Serikali: Hakuna nafasi ya mwanafunzi wa kidato cha tano kubadili mchepuo au shule

Mmezoea kulalamika.

Kuna mtu mmoja alisema, nitamnukuu "Watu wote wenye kupenda kulalamika, ni watu ambao hawafanikiwi maishani mwao, maana wao wanaona vitu kwa upande wa matatizo tu - ndio maana hautakaa uone tajiri analalamika"

Hivi watoto wote wakiomba uhamisho wa kuhama shule walizopangiwa kwenda nyingine, nani atasoma kule wanakohama?
Em jarbu kufikili vizuri.. mfano mm nmemalizia dar then nmepelekwa Kagera, na rafki zng mmoja kapangiwa Mtwara mwingine Kilimanjaro.. iv kuna maana gani ya kutupelek kanda za mbali na kuwaleta huku haaooo wa huko?? Kwan wangepanga kla watu ktk kanda zao au za jirani zaidi kingepunguka nn?? Ni wapuuz hao wanaopanga. Nchi ynyw maskin na bado tunapeana gharama zngne. Wajinga wa akili waliopanga
 
me naona tupo weng xn ambao hatujachaguliwa naomba ty serikali ituangalie na cc ktaa kubay ila inauma xn wakat umebalance comb vzur af unaachwa kuchsguliwa wakat kuna wengne wancombless af wamechaguliwa bac me naulz nn maana ya comb sasa?
 
sijaona tangazo la hovyo kama hili, wakumbuke hawa waliochanguliwa wapo watakaokwenda shule za binafsi, watakaoamua kwenda chuo, waliolewa na waliofariki, sasa nafasi hizo zitakuwa wazi? je wale 12 elfu waliokosa nafasi nao wanawafanyaje? wapo watoto waliopangiwa day school wakati hawana pa kuishi inakuwaje? waache shule waendeshe bodaboda na kuwa mama lishe? kuna watumishi wa umma badala ya kutumikia umma wameamuka kupambana na umma. ila hawajui zama zimebadilika sasa hatutasubiri watumbuliwe tutawabauruza makofi maofisini kabla ya kutumbuliwa.
 
Mmezoea kulalamika.

Kuna mtu mmoja alisema, nitamnukuu "Watu wote wenye kupenda kulalamika, ni watu ambao hawafanikiwi maishani mwao, maana wao wanaona vitu kwa upande wa matatizo tu - ndio maana hautakaa uone tajiri analalamika"

Hivi watoto wote wakiomba uhamisho wa kuhama shule walizopangiwa kwenda nyingine, nani atasoma kule wanakohama?

Kulazimisha mwanafunzi asome mchepuo usio fani yake ni ubeberu uliopitwa, ndio maana mtu anamaliza form six hana hata idea ya kitu chochote kwa kuwa kalazimishwa asome fani asiyoitaka. Na ni kawaida tu serikali kuchagua mchepuo ambao wewe hukuomba mfano mimi mwenyewe. Sio kila kitu ni kulalamika bali ndio hali halisi
 
Hizo shule zenu watasoma watoto wa masikini ambao hawana option.Binti yangu anapenda udaktari mnamlazimisha akasomee uhasibu haitawezekana.
 
Kuna wanafunzi wasioona kutoka shule ya Iringa wamepelekwa shule zisizo na miundombinu husika na isiyona waalimu wao.HivyoHivyo wasiliana na Iringa ili wasisumbuliwe pasipo sbb
wanafunzi wasioona wa kike au wa kiume???
 
wenye pesa zao wataenda shule za private,mtoto wa choka mbaya abaki hukohuko,tangu lini mtoto wa masikini husikilizwa?Hata hivyo siku hiz ni kuburuzwa tu,Serikali ikiamua cku hizi ni lazima iwe hivyo.Hofu na manyanyaso yameongezeka
 
Binafsi napingana na suala la msemaji wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali ya mtaa ya kuwa wanafunzi waliochaguliwa hawaruhusiwi kubadili michepuo waliyopangiwa kwa sababu kuu mbili;

moja ikiwa ni kwamba, kuna baadhi ya wanafunzi wanapangiwa michepuo ambayo kwao ni kama chaguo la mwisho, bila kuzingatiwa chaguo lake la kwanza ambalo amefaulu vizuri tu bila shida, lakini pia kutakuwa na shida kama huyo mwanafunzi atabadilisha mchepuo katika shule aliyopo?

Kwa mfano, shule X ina michepuo mitano ambayo ni PCB,PCM, CBG, EGM, PGM harafu mwananfunzi kachaguliwa kusoma PCB kwenye hiyo shule X, tatizo lipo wapi kama huyo mwanafunzi anataka kusoma PCM kwenye hiyo shule husika kama ana vigezo vya kusoma mchepuo husika?

Nafikiri hoja hapa ni kujaa kwa shule na siyo kubadikisha mchepuo kwani hata tafiti mbalimbali zinaonyesha ya kuwa, mtu atafanya vizuri kama alichopangiwa ndo chenyewe
huko sahii ndugu kwani kuna mdogo wangu amepangiwa combination ambayo hakiuijaza kabisa na yeye amesema anataka sayansi je hapo ni sahii ?
 
Wapo wanafunzi watakaosoma kwa shinikizo wakati mchepuo anaoutaka sio aliochaguliwa iwapo aba vigezo..hii itamsababishia kutokujituma maana atakuwa anasoma kitu ambacho hakipendi, hii itapelekea mwisho wa siku kuharibu future za watu!!
 
Hili ni tangazo lislo na mantiki, na aliyelitangaza amekosa weledi.

Wanafunzi hujaza combinations wakati wanapofanya mitihani. Kuna wakati mwanafunzi huwa na mashaka makubwa atapata nini kwenye mitihani aliyoifanya. Anaweza kujaza combinations ambazo siyo chaguo lake hasa bali ni kutokana na jinsi alivyoiona mitihani. Majibu yanapotoka yanakuwa kinyume kabisa cha mategemeo yake. Combinations zile ambazo alizipenda lakini akaogopa kujaza, ndizo alizofanya vizuri zaidi kuliko alizozijaza. Mwanafunzi kama huyo kwa nini asiruhusiwe kubadilisha na akasoma anachokitaka.

Viongozi wanatakiwa wajue kuwa mwanafunzi siyo kama mgambo, anatakiwa kupewa maximum flexibility kuliko viongozi kufikiria kuwa wao ni makamanda wa wananchi katika mambo yote na kwa makundi yote. Tukienda hivyo tutaua vipaji vya watoto wetu.
 
Kama ni hivyo inabidi nimpeleke yule kijana wangu private school au chuo cha afya maana naona atakwenda kuumia PCB na historia ya shule aliyechaguliwa
Kufaulu 70% inamtegemea mwanafunzi mkuu. Kama hajiweza hata ukimpeleka fedha atakuwa kama yule wa mh. wa msoga.
 
Hii haijakaa vizuri,nakumbuka kuna baazi ya shule za serikali huwa zinabandika utaratibu wa kubadili comb,.na hii ilinisaidia hata Mimi mwenyewe
 
Baada ya mwezi tufanye tathmini kuna shule hazitakuwa na wanafunzi. Nani atpeleka mtoto wa huko maporini hamna walimu wala vitabu, hakuna chakula wala huduma za afya. Huyu tamisemi mwache ajidanganye hadi atakaposhuhudia shule zake hazina wanafunzi ndipo atakapo tambua hata sie wazazi tumeamua 'hapa kazi tu'
 
Unaweza ukakuta 30% ya waliochaguliwa wasiende kwenye hizo shule. Kwa hyo shule zitabaki bila wanafunzi??
 
Mmezoea kulalamika.

Kuna mtu mmoja alisema, nitamnukuu "Watu wote wenye kupenda kulalamika, ni watu ambao hawafanikiwi maishani mwao, maana wao wanaona vitu kwa upande wa matatizo tu - ndio maana hautakaa uone tajiri analalamika"

Hivi watoto wote wakiomba uhamisho wa kuhama shule walizopangiwa kwenda nyingine, nani atasoma kule wanakohama?
Kwan hili lakuhama limeanza leo! Lin ulisikia nchi nzima wamehama pia tambambua unahama kwasababu maalum hasa zakiafya
 
Back
Top Bottom