Serikali haina hoja juu ya uwezo huu wa Mahakama

Mwanakijiji unajidanganya.Hakuna mgombea binafsi mwaka huu.

ok labda niweke hivi; uchaguzi mkuu hautafanyika pasipo kuruhusiwa kwa wagombea binafsi/huru.. haijaliishi mwaka gani.. ila uchaguzi mkuu wowote utakaofanyika utakuwa na wagombea binafsi/huru.
 
Chama Cha Majambazi pamoja na kujifanya wanakubalika wanaogopa wagombea binafsi i.e. Wagombea hewa WHY?! Wanafahamu nini kitawapata.
 
ok labda niweke hivi; uchaguzi mkuu hautafanyika pasipo kuruhusiwa kwa wagombea binafsi/huru.. haijaliishi mwaka gani.. ila uchaguzi mkuu wowote utakaofanyika utakuwa na wagombea binafsi/huru.

Ha ha ha.ofcoz 2015 kutakuwa na mgombea binafsi but not this year.Practically haitawezekana.
 
huyu bwana aliyeandika hii nakala ndie aina ya watu waliotakiwa kuishauri mahakama, hii vita ambayo serikali imejiigiza katika suala hili itaicost huko mbele tuendako...suala la mgombea binafsi ni haki ya kikatiba na hata ukifanya utafiti, ni idadi dogo sana ya waTanzana ambao ni wananchama wa vyama vya siasa, CCM pamoja na kuwa chama kikongwe na chama tawala kina wanachama wasiozidi milioni 4 Tanzania nzima, na idadi ya watu kwa sasa inafikia milioni40 nchi nzima, kwa hiyo wakilazimisha viongozi watokanena vyama si sahihi kwani sehemu kubwa ya wananchi si wanachama wa vyama vya siasa na ni washabiki wa siasa, na hata viongozi wengi huchaguliwa na wannchi wasio na vyama maana kwenye uchaguzi mkuu wengi hutumia tu kadi za kupigia kura kumchagua kongozi wanayemtaka, sas kwanini iwe kwa Mgombea tu??? kama wananchi bila kujali kuwa ni wanachma a chama fulani wanaweza kuchagua kiongozi, kwani na mwananchi asiye na chama asiweze kugombea????

"Lengo kuu la serikali ni kuleta ustawi kwa wananchi"
 
Mwanakijiji na wajuvi wa sheria wengine na pia wana historia.

Hivi Kwa USA, zamani ilikuwa kwenye katiba kuwa WANAWAKE na WAUSI (Red Indian pia?) walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura.
Baadaye wakabadili ikawa Wanaume weusi wanaweza kupiga kura ila wanawake hamna. Mwisho ikawa watu wote wenye umri wa kupiga kura basi wanaruhusiwa kupiga kura (sina uhakika sana na mtiririko huo na si lazima sana).

Swali langu ni je, ili weusi na hawa wengine waweze kupiga kura, si ilibidi kwanza wabadili katiba? Ili Mweusi aweze kuowa/kuolewa na mweusi, si ilibidi wabadili katiba? Sasa ili kubadili, hii VITA ilianzia Mahakamani au ilianzia moja kwa moja kwa watu wanaoshughulika na katiba? (kwa USA sifahamu ni chombo gani.
Ila nafikiri hata wao, ingawa KATIBA ilisema hapana, nafikiri pia wao walitumia hili neno HAKI ZA BINADAMU kutengea hiki kifungu. Sijui kama niko sahihi.
 
hapana.. kesi ikiamuliwa Mahakama Kuu kwa misingi ya Kikatiba ile sheria inatenguka hawahitaji kubadili katiba! Bunge linatakiwa tu kutunga sheria kutekeleza hukumu ya mahakama.
 
What do you mean by 'practically haitawezekana'?

Sheria za uchaguzi zitawabana..Kuna masheria mengi tu yanahitaji kurekebishwa kwanza kwa muda tulionao najua hautoshi.Vimebaki vikao viwili au kimoja nadhani kabla Bunge halijavunjwa.
 
Sheria za uchaguzi zitawabana..Kuna masheria mengi tu yanahitaji kurekebishwa kwanza kwa muda tulionao najua hautoshi.Vimebaki vikao viwili au kimoja nadhani kabla Bunge halijavunjwa.

hukumu ya kwanza imetolewa 1995 (hawakujiandaa), hukumu ya pili imetolewa 2005 hawakujiandaa.. huu ni 2010 kwanini unafikiria ikifika 2015 watakuwa wamejiandaa?
 
jamani acheni kujifurahisha, kabudi na masaju wako gado kabisa................ hakuna mgombea binafsi mwaka huu............ na mahakama yote (hadi hiyo ya rufaa) havina uwezo wa kubadili wala kujadili katiba........... kama katiba ni mbovu itarekebishwa na bunge na kwa utaratibu ulioanishwa kikatiba na si mahakama.......... hata kama kifungu cha katiba kinachodaliwa si cha "kikatiba" mahakama haina uwezo w a kufanyia judicial rview na tunapaswa kuwabana waabunge wetu wakifute kwenye katiba na si njia ya mkato ya akina mtikila............ lakini namshukuru tikila harakati zake zinatufungua sana macho.......... mtikila alipaswa kuingiza hoja sake bungeni na si kukurupukia mahakamani.........

kama hata hili nalo hamuelewi, subirini mahakama hiyohiyo ya rufaa itawaelewesha soon..................
 
