uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,424
- 1,966
Amani kwenu wana jamvi,
Nimetafakari sana nikaona kupitia jukwaa hili nipeleke ombi kwa serikali juu ya kiinua mgongo kwa wastaafu. Nikiri wazi kuwa mimi ni mfanyakazi kwenye makampuni ya watu binafsi, nimeshuhudia watu wakistaafu miaka ya nyuma na wengine waliostaafu miaka ya hivi karibuni ikiwemo mwaka huu baada ya sheria kubadilishwa.
Kule nyuma kulikuwepo kiinua mgongo kilitajwa kwenye sheria ya kazi, nakumbuka yakafanyika marekebisho
kutoka viwango vilivyokuwepo mpaka kikawekwa mstaafu kulipwa kiwango cha mshahara wa siku saba kwa kila mwaka.
aliofanyakazi kwa muda usiozidi miaka kumi hata kama umetumika zaidi ya miaka kumi,ikiwa na maana unalipwa siku sabini kama kiinua mgongo. Baadaye yakafanyika marekebisho mengine,hizo siku saba nazo zikafutwa kwenye sheria kwa maelezo kwamba mwajiri.
Anamchangia mfanyakazi kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii na hivyo akistaafu atapewa mafao yake huko.
Jambo hili limeendelea kufanyika hivyo hasa kwenye makampuni yetu yanayotegemea sheria za nchi zinasemaje,
sheria ikileta neema mnaneemeka ikileta balaa mnalipata, ilimradi ni kwa mujibu wa sheria.
Mshangao wangu namba moja ni huu,mtumishi anaitumikia kampuni kwa uaminifu, anastaafu kwa heshima
anaambiwa nenda kwa amani, utapata haki yako kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii. Na mtumishi mwingine anaenda kinyume na maadili anafukuzwa kwa mujibu wa sheria, huyu haagwi wala kuambiwa neno lolote la heri, lakini wanakutana na aliyeagwa kwa maneno ya heri kibao wote wanakutana kwenye benchi moja la mfuko wa hifadhi ya jamii kupata iliyo haki yao.
Mshangao wangu namba mbili, ni kwamba kwa sasa mifuko ya hifadhi ya jamii haitoi hayo mafao kwa wastaafu kwa wakati. watu wanakaa miezi tisa na kuendelea bila ya kupata chochote,huku hawana mshahara, maana wameishatoka kweye pay rolls za kampuni zao na hakuna fedha yoyote waliyopewa kama kiinua mgongo cha kuwasaidia wakati wanasubiri mifuko ya hifadhi ya jamii kufanya kazi zao. Matokeo yake utakuta pale kwenye benchi la ufuatiliaji wa mafao, aliyefukuzwa kazi au kwa kula rushwa au kuiibia kampuni iwe mali au muda kwa kwenda kwenye mishe zake ana hali bora kuliko mstaafu aliyestaafu kwa heshima. Hili jambo linaacha urithi mbaya kwa jamii.
Nihitimishe kwa kushauri,serikali irejeshe kisheria,fao la kiinua mgongo. Kama itaonekana linaongeza mzigo kwa wenye makampuni, basi ile fedha ya maafa anayotoa (WCF) ambayo mwajiri anamlipia kila mfanyakazi kila mwezi,endapo mfanyakazi huyo atafikia muda wa kustaafu bila kupatwa na maafa, basi serikali impatie sehemu ya ile fedha kama sehemu ya kiinua mgongo. Ili kumpunguzia makali ya kukosa mshahara na mafao muda wa miezi hiyo ya kusubiri.
Naomba kuwasilisha,
Kama una maoni zaidi unaweza kuongezea ili kuboresha.
lengo ni kwamba tujenge mfumo wa kuwafanya watumishi kufanyakazi.
kwa weredi na uaminifu wakijua hata wakistaafu hawataenda kuadhirika. Lakini pia kuwarithisha vijana
imani ya kwamba ukitumika kwa uaminifu unatunzwa, badala ya kushuhudia baba/ mama zao wakivuna mabaya
kwa utumishi wao uliotukuka.