Serikali idhibiti ongezeko la Wachina nchini

Tango73

JF-Expert Member
Dec 14, 2008
1,677
1,195
Baada ya kufa kwa ukomunisti duniani, China inawatupa kwa nguvu wanavijiji wake{proleretariants) barani Africa. Hawa wachina ni wale jamii ya watu waliojulikana kama proleretariants au walala hoi wasio na elimu na uwezo wa kumiliki mali. Wengi wao elimu yao wameishia darasa la nne. Watu hawa hivi sasa ni mzigo mkubwa sana kwa serikali ya China hivi sasa ndio maana inawatupa kijanja katika nchi za Africa.

Zambia wamelalamika nusura ya kuandamana kwa sababu wachina hawa wanafanya kazi za raia wao masikini kama vile kuuza maandazi, korosho na ubwabwa mitaani. Serikali isipowaangalia wachina hawa itakuja kujutia miaka ya 2090 maana watafikia uwezo wa kumiliki ardhi na raia wetu kubakia wapagazi wao.

Kuna kipindi nilikuwa China kikazi, nikabahatika kumuuliza Balozi wetu wa Tanzania huko, kwa wakati huo kwa nini wanatoa viza kwa wachina kuja Tanzania kama ubuyu?.

Yule balozi alinijibu kwamba ukiwaminya kuja nchini basi na serikali yao inabania viza za Wafanyabiashara wetu kwenda huko, akanipa mfano Waziri Nyalandu wakati huo alipoendesha zoezi la kuwafagia Wachina Kariakoo, China ilirespond kwa kuminya idadi ya viza za wafanyabiashara wetu!.
Balozi akaniambia kuwa, tatizo pia liko kwa taasisi nyingine za serikali ambazo kwa rushwa zinatoa vibali mbalimbali na nyaraka muhimu.

Na Wachina ni wajanja, wakifika wanatafuta vibali na documents zote zinazohitajika hata kwa Rushwa, kiasi kwamba ukitaka kumrudisha wanalalamika kwamba wameonewa na hivyo kuibua mgogoro wa kidiplomasia!

Hata hivyo nilimtahadharisha balozi kwamba, Iwapo mtaendelea kutoa viza kama njugu, na iwapo serikali Itaendelea kuwa corrupt katika taasisi za vibali, basi tutajikuta nchi hii baada ya miaka 50 kuna demographics tofauti kabisa na tulivyo sasa, Wachina watakuja, watazaa na Watanzania, Watoto wao watakuwa watanzania, watamiliki ardhi, wataingia bungeni na huwezi jua loyalty yao itakuwaje?

China inajaribu kutumia muscle yake ya kiuchumi kutapanya watu wake, kama leo unavyoona Singapore kuna Chinese ethnic people kibao, Malaysia na nchi nyingi za Asia, hawa huwa bado wanaitizama China kama motherland.

Ukitaka kufahamu akili ya China, kuna kisa cha kweli ambapo wakati Marekani inafanya mazungumzo ya kurejesha mahusiano ya Kidiplimasia na Marekani, Mao ZeDong ( Mao Tse Tung) alipendekeza kwa Raisi Nixon, China ipeleke mamia ya mabinti marekani kama gesture ya urafiki mpya, lakini Nixon alikataa hili wazo kistaarabu. Ni dhahiri Mao hapa alikuwa anapiga mahesabu ya mbali.

Kiufupi ni hivi:
Serikali itoe viza chache kwa wachina wasio wawekezaji kuja nchini, pili ihakikishe Ina Computerize mifumo ya Kutrack Wageni,
Tatu ihakikishe Mgeni hatoi pesa benki, Hapati huduma ya malazi gesti au hotelini mpaka atoe Passport yenye viza halali.
Nne ni lazima serikali iandae operations za kuwakumbusha ( japo kiakili) kwamba wageni bado ni wageni wasijisahau, Operations hizo ni kama kuwauliza waonyeshe passport zao, kama ziko poa basi ok, lakini kama haziko vizuri wawe deported.

Kule Guangzhu kwenye waafrika wengi, shurti mgeni atembee na Pasipoti, na hupati huduma yoyote mpaka uwe nayo, na wakati wowote polisi anaweza kukuuliza umuonyeshe passport yako!

Tusikubali umasikini wetu ukatupeleka kuuza identity ya Nchi, mchina ukimuachia utajikuta miaka 100 ijayo wako asilimia 40 ya population nzima, Wenzetu wako strategic!
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,643
2,000
Mwigulu Nchemba hili la kudhibiti wahamiaji haramu nchini na hasa hawa Wachina limemshinda kabisa. Wachina wanaingia nchini kwa idadi kubwa sana na hali hii ikiachwa iendelee na hasa tukitilia maanani wingi wa hawa jamaa duniani basi miaka 15/20 ijayo hawa jamaa wanaweza kuwa wengi kuliko wazawa.
Hahaaaa...ndo maana Trump anataka kujenga ukuta!
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,643
2,000
Hawa jamaa aisee wanaingia nchini kwa wingi sana. Na idadi yao kwao tu wako 1.4 billion hujaweka na wengine nchi nyingine. Serikali isipokuwa makini hawa jamaa wataitawala Tanzania miaka michache ijayo halafu jamaa hawa wana roho mbaya sana.
Yeah..wahamiaji haramu ni haramu tu.