Ukiona umedhulumiwa haki yako utaenda wapi kulalamika?
 
Ukiona umedhulumiwa haki yako utaenda wapi kulalamika?

inategemea ni haki gani na nani aliyekudhulumu.......... katiba ikikudhulumu, huwezi kwenda mahakamani kama unajua sheria japo main principles.......... ila sheria ikikudhulumu hapo mahakamani ndio muafaka.......... kazi ya katiba si kuweka haki, bali kutambua na kulinda haki, so kama kitu kiko ndani ya katiba, jua kimetambuliwa tu lakini kitatolewa kulingana na kwa mujibu wa sheria............

hapa imefanyika technical error...... na tukubali kuwa ndio mapungufu yetu, kama tungeshikamana na mtikila toka hukumu ya kwanza, leo tungekuwa tunashangilia ushindi, lakini kwa vile tulimwona ni mzee wa makesi ya kila siku tukampuuza kama mwendwazimu, ndio sasa tunaona alichokuwa akipigania kina umuhimu......... tulipaswa kukipinga kifungu hiki hata kwa maandamano ili kulishinikiza bunge likibadili lakini wapi, hata CUF mabingwa wa maandamano hawajwahi kushinikiza hili.......... wako tayari kuandaman kuunga mkono kuwa Yesu si Mungu lakini wakichekelea mambo ya msing kama hili............... watanzania tuna safari ndefu sana.......
 
Nakusikia lakini tatizo ni kuwa mahakama mara zote imekuwa ikitoa agizo kutokana na nguvu zake kutaka wahusika wasahihishe walichoharibu. Lakini serikali inajaribu kujiweka nje ya maagizo ya mahakama. Mahakama isipokuwa na uwezo wa kuagiza kilichoharibiwa (baada ya kukikuta hivyo) kitengenezwe ni jinsi gani wahusika watatekeleza? Kwenye suala la Valambhia ilikuwa hivi hivi.. Hivi majuzi sehemu moja huko US mahakama imetaka school district kuondoa sera za kibaguzi kwa wanafunzi na kuwapa vipimo vya kutumia. Hiyo ni sehemu ya judicial review.

sehemu ya hukumu ya Manento inasema hivi:

Huo msisitizo ni wa kwangu. Mahakama haikuweka utaratibu wa wagombea binafsi uwe vipi hapo ingekuwa inatunga sheria kama maprofesa wanavyodai. Mahakama haikufanya hivyo... imeweka muda (kitu ambacho inauwezo wa kufanya) na kutaka Bunge litengeneze mazingira ya kuwahusisha wagombea binafsi. Hii ilikuwa in 2005. Kumbuka alisema hivyo kwa sababu katika hukumu ya Lugakingira licha ya kuruhusu wagombea binafsi lakini kulikuwa na ombwe, serikali haikufungwa kulazimishwa kuweka mazingira ya wagombea binafsi ndio maana in 2000 na 2005 hakukuwa na utaratibu huo. Manento ameremedy tatizo hilo kwa kuwaambia serikali waandae utaratibu huo by 2010. Sasa leo serikali ikisema haina muda mimi naona ni wapuuzi kwa sababu they have had 4 years to take heed ya agizo hilo la mahakama na wamekataa defiantly.

Mzee Mwanakijiji, asante kwa kutunyofolea sehemu ya hukumu ya Maneto, ukiweza kutupa yote mkuu utakuwa umecheza heko sana.

Nadhani hili swala linahitaji ujuzi mwingi wa sheria na ndo maana hata wanasheria wenyewe hawakubaliani kuhusu nini mahakama inaweza kufanya na nini haiwezi, naamini hata majaji wanaosikiliza kesi hii wanaweza kuwa na maoni tofauti ( by the way, ni ktk mazingira gani mahakama huwa inaomba ushauri toka kw a marafiki wa mahakama? nisaidie ktk hili). Just hope hukumu itakayotolewa itaruhusu mgombea binafsi kwani hapo tutakuwa tumepiga hatua kuelekea kwenye demokrasia ya kweli.
 
Back
Top Bottom