimi ni mkazi karibu kabisa na hapo Coco Beach. Hawa jamaa tunawafahamu kwa sura mpaka majina. Hata askari hapo wa doria hilo eneo wanafahamu kinachoendelea. Nathubutu kusema wanapuuzia tu. Huwa wanakamata wale watu wanaofanya mapenzi kwenye magari na kule mapangoni karibu na upande wa Police Mess coz huwa wanahongwa na wakamatwaji

Huu ubakaji huwa unafanyika zaidi nyakati za asubuhi (midday) mpaka mida ya saa 10 jioni watu wanapoanza kujaa then wanaacha coz watu wanakuwa wengi sana. Mwaka 2013 nilishachunguza kwa kuwazoea na kuwa nakaa nao kwenye 1 ya vibanda vyao (coz kama sio 1 wao hawakuruhusu ukae nao muda mrefu) na huwa wanapigiana stori ya kila baada ya tukio wanalofanya (kuelezea mwanamke yukoje, ana ladha gani, alimlazimishaje mpaka akakubali n.k).

Ni kweli kama anavyosema huyu dada, kuwa wakimaliza huwa wanachukua tu nguo zao (coz huziacha vibandani kwenye mifuko wakiingia kwenye maji) na kujiondokea na maumivu moyoni na mwilini. Mabinti wadogo ndio huwa waathirika zaidi coz wao ndio huwa wanapendwa zaidi na ni rahisi zaidi kutishiwa.

Mamlaka husika zichukue hatua kali za kisheria, la sivyo mimba za utotoni, wanafunzi na kuenea kwa maradhi hakutaacha kuisha. Watu waache kutoa comments za kejeli hasa kwenye mambo ya msingi kama haya. Kuna kesho, unaweza kukuta ni mkeo or dada yako or hata g/f wako amefanyiwa hivi. Mwisho wa siku kama ni maradhi ukaletewa ndani ya nyumba.

Naomba kuwasilisha
Ninyi watu wa ajabu.
Yaani hao wabakaji mnawafahamu kwa majina na sura, na mnasikia wanavyosimulia na muda wanaofanya huo upuuzi mnaujua halafu hamchukui hatua yoyote,,,,,, mnataka nni sasa kama ninyi tu mko kimya, hii ni aibuuuu
 
Back
Top Bottom