Serikali iimulike CRDB Bank. Inadhulumu wateja kwa kiwango cha ajabu

Bank ya CRDB ina makato ya hovyo na ya ajabu .
Yaani hii benki unaweza kukatwa kila siku elfu 10 bila kujua.
Wanakaa wanakata tu 1500, ukizubaa kidogo wanakata 3000 ukishangaa kidogo wanapita na sh. elfu 2, . Ukicheki statement wanaandika tu imelipwa. Bila kutaja umemlipa nani na kwa malengo yapi.
Hii benki inayojitapa kupata faida za mabilioni kwa mwaka kumbe ni faida za makato ya hovyo.
Haiwezekani waandike tu imelipwa bila kutaja nani kalipwa na kalipwa kwa malengo yapi.
Huu ni utapeli..
Vitu vidogo vidogo kama hivi ndivyo vinapelekea vijana kutokuwa wazalendo kwa Taifa lao.
Mamlaka za udhibiti za Tanzania hazipo kwaajili ya mteja (mlaji)
Wakigundua kampuni au taasisi imedhulumu haki ya mlaji wanaipiga faini ambayo inaingia kwenye mfuko wa mamlaka husika na si kwa mwathirika.
Banana republic, na risti hawatoi, ukienda Sim-banking unambiwa kuna changamoto ya internet, inakamua kumeza tu
 
2022 nilifungua account nmb ila sikurenew 2024 sasa leo nimekaa nimetumiwa message kama inavoonekana

TZS 4859.41 imetolewa kwenye akaunti inayoishia na 2..39 tarehe 13-05-2026 12:59. Kama hutambui muamala huu piga 0800002002. NMB Karibu yako

Nikakaa nikajitafakari nikasema kama hawa wamechukua kwenye account moja kiasi hicho je wamefanya hivo kwa account ngapi?

Kila sehemu ni wizi tuu
 
Mimi bank napitishia mshahara tu, yani SMS ya salary ikiingia saa 12:40 mimi saa 12:42 tayari mzigo wote nimeshauhamishia kwenye lipa namba yangu

Yan nikijisahau hela ikilala siku moja tu nakuta transaction zaidi ya kumi zimeshatoka kurudi bank
 
Bank ya CRDB ina makato ya hovyo na ya ajabu .
Yaani hii benki unaweza kukatwa kila siku elfu 10 bila kujua.
Wanakaa wanakata tu 1500, ukizubaa kidogo wanakata 3000 ukishangaa kidogo wanapita na sh. elfu 2, . Ukicheki statement wanaandika tu imelipwa. Bila kutaja umemlipa nani na kwa malengo yapi.
Hii benki inayojitapa kupata faida za mabilioni kwa mwaka kumbe ni faida za makato ya hovyo.
Haiwezekani waandike tu imelipwa bila kutaja nani kalipwa na kalipwa kwa malengo yapi.
Huu ni utapeli..
Vitu vidogo vidogo kama hivi ndivyo vinapelekea vijana kutokuwa wazalendo kwa Taifa lao.
Mamlaka za udhibiti za Tanzania hazipo kwaajili ya mteja (mlaji)
Wakigundua kampuni au taasisi imedhulumu haki ya mlaji wanaipiga faini ambayo inaingia kwenye mfuko wa mamlaka husika na si kwa mwathirika.
Wanafuata maelekezo ya Chama lako pendwa
 
2022 nilifungua account nmb ila sikurenew 2024 sasa leo nimekaa nimetumiwa message kama inavoonekana

TZS 4859.41 imetolewa kwenye akaunti inayoishia na 2..39 tarehe 13-05-2026 12:59. Kama hutambui muamala huu piga 0800002002. NMB Karibu yako

Nikakaa nikajitafakari nikasema kama hawa wamechukua kwenye account moja kiasi hicho je wamefanya hivo kwa account ngapi?

Kila sehemu ni wizi tuu
kiongozi kwa takriban miaka mitatu, wamekata 4859.41 ya uendeshaji wa account yako hiyo ni wastani wa shs 200 kwa mwezi... Hayo makato yapo na unajulishwa wakati unafungua account.
Ila ukitaka usikatwe hayo makato, unafungua fixed account.
Hata sasa unaweza kuwaambia wahamishie pesa zako kwa fixed account na hutakatwa makato yoyote.
 
kiongozi kwa takriban mitatu, wamekata 4859.41 ya uendeshaji wa account yako hiyo ni wastani wa shs 200 kwa mwezi... Hayo makato yapo na unajulishwa wakati unafungua account.
Ila ukitaka usikatwe hayo makato, unafungua fixed account.
Hata sasa unaweza kuwaambia wahamishie pesa zako kwa fixed account na hutakatwa makato yoyote.
Sawa Afisa wa benki
 
CRDB ni wezi mno makato yao ya kipumbavu mno. Wanakata jinsi wanavyojisikia. Ukiangalia statement makato yanaandika "Annual card fee" halafu inakatwa mara 3 kwa siku moja hadi 15000 huu ni wizi uliopitilizq.
 
Back
Top Bottom