Serikali haiuoni uchochezi huu wa kidini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali haiuoni uchochezi huu wa kidini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkwele, Mar 30, 2011.

 1. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwandishi:George Maziku

  Kuna harakati kubwa zinaendelea nchini kote kuwachochea wananchi wa imani ya Kiislamu kuwachukia wananchi wenzao wa imani ya kikristo.

  Wanaoendesha harakati hizi ni baadhi ya viongozi wa kiislam ambao wanatembea huku na kule nchini kueneza taarifa za uongo dhidi ya wakristo.

  Watu hawa wamekuwa wakihutubia misikitini, katika makongamano yao, na kutumia vyombo vyao vya habari, wakieneza madai ya uongo na uzushi kwamba nchi yetu inaongozwa na "mfumo Kristo".

  Kwamba serikali ya Tanzania tangu zama za utawala wa awamu ya kwanza wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, imekuwa ikiwapendelea Wakristo katika nyanja mbalimbali za kimaisha huku ikiwabagua Waislamu.

  Viongozi hao wa Kiislamu wamekuwa wakitangaza kuwa serikali imekuwa ikifanya upendeleo kwa wakristo na kuwabagua waislam katika utoaji wa huduma za elimu, uteuzi wa viongozi serikalini na taasisi za umma na ajira, ambapo wanadai kuwa nafasi nyingi hupewa Wakristo.

  Wanawashambulia na kuwashutumu vikali hayati Mwalimu Nyerere na viongozi wa makanisa ya Kikristo hususan viongozi wa Kanisa Katoliki nchini, kuwa ndio waasisi wa ‘dhuluma' hii dhidi ya Waislam.

  Wanazungumza maneno mengi ambayo wanadai kuwa ndio ushahidi wa tuhuma zao dhidi ya serikali na makanisa, na wanahitimisha kwa kuwataka Waislamu kuamka na kupambana kudai haki zao kwa njia na gharama yoyote.

  Watu hawa wamekwenda mbali zaidi hata kufikia kuhamasisha machafuko nchini kote, wanasema kuwa kama Wakristo wamemwaga ugali, basi nao wako tayari kumwaga mboga, wakimaanisha kuwa ni bora kusiwe na amani nchini ili tukose wote, yaani asiwepo mtu au kundi la watu wanaofaidi nchi peke yao wakati wengine wakibaguliwa.

  Wachochezi hawa wanazunguka kila kona ya nchi yetu wakieneza sumu hii, wanafanya hivyo bila kificho kana kwamba nchi hii haina serikali, naamini viongozi wa ngazi zote wameyasikia matamshi ya watu hawa lakini cha kushangaza hakuna kiongozi yeyote aliyetoa kauli kuwakemea wahusika, sijui wanawaogopa au wanatenda hayo kwa baraka za viongozi wa serikali yetu!

  Matokeo ya kauli hizi za uchochezi ni mabaya sana kwa sasa kwani kumeibuka chuki ya kutisha miongoni mwa waislam dhidi ya wakristo hususan katika mikoa ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi hususan Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara
  na Morogoro.

  Jambo la hatari zaidi ni kwamba propaganda hizi chafu na hatari zimepenyezwa kwenye siasa, Waislamu wengi wa ukanda wa pwani sasa wameshikamana na Chama cha Mapinduzi (CCM) eti kwa sababu kiongozi wake Rais Jakaya Kikwete ni Mwislamu.

  Waislamu hawa sasa wananadi kuwa hizi ni zama za Waislamu kutawala nchi, wanauchukulia uongozi wa rais Kikwete kama utawala wa Waislamu, wanamsifia kuwa ameleta uwiano mzuri wa mgawanyo wa fursa za uongozi, ajira na nafasi za elimu kati ya Wakristo na Waislamu.

  Waislam wengi sasa wamegeuka walinzi na watetezi wa serikali ya Rais Kikwete, wanaamini kuwa wote wanaompinga na kumkosoa ni Wakristo ambao wanaona kawakatia mirija yao ya kuendelea kuwakandamiza na kuwanyanyasa Waislamu.

  Waislamu hawa wa ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi wengi wanaamini kuwa upinzani mkali dhidi ya serikali ya Rais Kikwete unaoendeshwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni njama za viongozi wa makanisa hususan Kanisa Katoliki ambao hawampendi Rais Kikwete kutokana na uongozi wake unaojali haki za Waislamu.

