Serikali ifanye usafi kwenye mitaro, wananchi wachafue!

Serikali ifanye usafi kwenye mitaro, wananchi wachafue!

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,324
Reaction score
2,494
Nimesikiliza idhaa ya Kiswahili ya BBC asubuhi hii nikasikia wakazi wa Buguruni DSM wakilalamika kuwa wanatoa pesa lakini serikali haifanyi usafi kwenye mitaro.

Maswali ya kujiuliza;

Kazi ya wananchi ni kuchafua hiyo mitaro kwa kutupa taka ovyo, kutiririsha kinyesi, n.k. ili serikali ikasafishe?
Mlipuko wa magonjwa ukija serikali ndiyo inapata athari kiafya?
Je, jukumu la usafi ni la serikali ama wananchi?

Kama wananchi wanatoa michango ili mitaro wanayoichafua isafishwe na serikali, basi serikali itoe kiasi hicho hicho wanachotoa wananchi, iwape wajifanyie usafi wenyewe katika hiyo mitaro yao.

Karibu kwa mjadala.
 
Sikuwasikia hao wananchi lkn kwenye suala la usafi pande zote zinawajibika. Mamlaka husika zinapaswa kuweka vifaa vya kutosha vya kuhifadhia taka ktk maeneo ya umma na kuhakikisha taka zinasombwa kwa wakati.

Kama huduma hiyo haipatikani wananchi wanaishia kutupa taka ovyo. Wakati huo huo wananchi nao wanawajibika kwa sbb wapo ambao hawajali. Utamuona mtu yupo kwenye gari anarusha uchafu barabarani. Hiyo tabia nayo muhimu ikomeshwe.
 
Back
Top Bottom