Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ilala amepinga vikali kuapishwa kwa mwenyekiti wa mtaa wa segera-Migombani kulikofanywa na wakili binafsi, akisema kuwa ni ubabaishaji na kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Kauli hii imekuja Siku moja baada ya wananchi wa mtaa huo wa Migombani jijini Dar es Salaam kuchukua dhamana ya kumuapisha mwenyekiti wao kwa kutumia wakili binafsi.

Wakati Mkurugenzi huyo wa Ilala akitoa kauli hiyo, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Segerea, Gango Filemon Kidera amebainisha kuwa wananchi wataendelea kupata huduma za kiserikali kutoka ofisi hiyo kama inavyotakiwa kwani kilichofanywa kilikuwa wazi na kilizingatia sheria za nchi na si batili kama inavyozaniwa.

“Tunasubiri tuone mkurugenzi anataka kumuweka nani badala ya kiongozi ambaye wananchi wamemchagua. Sababu za kutowaapisha viongozi waliochaguliwa hazijitoshelezi ndiyo maana wananchi wameshinikiza zoezi hilo lifanywe na wakili wa kujitegemea na sheria zinaruhusu kwakuwa zinataka mtu anayefanya hivyo ama awe hakimu au kamishna wa viapo,” alisema Kidera na kuongeza kuwa:

“Endapo kutakuwa na utata wowote utakaojitokeza baada ya mwenyekiti na wajumbe wake kuanza kutekeleza majukumu yao basi nguvu ya umma itatumika kuamua hatma ya hali hiyo…tutaandamana na wananchi wanasubiri kuona hilo linatokea.”

Ninapata raha sana,nilikuwa na maumivu ya tumbo nimepona ghafla.
 
MKURUGENZI KWA UZEMBE WAKE ANASTAHILI KUSHTAKIWA KWA SABABU ANACHELEWESHA HAKI ZA WANANCHI BILA SABABU ZA MSINGI ni lazima ayakabili mashtaka/reason kuchelewa kwake kumeweza kuhatarisha #amani
 
sheria ya uchaguzi kanuni no 40.0 inatoamaelelkezo ya kuapishwa na wakili au hakimu mbele ya hadhara ya wananchi
 
Mkuu. Kwani serikali ilijiweka yenyewe madarakani?
Si wananchi hao hao ndio waliamua hawa wawe viongozi wetu?

Kwa mtindo huu unaendelea tunaanza kuamini imejiweka madarakani.
Wananchi sasa wameamua hawa wasiwe viongozi wetu hamkubaliani na maamuzi yao. Subirini October.
 
WaHabari wana JF.

Asubuhi ya leo nilikuwa nikisoma Post inayosema serikali haijamuapisha mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Migombani huko Segerea. Nilishangazwa sana na comments zilizotolewa na mtu mmoja anaitwa MUSSA ALLAN. Kijana huyu, Faiza Foxy na wengineo walioko humu JF wanamkosea sana Mungu kwa kutumiwa vibaya na serikali ya kifisadi ya CCM kwa kuitetea CCM na wana CCM kwa mabaya wanayofanya, zuluma, ufisadi,utekaji na mauaji ya serikali ya CCM yamekua yakitetewa na vijana hawa.

OMBI
Mimi ni Mkristo nawasihi sana wakristo wenzangu na ndugu zetu waislamu mwaka huu wa 2015 tuungane pamoja kuwaombea mabaya vijana hawa na mabosi zao, chochote kitakachofanywa kwa kazi ya mikono yao kilaaniwe,Mungu awalaani vijana hawa na mafisadi wote wa serikali ya CCM. Kama Mungu hapo mwanzo aliweza kuwaongoza watu wake kupambana na maadui zao tena kwa njia ya kumwaga damu basi nasi Mungu atatuongoza watanganyika katika dua hili.


HITIMISHO
Wataenda India na Marekani kwa kutafuta tiba na hatimaye kufa na watatuacha watanganyika masikini tukiendelea kuishi katika Tanganyika yetu.
 
Yesu alifundisha kuwapenda adui zenu. Inakuwaje wewe Lusam unayejiita mkristo unachukia watu walio na mawazo tofauti na yako?
 
Last edited by a moderator:
Yesu alifundisha kuwapenda adui zenu. Inakuwaje wewe Lusam unayejiita mkristo unachukia watu walio na mawazo tofauti na yako?

mimi niko upande mmoja na huyo bwana! Kweli wewe na wenzio mnaleta laana kwa nchi yetu pendwa, mnashabikia wezi, wauwaji kwanini tusiwaombee mpotee kabisa? kuna neno kama mkono wako ukiwa unakukosesha ufalme wa Mungu ni bora kuukata na uingie bila mkono! nyie ni wa kukatwa!
 
Last edited by a moderator:
Huo ukinyemela ni upi wakati kaapishwa mbele ya halaiki na media zimetanganza na aliyemwapisha ni Mwanasheria wenye kiapo na usajili?

Mnajidhalilisha na ubishi wenu usio na hoja.

Anayepeleka nchi kwenye matatizo ni nani kama si ccm na mamluki wake kuendesha nchi kwa ubabe na udanganyifu? kwa nini serikali ilikataa kumwapisha wakati wananchi wamemchagua?

Mnachosha.


Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.
 
Mbona kama hujitambui na wala huelewi kilichotokea mkuu!...hapa anaesababisha vurugu ni nani kati ya mkurugenzi anayekataa kumuapisha mtu aliyeshinda kihalali na wananchi ambao wamemchagua waliemtaka awaongoze, kisha wakaamua kumuapisha kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
sina shaka na wewe ni sehemu ya tatizo kwa kukumbatia utawala dhalimu usio sikia sauti za wananchi. Nakupa pole nikitarajia siku moja utajitambua
 
Back
Top Bottom