Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

Serikali: Hatujaapisha viongozi Migombani

Kanuni za uchaguzi zipo na zimefuatwa kelele za nini? Tangu uchaguzi ukamilike ni zaidi ya mwezi mmoja na walioona uchaguzi haukuwa huru na wa haki wameshafungua kesi mahakamani kama kanuni zilivyoagiza. Sasa huko mgombani ni drc au ni hapahapa dsm? Nguvu ya umma na itawale mahali popote haki inapominywa!
 
Bila idhini ya mamlaka halali?

Hakuna kanuni ya uchaguzi wa serikali zq mitaa inayosema wataapishwa mbele ya mkurugenzi wa manispaa. Ila inasema wataapishwa mbele ya wananchi na mwanasheria aliyesajiliwa au hakumu fullstop
 
Ni zamu ya ccm kwenda kulalamika mahakamani
 
Kama CCM wanaona sheria zimekiukwa waende mahakamani.
 
Utaipelekea kwenye machafuko? Kwani machafuko hayapo mpaka sasa kwa hii serikali ya CCM. Mifano kidogo angalia picha hizo hapo chini




Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.

 
Mkurugenzi kama anaona kitendo kilichofanywa na wananchi ni kinyume cha sheria aende mahakamani. Kwani si ndivyo kila siku wanasema kwamba hasiyeridhika na hatua aende mahakamani?
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ilala amepinga vikali kuapishwa kwa mwenyekiti wa mtaa wa segera-Migombani kulikofanywa na wakili binafsi, akisema kuwa ni ubabaishaji na kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Kauli hii imekuja Siku moja baada ya wananchi wa mtaa huo wa Migombani jijini Dar es Salaam kuchukua dhamana ya kumuapisha mwenyekiti wao kwa kutumia wakili binafsi.

Wakati Mkurugenzi huyo wa Ilala akitoa kauli hiyo, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Segerea, Gango Filemon Kidera amebainisha kuwa wananchi wataendelea kupata huduma za kiserikali kutoka ofisi hiyo kama inavyotakiwa kwani kilichofanywa kilikuwa wazi na kilizingatia sheria za nchi na si batili kama inavyozaniwa.

"Tunasubiri tuone mkurugenzi anataka kumuweka nani badala ya kiongozi ambaye wananchi wamemchagua. Sababu za kutowaapisha viongozi waliochaguliwa hazijitoshelezi ndiyo maana wananchi wameshinikiza zoezi hilo lifanywe na wakili wa kujitegemea na sheria zinaruhusu kwakuwa zinataka mtu anayefanya hivyo ama awe hakimu au kamishna wa viapo," alisema Kidera na kuongeza kuwa:

"Endapo kutakuwa na utata wowote utakaojitokeza baada ya mwenyekiti na wajumbe wake kuanza kutekeleza majukumu yao basi nguvu ya umma itatumika kuamua hatma ya hali hiyo…tutaandamana na wananchi wanasubiri kuona hilo linatokea."
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.

Na ni utezi dume kutaka kuwachagulia wananchi kiongozi. Msituletee utezi dume hapa, kwanini yeye mkurugenzi hakumuapisha huyo chaguo la wananchi? Je huo sio uhuni?
 
Tukianza kuapishana kizembe hivi mwisho wake so mzuri.itafikia wakati mpaka rais tutakuja kumuapisha kihuni hivihivi.serial I kemea upumbavu huu.

Sidhani kama Mpumbavu anaweza kemea upumbavu ikiwa tu ilichokifanya serikali pia ni upumbavu.
 
Sidhani kama Mpumbavu anaweza kemea upumbavu ikiwa tu ilichokifanya serikali pia ni upumbavu.

Watawala wetu ni kati ya vichekesho ktk eneo hili la Afrika! Ukisha ona watawala hawaheshimu chaguzi tambua machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe ni karibu. Alafu kuna mabwege fulani badala ya kukemea uhuni eti yanaliombea taifa amani. Mtu mweusi bure kabisa!
 
Huyu mkurugenzi mbona anajichanganya yeye keshasema kuwa amepata maagizo kutoka uongozi wa juu wa ccm kuwa lazima jamaa wa ccm apitishwe sasa hapa anatuletea stori gani tena.
 
Huu uhuni wa kuapishana kinyemela inabidi ukemewe kwa nguvu zote utaipeleka nchi kwenye machafuko.

Sasa hapa nani mhuni,kati ya mamlaka inayodhihaki maamuzi ya wananchi au huyu mkurugenzi anayemtumikia makongoro mahanga?😡😎:thumbdown::thumbdown:
 
Na ni utezi dume kutaka kuwachagulia wananchi kiongozi. Msituletee utezi dume hapa, kwanini yeye mkurugenzi hakumuapisha huyo chaguo la wananchi? Je huo sio uhuni?

Wanataka wakupige ngumi ukitaka kurudisha ili kujibu mapigo kwa namna inayokufurahisha CCM hawataki wanataka ukashtaki mahakamani, eti ndiko kufuata sheria!!!
 
Wanataka wakupige ngumi ukitaka kurudisha ili kujibu mapigo kwa namna inayokufurahisha CCM hawataki wanataka ukashtaki mahakamani, eti ndiko kufuata sheria!!!
Wanaona aibu waziri na kada maarufu wa chama anaishi chini ya himaya ya ukawa
 
Samahani mkuu nivyokusoma haraharaka nikajua ndio yule Musalani wa Lumumba buku saba.

Inawezekana ni yy maana mchango wake km ule ule alafu avator yake ni ile ile! Naona kamodify jina tu
 
Last edited by a moderator:
si huwa wanasema serekali ni WANANCH! sioni tatizo wananchi ambao ndio serekali wakimuapisha kiongozi wao waliyemchagua!
 
Back
Top Bottom