Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

ifike wakati utaratibu wa kuapata wakurugenzi ubadilike hii habari ya mwenyekiti wa chama anawateuwa ndio madhara yake....
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.
Samahani mkuu nivyokusoma haraharaka nikajua ndio yule Musalani wa Lumumba buku saba.
 
Last edited by a moderator:
Tutegemee matatizo makubwa WAKURUNGENZI WAJINGA kama huyu ndiyo wasimamizi wetu wa uchanguzi wa Oktoba 2015.Mimi si nabii wala mnajimu kwa picha hii naona matatizo na hata damu kumwangika tusipokuwa makini.
 
wanasubiri nini sasa kuwaapisha? hawajui wananchi wanataka huduma kutoka kwa hao viongozi? ccm sijui kwa nini hawakubali kushindwa, walijinasibu wamechua ubingwa sasa wale waliokosa ubingwa huo kwa nini kuwanyima hicho kidogo walichopata? Huyo mkurugenzi ni wa kumfuata huko ofisini atoe tamko anataka nini kwenye hicho kitongoji akijiumauma apigwe tu.
 
Hawa wakurugenzi ni chanzo cha machafuko, wao wakubali tu pale anaposhinda yeyote

Wakurugenzi wengi wanafanya kazi kwa maelekezo ya ccm, ndiyo maana haya yanatokea, shame on you CCM
 
Bila idhini ya mamlaka halali?
Kweli chumvi ni kiungo safi sana na ni muhimu mno kwa chakula cha kawaida. Lakini chumvi ikiharibika itiwe nini ili iweze kurudia ubora wake unaotakiwa??? Ni serikali gani ambayo inakubali maamuzi yake tu na kugandamiza maamuzi ya uma wakati uohuo inasisitiza kufuata demokrasia ya wengi wape? Walishatangaza kwamba Wilaya yote ya Ilala ni CCM tu wameshinda viti vya serikali za mitaa. Kumbe wakasahau kwamba wananchi wa leo ni tofauti na wale wa Enzi za "ZIDUMU FIKRA ZA MTU MMOJA" Wamechakachua mahali pengi ndio maana wanaweweseka, lakini ccm ijue kila kitu kina kikomo. Vuvuzela anakoroma na kutoa povu kila mahali huku akijua ccm ni wezi waliobobea. Muulizeni Zuma Afrika kusini joto la mwili lilikuwa ngapi alipoambiwa bungeni waziwazai na mmama mmoja kuwa "President Zuma is an international Criminal, and a big Thief". CCM wajipange kurekebisha mambo na sio kulazimisha. Serikali za mitaa ndiko kwenye kila sababu ya kuhitaji viongozi wanaokubalika sana na wananchi wa maeneo hayo ili maendeleo yaje. Kuchomekeana ndiko kunakodhoofisha maendeleo. Wiki mbili tu baada ya kuapisha, tayari wenyeviti waliochomekwa na ccm wameanza kuuza viwanja na mashamba ya watu, wameweka sharia zao za kukandamiza wapinzani wao na watu ambao wanahisiwa hawakuwapa kura zao. kila mahali tyunayasikia hayo. CCM ndiyo itakayozalisha uharibifu wa amani nchini.
 
Hawa wakurugenzi ni chanzo cha machafuko, wao wakubali tu pale anaposhinda yeyote

serikali ya mtaa iliyoapishwa endeleeni kuwahudumia wananchi kwani mmechaguliwa kihalali na mnaongoza kihalali. mpaka sasa hakuna pingamizi lolote mahakamani. hao mahakimu wa magamba wanagoma kuwaapisha ili iweje? chapeni kazi kama kawaida, achana na propaganda za CCM.
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.

na huo uhuni wa kukataa kuwaapisha viongozi wa umma uachwe uendelee? wewe una akili ndogo kuliko konokono.
 
Samahani mkuu nivyokusoma haraharaka nikajua ndio yule Musalani wa Lumumba buku saba.

ndio huyo ni msalani wa lumumba. atabadilisha sana id mwaka huu ila mwisho wake ni Oktoba mwaka huu.
 
Last edited by a moderator:
Wana migombani wanahitaji huduma KAMA WATANZANIA wengine who to blame uzembe WA mkurugenzi ktk utenndaji au?must be nutty!
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.
Kama ndivyo kwanini Mkurugenzi asimuapishe? Vurugu analeta Mkurugenzi mwenyewe kwa maelekezo kutoka anakojua yeye. Haiwezekani tangia tarehe 14/12/2014 serikali ya mtaa haijaanza kazi wakati kashachaguliwa. Naomba uwashauri hao unaowatetea waache kuatarisha amani ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom