Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ilala amepinga vikali kuapishwa kwa mwenyekiti wa mtaa wa segera-Migombani kulikofanywa na wakili binafsi, akisema kuwa ni ubabaishaji na kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Kauli hii imekuja Siku moja baada ya wananchi wa mtaa huo wa Migombani jijini Dar es Salaam kuchukua dhamana ya kumuapisha mwenyekiti wao kwa kutumia wakili binafsi.

Wakati Mkurugenzi huyo wa Ilala akitoa kauli hiyo, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Segerea, Gango Filemon Kidera amebainisha kuwa wananchi wataendelea kupata huduma za kiserikali kutoka ofisi hiyo kama inavyotakiwa kwani kilichofanywa kilikuwa wazi na kilizingatia sheria za nchi na si batili kama inavyozaniwa.

“Tunasubiri tuone mkurugenzi anataka kumuweka nani badala ya kiongozi ambaye wananchi wamemchagua. Sababu za kutowaapisha viongozi waliochaguliwa hazijitoshelezi ndiyo maana wananchi wameshinikiza zoezi hilo lifanywe na wakili wa kujitegemea na sheria zinaruhusu kwakuwa zinataka mtu anayefanya hivyo ama awe hakimu au kamishna wa viapo,” alisema Kidera na kuongeza kuwa:

“Endapo kutakuwa na utata wowote utakaojitokeza baada ya mwenyekiti na wajumbe wake kuanza kutekeleza majukumu yao basi nguvu ya umma itatumika kuamua hatma ya hali hiyo…tutaandamana na wananchi wanasubiri kuona hilo linatokea.”

Nilisoma kwenye magazeti ati CCM imeweka pingamizi kuhusu matokeo ya kura hapo Migombani. Swali langu la msingi. CCM kama wanavyojinadi kuwa ni wakongwe wa demokrasia, kwa nini swala hilo hawajapeleka Mahakamani kama jinsi wanavyowaambia wapinzani pindi wanapokuwa na malalamiko yao, badala yake wamekimbilia kwenye Halmashauri. CCM nendeni mahakamani mdai haki yenu kama mnadhani CHADEMA wamechakachua ushindi kuliko kuendeleza malimbano na kuwakosesha wananchi huduma ambazo ni haki yao.
 
Haya ndio matokeo ya ubishi wa chama changu. Kwanini mtu alieshinda asipewe haki yake? Sasa tusubiri wabunge na raisi
 
Hatimaye Makongoro Mahanga ametimiza mipango yake ya kumg'oa mkurugenzi , na yeye bila kujua kaingia mkenge ! Siasa za ccm ni hatari sana ! Pole ndugu ofisa kwa yaliyokukuta , utavuna ulichopanda , hakuna mahali popote katika dunia hii ambapo umma uliwahi kushindwa na wezi .
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.

Acha ungese ww..!! Hiyo demokrasia mnayojifanya mnahubiri iko wapi???

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Hatimaye Makongoro Mahanga ametimiza mipango yake ya kumg'oa mkurugenzi , na yeye bila kujua kaingia mkenge ! Siasa za ccm ni hatari sana ! Pole ndugu ofisa kwa yaliyokukuta , utavuna ulichopanda , hakuna mahali popote katika dunia hii ambapo umma uliwahi kushindwa na wezi .

Eeeh ati nini? Huyu anawalamba booty wanasiasa uchwara kaliba ya akina mahanga?

Akafilie mbali huyo, hafai kuwa mtumishi wa umma huyo
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.

Kati ya waliojiapisha na huyo Mkurugenzi na CCM yake nani atasabisha machafuko?? Kwa vile Mwenyekiti aliyeshinda tena kwa kura nyingi, haapishwi kisa Mhe. anaishi eneo hilo. Kama amachokwa, amechokwa tu. CCM mwogopeni Mungu.
 
Haya ndio matokeo ya ubishi wa chama changu. Kwanini mtu alieshinda asipewe haki yake? Sasa tusubiri wabunge na raisi

Hiki chama chetu hakina msamiati wa kushindwa. "Tutaongoza milele". Mkurugenzi wetu wa itikadi na uenezi.
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.

Hii ni ishara mbaya kwa huko tuendako, lakini huu ujumbe ni mzuri kwa viongozi kwamba waongozwa wamechoka, wanataka mabadiliko. ni budi sasa viongozi wa CCM kuyasoma mabadiliko jamii inayoyataka na kuyaridhia.

Viongozi wetu wakiendelea kukaidi matakwa ya jamii watakwenda kudhurika wao pengine na familia zao na jamii wanayoiongoza.

hii ni "vision" yangu, naweza nisiwe sahihi
 
Serikali haiwezi kupambana na nguvu ya umma.
Nashukuru sana Mamndenyi umeanza kueleewa kua ccm ni chama cha wahuni, tokea kombe la dunia limeisha na we umebadirika sana, thanks very much and big up for M4C, elimu imefika kwa wengi.
 
Kati ya waliojiapisha na huyo Mkurugenzi na CCM yake nani atasabisha machafuko?? Kwa vile Mwenyekiti aliyeshinda tena kwa kura nyingi, haapishwi kisa Mhe. anaishi eneo hilo. Kama amachokwa, amechokwa tu. CCM mwogopeni Mungu.

Jinsi wasivyo na haya wanatumia nguvu kubwa sana kutupotosha ili tuwaone Chadema wakorofi kumbe wao ndio wanaanzisha vurugu!
 
Tukianza kuapishana kizembe hivi mwisho wake so mzuri.itafikia wakati mpaka rais tutakuja kumuapisha kihuni hivihivi.serial I kemea upumbavu huu.
 
Inabidi sasa awajibishwe mkurugenzi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake, asipowajibishwa wananchi tutamshughulikia
 
Anayeleta machafuko ni nanai?anayeleta machafuko ni CCM.CCM msipotenda haki amani haiwezi kuwepo,soma Biblia Zaburi 85.10,inasema hivi Fadhili na kweli zimekutana.Haki na amani zimebusiana.....
Vitu vinavyobusiana viko karibu kabisa,vinapendana.Kwa hiyo uwezi pata amani bila haki.Na mwaka huu wapenda haki wengi watakufa.
 
Back
Top Bottom