  Kwa msingi huo, Waislamu wameihukumu CHADEMA kuwa ni chama cha Kikristo, kwamba ni chama cha Wakatoliki, wameshiba propaganda za uongo na uzushi za CCM zilizoanza mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

  Kwa hakika huu si mwelekeo mzuri kwa taifa letu, tunajenga mazingira hatari yatakayoiangamiza nchi yetu katika siku za usoni, tunaichimbia kaburi amani ya nchi yetu, tunaandaa vita ya kidini ambayo itasababisha mauaji ya kiholela ya wenyewe kwa wenyewe.

  Athari za chuki kati ya Waislamu na Wakristo tayari zimeanza kuonekana wazi, tumesikia mapigano kati ya Waislamu na Wakristo yaliyotokea wiki iliyopita huko Mto wa Mbu, mkoani Arusha, yaliyosababishwa na mihadhara ya kashfa ya kidini ambayo imekuwa ikiendeshwa na makundi ya Waislamu na Wakristo ambayo tumehadharisha kwa muda mrefu kuwa ni hatari na sumu kwa amani ya nchi yetu.

  Uhasama huu wa kidini hauwezi kumnufaisha yeyote, si Waislamu wala Wakristo watakaofaidika na hali hii, wote tutapata hasara, na bahati mbaya uhasama huu utawakumba hata wasiokuwa wafuasi au waumini wa dini hizi na hata wasiokuwa na dini, wote tutapata hasara kubwa.

  Pia napenda kuionya serikali na chama tawala - CCM kwamba hamtabaki madarakani milele kwa kuchochea mitengano na machafuko baina ya wananchi, njia pekee ya kurudisha imani ya wananchi kwenu na hivyo kuendelea kutawala ni kuwahudumia watu kwa uaminifu na uadilifu, kuondoa kero zao za kila siku, kuboresha maisha yao, na kuwawezesha kuishi maisha yenye hadhi ya binadamu, huo ndio ‘uchawi mtakatifu' wa kisiasa. Mwenye masikio na asikie.
  KUNA harakati kubwa zinaendelea nchini kote kuwachochea wananchi wa imani ya Kiislamu kuwachukia wananchi wenzao wa imani ya kikristo.

  Source: Tanzania Daima

  Kwa mwendo huu hatutafika, serikali kimya inasubiri CDM waandamane ndio waanze kuongea na kukemea, lakini hawa wenzangu wanachofanya sio sahihi kabisa labda ni sahihi kwa JK peke yake.
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hao wa2 ni wajnga na wana2mika vbya hawajui 2! Hv c wajiulze mbona Jk na El ni marafk na wanashrkiana kuwaibia waTZ? Wanadanganywa ili waibiwe vzr. Huyo Jk hamjui m2 zaid ya mwanae Riz.
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  very advanced crap.
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hayakuanza leo, na hayatafanikiwa. WaTZ wanajua yote; tumeoleana na kuzaliana hakika hakuna wa kumchinja mwenzie. Propaganda zimeanza muda mrefu tu. WaTZ tusitoke katika mada maana maisha ni magumu kwa muislam, mkiristo na asiyekuwa na dini.
  Je 2015 CCM wakimsimamisha mkristo kuwa mgombea, waislam watasemaje?
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Maaskofu 'wagombea' waraka wa Mtikila Send to a friend Thursday, 27 May 2010 10:21 0diggsdigg

  Mussa Mkama
  MAASKOFU waliohudhuria mkutano wa siku moja wa Jukwaa la Wakristo, juzi walifanya kazi ya ziada kupata nakala ya waraka ulioandaliwa na mwenyekiti wa Chama cha Kidemokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye alitumia mkutano huoo kuusambaza.

  Mkutano huo ulikuwa wa kuzindua chombo hicho kikubwa cha mshikamano baina ya Wakristo, lakini Mchungaji Mtikila, ambaye anaongoza kanisa la Full Salvation, aliutumia kugawa takriban nakala 60.
  Alikuwa akigawa waraka ambao ulisababisha polisi kuvamia nyumba yake iliyo Mikocheni na kufanya upekuzi kabla ya kuondoka na mwanasiasa huyo ambaye pia ni kiongozi wa kiroho na kwenda kumuhoji kituo cha polisi kwa saa kadhaa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

  Waraka huo wenye kurasa 24 ambao Mwananchi ina nakala yake, unazungumzia harakati za kuwaamsha waumini wa dini ya Kikristo kuamka kutetea dini yao dhidi ya utawala wa sasa ambao mchungaji huyo anautuhumu kuwa unawabagua.