Binafsi sijui nchi yoyote ile isiyowachukulia hatua wahamiaji wa namna hiyo.

Jaribu wewe kuhamia China kiharamu uone.

Unaweza kunyongwa....hahahaa.

But seriously, uhamiaji haramu si mzuri. Hata Mexico hukamata na kuwarudisha makwao wahamiaji haramu.

Serikali inapaswa kuchukua hatua thabiti za kukabiliana na hilo tatizo.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
101,752
2,000
Unaona eeh! Halafu jamaa wanafanya mambo mbali nchini ya kuvunja sheria za nchi.

Yeah..wahamiaji haramu ni haramu tu.

Binafsi sijui nchi yoyote ile isiyowachukulia hatua wahamiaji wa namna hiyo.

Jaribu wewe kuhamia China kiharamu uone.

Unaweza kunyongwa....hahahaa.

But seriously, uhamiaji haramu si mzuri. Hata Mexico hukamata na kuwarudisha makwao wahamiaji haramu.

Serikali inapaswa kuchukua hatua thabiti za kukabiliana na hilo tatizo.
 
Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,011
2,000
Mwigulu Nchemba hili la kudhibiti wahamiaji haramu nchini na hasa hawa Wachina limemshinda kabisa. Wachina wanaingia nchini kwa idadi kubwa sana na hali hii ikiachwa iendelee na hasa tukitilia maanani wingi wa hawa jamaa duniani basi miaka 15/20 ijayo hawa jamaa wanaweza kuwa wengi kuliko wazawa.

Kweli kabisa.. kwa hili Mh. Mwigulu kafeli kabisa.. hata yeye Mh. Mwigulu siku moja niliona humu JF AKILALAMIKA, ETI ALIKUTANA NA WACHINA CARGO AIRPORT, WAKICHUKUA MIZIGO HAWANA HATA PASSPORT ILA WANA VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA NADHANI.. na akatoa amri wafuatiliwe... sijasikia lolote from there..

Pili, Mh. Mwigulu, alikiri wachina kumkimbia ktk gereza moja ktk mgodi ule mchina alimpiga mtanzania kinyama sana, alisema, alipofika, mgodini, wachina walikuwa wengi na kuruka ukuta na kukimbia mbele yake... kumbe walikuwa mgodini kinyemela..

Ushauri wa haraka sana kwa Mh. Mwigulu..

Wachina ni hatari sana nchini kwa sasa, na nchi nyingi barani Afrika.. nilitegemea kabisa kutokana na matukio hayo mawili yaliyokukuta ww kama Waziri mwenye dhamana ya ulinzi wa raia na mali zao, ikiwemo kudhibiti wahamiaji haramu, UNGEWASAKA HAWA WACHINA, WAMEZAGAA SANA MITAANI, WANAFANYA KAZI ZA KIMACHINGA SANA, NA VITU FEKI VINGI WANATENGENEZA, hata ww unajua, wachina ni feki sana, UMENIANGUSHA SANA Mh. Waziri, nina imani na ww, ila imepungua sana sana..

Wachina wanaokuja kwa ajili ya UJENZI MBALIMBALI KTK CONTRACTS NA WAKIMALIZA WANARUDI KWAO HAO HAKUNA SHIDA.. ILA HAWA WENGINE WACHINA MACHINGA, NI HATARI SANA SANAAAAAAAAAA...

Mh. Waziri Mwigulu, hili limekushinda kabisa.. niwe muwazi tu.. act now..!! plse..

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
7,115
2,000
Baada ya kufa kwa ukomunisti duniani, China inawatupa kwa nguvu wanavijiji wake{proleretariants) barani Africa. Hawa wachina ni wale jamii ya watu waliojulikana kama proleretariants au walala hoi wasio na elimu na uwezo wa kumiliki mali. Wengi wao elimu yao wameishia darasa la nne. Watu hawa hivi sasa ni mzigo mkubwa sana kwa serikali ya China hivi sasa ndio maana inawatupa kijanja katika nchi za Africa.

Zambia wamelalamika nusura ya kuandamana kwa sababu wachina hawa wanafanya kazi za raia wao masikini kama vile kuuza maandazi, korosho na ubwabwa mitaani. Serikali isipowaangalia wachina hawa itakuja kujutia miaka ya 2090 maana watafikia uwezo wa kumiliki ardhi na raia wetu kubakia wapagazi wao.

Ni kweli, mkuu.
 
24hrs

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
2,599
2,000
Wagumu kutoa hela sijawahi ona jamani nina best yangu yupo Mbezi beach alikuja Tz toka August. Hawajui hata kiswahili na wamesajili na namba zao. Jaman hii ni hatari, ukimuuliza anafanya kazi gani mnagombana hatari
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,404
2,000
Tumenunua Dreamliner inakuja 2018 kwa ajili ya safari za moja kwa moja China. Hao ndio wawekezaji wenyewe tuliowavutia ba wengine ni watalii
 
tozi25

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
5,919
2,000
Wapi kwenye hiyo massage mkuu?
Mkuu siwezi kuitaja kuna siku nilitoa location ya kupata papuchi za kidosi kumbe kulikuwa na usalama wa taifa wakaharibu mambo. tena walinifata PM dadeki zao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom