Serikali: Hakuna nafasi ya mwanafunzi wa kidato cha tano kubadili mchepuo au shule

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
SERIKALI imesema shule zote zenye nafasi za wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu, zimejaa hivyo hakuna nafasi ya mwanafunzi kubadilishiwa shule au mchepuo aliochagua.

Hayo yalibanishwa jana katika taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari mjini hapa na Msemaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Rebecca Kwandu.

Kwandu alisema baada ya serikali kutangaza wanafunzi waliojiunga na kidato cha tano, baadhi ya wazazi na wanafunzi wamekuwa wakifika ofisi za Tamisemi kuomba kubadilishiwa shule au tahasusi (michepuo) walizochaguliwa.

“Tunapenda kuwaarifu kwamba shule zote zenye nafasi za wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2016 zimejaza, hivyo hakuna kinachoweza kubadilishwa,” alisema Kwandu.

Aidha, Kwandu alisema vigezo ambavyo vilitumika katika uchaguzi huo ni pamoja na ufaulu na uchaguzi wa wanafunzi wenyewe juu ya masomo wanayopenda kuendelea nayo kidato cha tano na sita.

“Kulingana na utaratibu uliowekwa na serikali, mwanafunzi mwenye sifa za kuchaguliwa kuendelea kidato cha tano na vyuo vya ufundi ni yule ambaye ufaulu wake ni kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu. Wanafunzi hao wamepangwa kulingana na ufaulu wao masomo waliyochagua na nafasi zilizopo,” alisisitiza.

Pia alisema nafasi za shule walizopangiwa wanafunzi zimezingatia miundombinu ya shule husika na uwezo, na kwamba kila shule imepewa wanafunzi kulingana na nafasi zilizopo, hivyo hakutakuwa na nafasi ya kuwabadilisha kutoka shule moja kwenda nyingine kwa sasa.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kuripoti katika shule na vyuo walivyopangiwa kama walivyoelekezwa.

Alisema mwanafunzi ambaye hataripoti ifikapo Julai 24, ambayo ni tarehe ya mwisho kwa muda uliopangwa, atakuwa amepoteza nafasi yake kwa kuwa itachukuliwa na mwanafunzi mwingine ambaye hakupata nafasi awali.

Aisee mbona hii serikali inataka kuendesha kila kitu kibabe? Tangu enzi hizo, watu waliruhusiwa kuhama shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo hali ya hewa. Kwa mfano kuna mtu alipangwa Mbeya au Iringa, kutokana na baridi kali labda ana tatizo la pumu akalazimika kuhama. Kuhusu kubadili tahasusi, kuna mtu alichaguliwa PCM au PCB akaona ni maji marefu yatamzamisha akaamua kuhamia tahasusi za masomo ya sanaa. Rai yangu serikali hii ambayo inataka kuwaburuza Watanzania, chukueni mfano wa mbuzi, mbuzi ukimvuta ili akanyage maji mwisho hulala chini sasa wewe ndiyo uamue moja, kumbeba au kubadili njia.
 
Mmezoea kulalamika.

Kuna mtu mmoja alisema, nitamnukuu "Watu wote wenye kupenda kulalamika, ni watu ambao hawafanikiwi maishani mwao, maana wao wanaona vitu kwa upande wa matatizo tu - ndio maana hautakaa uone tajiri analalamika"

Hivi watoto wote wakiomba uhamisho wa kuhama shule walizopangiwa kwenda nyingine, nani atasoma kule wanakohama?
 
Binafsi napingana na suala la msemaji wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali ya mtaa ya kuwa wanafunzi waliochaguliwa hawaruhusiwi kubadili michepuo waliyopangiwa kwa sababu kuu mbili;

moja ikiwa ni kwamba, kuna baadhi ya wanafunzi wanapangiwa michepuo ambayo kwao ni kama chaguo la mwisho, bila kuzingatiwa chaguo lake la kwanza ambalo amefaulu vizuri tu bila shida, lakini pia kutakuwa na shida kama huyo mwanafunzi atabadilisha mchepuo katika shule aliyopo?

Kwa mfano, shule X ina michepuo mitano ambayo ni PCB,PCM, CBG, EGM, PGM harafu mwananfunzi kachaguliwa kusoma PCB kwenye hiyo shule X, tatizo lipo wapi kama huyo mwanafunzi anataka kusoma PCM kwenye hiyo shule husika kama ana vigezo vya kusoma mchepuo husika?

Nafikiri hoja hapa ni kujaa kwa shule na siyo kubadikisha mchepuo kwani hata tafiti mbalimbali zinaonyesha ya kuwa, mtu atafanya vizuri kama alichopangiwa ndo chenyewe
 
Tuwe wakweli, si wazazi wote watakubali watoto wao waende shule za hovyo. Maana watapotea. Lakini pia hivi unalazimishaje career ya mtoto wa mwenzio? Mtu anataka kuwa daktari unasukumia HKL. Suala la kubadili shule watu wanaweza KUVUMILIA ila si combination. Tuache kutoa miongozo isiyo jenga. Hayo waachiwe walimu wakuu mashuleni. Hadi uamuzi wa combination unatoka tamisemi???
 
Huku tunakoelekea sio kuzuri kama mambo ndo haya.

Umenipangiwa nikasome pcm na hesabu siwezi fizikia siwezi

Nataka niende ninakoweza hutaki nibadili sasa unataka nifeli halafu mwisho wa siku tuanze kuita ki.laza kumbe nyie ndo mnasabisha tuwe vilaza .

Jamani jamani tusifike huko aisee tutawapoteza wanetu kwa kutofikia malengo yao.
 
Kigezo kilikuwa selection ya mwanafunzi na combination alio faulu, sasa serikali imeona combination inayo mfaa mwanao/ binti kufuata na na uchaguzi wake na ufaulu wake ni HKL au PCB sasa lawama za nini ??
 
mtu akiona hawezi kubadili mchepuo aamue kuchepuka ndipo ataweza kubadili mchepuo lakini akubiliane na gharama mpya maana kule private ni hapa mpene tu!
 
Huu ni unyanyasaji wanakatisha ndoto za vijana wetu kusomea vitu wanavyovitaka , Utasomaje combination ambayo shule yenyewe poor performance combination ni ngumu, bora ubadilishe uchukue masomo ya kufaulu asonge mbele.
 
Kigezo kilikuwa selection ya mwanafunzi na combination alio faulu, sasa serikali imeona combination inayo mfaa mwanao/ binti kufuata na na uchaguzi wake na ufaulu wake ni hkl au pcb sasa lawama za nini ??
UMETUKUMBUSHA KITU CHA MSINGI LAKINI KWA UZOEFU WANGU WANAFUNZI WENGINE WALIKUWA WAKIPANGIWA COMBINATION AMBAZO HAWAKUCHAGUA,, LAKINI NAONA KWA KIPINDI HICHI NECTA IMEJITAHIDI SANA KUPANGA KAMA MAOMBI YA WANAFUNZI YALIVYO TATIZO NI KWA WALE WENYE UFAULU HAFIFU..............
 
Kuna wanafunzi wasioona kutoka shule ya Iringa wamepelekwa shule zisizo na miundombinu husika na isiyona waalimu wao.HivyoHivyo wasiliana na Iringa ili wasisumbuliwe pasipo sbb

Back
Top Bottom