  Waraka huo pia unawataja watu mbalimbali, kuanzia Rais Kikwete, viongozi wengine wa kisiasa na watu maarufu ukiwahusisha na tuhuma mbalimbali kubwa.
  Maaskofu kadhaa walionekana kumfuata Mtikila ili kupata nakala ya waraka huo ambao mchungaji huyo alikuwa amebeba nakala zake kwenye mkoba wa mkononi.

  “Nilikuja na nakala chahe sana... 60 tu, zikaisha na wengine wakawa wanautaka tena," alisema Mtikila mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kuzindua chombo hicho ambacho kazi yake kuu itakuwa ni kutetea haki za Wakristo.

  "Nimegawa hapa kwa sababu viongozi wenyewe waliutaka ndiyo nikaona niwape; nisiwe mchoyo,” alisema Mtikila.

  Mtikila alisema kuwa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ni kuzaliwa kwa tatizo kubwa kwa Rais Jakaya Kikwete na kumtaka ajihadhari, akidai kuwa ajira yake sasa ipo kwenye "danger zone (sehemu ya hatari).”
  Mtikila, ambaye ana ujasiri wa kutoa kauli zisizo na simile, alisema jukwaa hilo ni gharika kubwa kwa Rais Kikwete kwa sababu alizodai kuwa kiongozi huyo wa nchi ni adui mkubwa wa Ukristo.

  “Wakristo nchini tupo milioni 27 hivyo ajira ya JK hivi sasa ipo shakani," alisema.
  Viongozi wa makanisa ambayo yalishirika katika kuunda jukwaa hilo ni pamoja na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Tec), Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo (CCT) na Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT).
   
 6. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Thibitisha kwa ushahidi ulio wazi kuwa waislam wanaeneza uongo.Utaje wazi huo uongo ili ujulikane.Waislam sio vilaza kama mnavyodhani,tunazungumza with clear evidence.SWALI:Nyaraka za makanisa hujaziona? Kama uliziona hazichochei uvunjifu wa amani? Maaskofu walipo sema 'damu itamwagika nchi ikijiunga OIC na waislam kupewa mahakama za kadhi," walimaanisha nini? Au damu ya nani inatakiwa kumwagwa? Mbona Mkapa aliyeuza nchi hamumtukani? Nyerere alipofanya mle unga wa yanga mbona hatukanwi? Mbona matusi kwa Mwinyi na Kikwete? Makongamano yataendelea ili kuwaeleza waislam fitna zinazofanywa dhidi yao. Kumbuka kampeni za mwakajana ambavyo zilishamili makanisani,haya hatubahatishi kwani tunaishi kwenye jamii mchanganyiko na pia baadhi ya watu wetu wakaribu ni waumini wa makanisa.Binafsi niko kwenye institution ya kikristo na hapa kwakuwa asilimia 99.9 ni wakristo mengi hujadiliwa na mimi nakuhakikishia chuki yenu juu ya waislam ni kubwa kuliko,mfano wanasema rais ajaye akiwa muislam lazima damu imwagike,hatutaki kuongozwa na muislam namengine mengi tu.Mfano wa pili ni hapahapa JF utaona thread yenye jina la waislam comment nyingi ni za kutukana waislam na hapo utagundua ni jinsi gani wakristo walivyo na chuki kwa waislam.SWALI:Kwanini Dr.Slaa wakati wa kampeni Arusha alilala parokiani? Alienda kuchukua mawaidha gani? Nakusisitiza tena kama huna waraka kwa makanisa yote wakati wa uchaguzi utafute usome na ndio ulete hoja yako.Waislam hawahongwi na yoyote umdhaniaye ila sasa BASI! TUMECHOKA.
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  itakuwa vp 2015 2kimptisha Lowasa kugombea kw ticket ya CCM? Mtahamia kwa wakrc2? Acheni kudanganywa! Mta2mika mpk lin jaman? Hz shda za Tz mbna twazpata wte waislam na wakrc2?
   
 8. kessy kyomo

  kessy kyomo Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  jamani hali kama ndio hii sasa tunaelekea pabaya tunajua walianza zamani miadhara ya kidini lakini is too much hii siyi issue ya ccn hii ni issue ya waislam wote tanzania ndio tamko lao kwamba hawawataki wakristo sasa tujiulize mbona kipindi cha rais wetu mpendwa haya mambo ndio yamekuwa kwa kasi hivi mara radio iman mara miadhara hile ya tanga mwanza arusha mtwara yote kuisema dini ya kikristo sasa paka wanafikia hatua ya kusema wawavamie wakristo natoa angalizo kwa viongozi wa kikristo nanyi mtoe ombwe lenu kwani dawa ya moto ni moto hawa watu ni hatari sana sasa hivi badala ya kushindwa kuhubiri kwenye miadhara wameingilia kwenye mambo ya kisiasa kutumia mgongo wa kisiasa kufanya ghiriba zao sasa tunasema tunayahitaji hayo machafuko kwa hamu sana wanayoyahitaji wao tuko tayari kwa lolote kujilinda kama sisi wakristo na tuko tayari kwa lolote ikiwezekana kufa kwa ajiri ya hii fadhaa ambayo haiwezi kuvumilika kwani tunaona serikali yetu imekaa kimya sana kwa haya machochezi tunasema sisi wakristo tuko tayari kwa lolote kwa huu uchochezi wa kiislamu nawasilisha
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kama ndio hivyo, basi, jua tumefika mahali pasipo faa kama taifa. Kikubwa zaidi ni kwamba watu wenye kuamini hivyo hawajui wanachohitaji kutoka kwa watawala wao bali wanashabikia tu! Waibiwe, sawa tu kwamba bora mwizi awe wa dini yao, lol!
   
 10. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Moja ya mambo, ambayo ni uongo ni haya: Wanasema Kanisa Katoliki lina Jeshi linaloitwa Commission for Armed Forces na pia Wakristo wana jeshi pia linaloitwa Salvation Army. Unaweza kusikia haya kwenye baadhi ya mihadhara inayoendelea hapa Dar es Salaam.
   
 11. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Rais: Jakaya Mrisho Kikwete [ITIKADI KALI]
  Makamu wa Rais: Dr. Ghalib Bilal [ITIKADI KALI]
  Waziri Mkuu: Mizengo pinda [mtii-zitiini mamlaka zilizopo madarakani]
  Mkurgenzi wa usalama wa Taifa: Othman [ITIKADI KALI]
  Waziri wa Ulinzi: Hussein Mwinyi [Mshindi wa kusoma qurani]
  Waziri wa Fedha: Mustafa Mkulo/Kijjah [Kija ni ITIKADI KALI, Mkulo kawekwa kando kutokana na uislama koko wake]
  Wizara ya Mambo ya Ndani: Shamsa Nahodha [ITIKADI KALI]
  HIVYO VITENGO NDIVYO HUENDESHA NCHI SEHEMU YEYOTE DUNIANI.
  Viongozi walopewa dhamana ya kuongoza hizo taasisi wanaamini kuwa hivi sasa ndiyo wakati wa kuhamasisha waislam wapiganie nyadhifa mbalimbali kwa kuwahakikishia ULINZI na FEDHA. Jambo hili ni baya sana!!! Maana siku zote ACTION AND REACTION ARE EQUAL IN OPPOSITE DIRECTION. Maana yake watakapomaliza kuwashambulia wasio waislam watarudi kushambuliana wao kwa wao katika mtindo wa huyu ni muislam zaidi kuliko mwenzake [Angalia ilivyokuwa Afghanistan na Somalia]
   
 12. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kumbe na wewe umeshaambukizwa yule virus wa "waislam wanaonewa!!!!"
  1. Nyerere alipotaifisha Mashule na hospitali [nitajie idadi ya zile za kiislam na zile za kikristo zilizotaifishwa]
  2. Zanzibar ilikaliwa na waarabu ambako ndiyo chumbuko la uislam [waliacha shule na hospitali ngapi? vipi kuhusu vyuo?]
  3. Kipindi cha utumwa kuna waliopelekwa uarabuni na malaysia na kuna walopelekwa america [Niambie how many dissendants are in Arab country and how many are in Americas?]

  TAFAKALI HAYO MASWALI YANGU KWA UMAKINI MKUBWA JIBU UTAKALOPATA NAKUOMBA LITUNZE TU ROHONI MWAKO!!!!
   
 13. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Nikweli jeshi lipo hii hatuongopi,kama hujui kaakimya kwani wanaojua watakushangaa.Ushahidi nenda karejee Ripoti iliyosomwa kwa Papa John Paul 2 alipotembelea Tanzania ambapo hilo ilikuwa moja ya mafanikio ya kanisa nchini.Pili,jibu maswali yangu hapo juu na sio kupoteza muda.Ukweli ni kuwa hata mpinge hoja za waislam ni za haki ila mnaposema inajulikana tu kuwa nikauli za kujitetea na kujisafisha.
   
 14. k

  kibokogiziba Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAOMBA sote tujaribu kufikiri kwa makini madai ya waislamu: hawa si wajinga kiasi kwamba tuseme wanatumiwa kuna watu wanaacha kazi zao za msingi na kufanya tafiti juu ya hayo majadiliano na wakati wale wanaodai waislamu waongo utafiti mliofanya ni mdogo sana. mi ntakupa mfano kidogo ambao mtu yeyote hatoukubali bali rafiki zangu nilokua nao kwenye msitari katika taasisi moja kubwa sana ya elimu (UDSM) PALE NILIPOINGIA OFISINI ILI NIJAZIWE FOMU TU YA KOZI FULANI niliambiwa "TOKA NJE" na nilipouliza nini kosa langu nikaambiwa toka nje hapa si msikitini. baadae alipoingia rafiki yangu alihudumiwa bila tatizo lolote ndipo nikaona njia pekee ni kumpa rafiki yangu ile fomu akanipelekea na ikasainiwa. Acha hapo kuna watu wanaambiwa kabisa kwamba hutomaliza hapa degree kisa tu kaonwa anafuga ndevu. jamani acheni tu mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, nakwambieni wana jamiiforum fanyeni tafiti muone jinsi vijana wa kiislamu wanavyopewa mateso na wahadhiri, asilimia kubwa wanapewa sababu zisizo za msingi na kukatishwa masomo yao tena ni wengi na kama ukitaka nitakutajia na ukifuatilia GPA zao ni za juu hata huwezi tarajia na ndo utashangaa wanaosema hakuna udini ni wale waliopita straight bila kukumbana na vikwazo hivyo hawajui hali wanayokabiliana nayo wenzao. kuna mtu mmoja kasema yuko tayari kwa vita ukweli ni kwamba siku moja nimetamani na kujiuliza madhara haya waislamu wanapenda sana kuishi au? but its good at the moment nafurahia hii hali maana bora kufa kwa panga kuliko kuishi na watu wanaotufukuza maofisini bila sababu za msingi kisa tu umevaa kanzu. nimemaliza nitukaneni kama kawaida yenu maana uislamu kwenu sumu labada sukari kwa waislamu poa kma hao mnaowaoa na kuishi nao.
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Taifa lina mwaka wa sita sasa bila rais. Ila tuna aliyeshikilia hicho kiti mpaka rais atakapopatikana.
  Kwa upande wa hawa waislamu hatuna haja ya kuwahofia kwani hawa ni watu wanaoweza kutumiwa na kundi lolote, hata wewe ukitaka utawatumia.
  Sasa hivi wanaichukulia ccm kuwa ni chama cha kiislamu kwa sababu mwenyekiti ni muisilamu, hivyo sisiem itakapokuja na mgombea wa itikadi tofauti 2015, watakuwa na kazi ya kujiondoa kwenye choo cha kike walichojiingiza wenyewe kwa miaka 10.
  Watakapofanya kazi hiyo ya kujiondoa kwa miaka mingine 10, choo hicho hicho kitafagiwa n
  Kwa kupingwa rangi na watakaribishwa tena kikiwa cha bado ni cha kike.
  Watazurura hapo jangwani na utumwa wao hadi ezee wao, kwani ujinga ama ukichaa ni kuchagua.
   
 16. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Jamani serikali itawakemeaje hao wachochezi wakati yenyewe ndio imewatuma ikaeneze hiyo sumu ili kutetea maslahi yao?

  kwa hakika ni serikali ya ajabu kabisa kupata kutokea duniani ambayo ipo tayari kuangamiza watu wake kwa kulinda maslahi yao, kwa hakika inasikitisha sana, lakini haya yote yana mwisho time w'll tell. Na waislam wa kweli watabaini kwamba wanatumiwa.
   
 17. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mimi hayo yote uliyosema nimekwishayasikia live mara kadhaa kwenye kipaza sauti kikubwa hapa Ikwiriri ambako nipo kwa muda. Yanarudiwa kila siku. Ilinibidi nitafute sehemu ya mbali zaidi pa kupata moja baridi saa za jioni.
   
 18. A

  Anold JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Wanajisumbua tena wanapoteza muda wao bure. Mfumo wa serikali yetu hauna ubaguzi hata chembe kitakacho kubagua ni uwezo wako wa kitaaluma si vinginevyo. Hivi wanataka wataalam watoke madrasa? Kwenye chuo kikuu cha Kiislam kuna wahadhiri wakristo hiyo interview wamefanyiwa na Kanisa Katoliki? Hao wanaozunguka kueneza chuki ni lile kundi dogo la waislam ambao hawajui dunia ilipo kwa sasa. Hizi ni zama za sayansi na technologia, ukitaka uwiano nenda shule, peleka mwanao shule asome apasi vizuri awe mtaalam wa kuaminika!Akibobea kwenye elimu ya dini sio vibaya ila asiache na elimu dunia ili awe na uwezo wa kushindana na wengine matangazo ya kazi yanapotokea.

  Hao wanaozunguka sio waislam wasomi ni wale maamuma ambao hata waislam wenzao wanawashangaa maana hizo lawama zao hawajui zinatoka wapi? Huyo anayedai kuwa nchi hii inamfumo wa kikristo anajichanganya tu kwani bidii yao binafsi ndiyo inayofanya daiwa wawe mbele kwa kuwa wao pamoja na elimu ya dini ila mkazo mkubwa wamewekeza kwenye elimu ya dunia ambayo ndiyo inayohitajika. Mkristo yupo tayari kumsomesha mtoto wake kwa gharama yeyote elimu dunia sio elimu ya dini. Hata waislamu wanaofanya hivyo wamefanikiwa sana na wapo mbali.

  Hawa wachache wanaozunguka ni wale waislamu wavivu ambao kazi yao kubwa ni wivu wa dhahiri dhidi ya wenzao wenye maendeleo. Nchi nyingi za kiislam sasa zimezinduka kwenye dimbwi la usingi mzito wa kuamini kuwa misingi ya dini ingeweza kuwafikisha mbali, hawa sasa wameelimika maana wanachotafuta sasa sio kuenea kwa uislam bali maendeleo ambayo yatawatoa kwenye tope la umaskini na kuwapeleka kwenye uwanja mpana wa mafanikio.

  serikali yeyote sasa hivi itakayo inuka kwa misingi ya kidini ijue wazi kuwa itaangushwa na kusambaratishwa. Ndiyo maana dunia sasa inashuhudia nchi zilizokuwa zinaongozwa na viongozi waliotetea uislam na kuwakandamiza waislam zinasambaratishwa na waislam waliozinduka kwenye usingizi wakidini.

  Hao wanozunguka nchi nzima naamini wanajifurahisha na kupoteza muda wao maana mfumo wa nchi yetu pamoja na mwingiliano wa mahusiano (familia moja unaweza kukuta kuna waislamu pia wakristo) sio rahisi na haitawezekana kushawishi waislamu wa aina niliyotaja wawachukie ndugu zao. Hivyo badala ya kupoteza muda kupandikiza chuki ni afadhali watafute namna ya kujiendeleza ili waondokane na ujinga wa kupandikiza chuki zisizo na maana kwani kwa Tanzania yetu hii hawatafanikiwa kamwe vinginevyo wanatafuta kipigo kutoka kwa vyombo vya dola. Mfano mzuri ni lile suala la waislamu kupinga bucha za ngurue pale magomeni ambapo mzee mwinyi aliwapa kipigo cha mbwa wale waislamu waliokuwa wamejaribu kuandamana kupinga uwepo wa bucha za ngurue. Neno "ruksa" lilishika kasi kipindi kile.
   
 19. A

  Anold JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  hao waislam wanaozunguka kupandikiza chuki ni wale waislam wanaovaa kanzu na vibarakashia au ni wale wanaovaa suti?
   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio waislamu ila tatizo ni ukristo unaofundisha kuwa wavumilivu,kufundisha amani na upendo kwa vitendo, akupigaeshavu lakulia mgeuzie na la pili-sio jiuno kwa jino......................la sivyo vita inayopaliliwa na viongozi wa ccm hasa kikwete na ccm vya kidini vingelishatokea zamani tangukikwete na ccm walipoamua kuifanya ccm chama kinachoweza kushughulikia mambo binafsi ya dini fulani km mahakama ya kadhi...............................oci
   
Loading...