Serikali haikagui vyakula, kipi kinawazuia wenye migahawa kupika mizoga, mchele wa plastiki, viungo expired, mafuta ya transfoma / nguruwe, n.k

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
-kuweka hamira kwenye wali
-kupika nyama zilizokaa mda mrefu (kuna namna ya kukata harufu),
-kupika mizoga (zipo tetesi kuku wanaotupwa hukaangwa na kuuzwa buku kipande)
-viungo viungo viliyo expire kama mchuzi mix, royco na nazi za kwenye makopo.
-kutumia mafuta ya transfoma ama ya nguruwe ambayo ni bei rahisi
-kupika mchele wa plastiki
-kuchanganyiwa chakula cha jana na chakula cha leo
-n.k.

Serikali haina chombo maalum kukagua vyakula, Hali hii inawazuiaje mama ntilie, wenye migahawa, wenye hoteli, n.k. wasishawishike kufanya mambo tajwa hapo juu.

Hali hii inaenda mbali zaidi, kwenye migahawa ya mtaani unaweza kuta mwenye mgahawa anajipikia chakula chake, hali chakula anachowapikia wateja, hii huwa inatia mashaka.

Huenda hali hii ndiyo inayosababisha hata vijana wengi kupata matatizo mazito ya kiafya.
 
Vingine wanashindwa kuvifanya maana hakuna siri chini ya jua,kumbuka ana wahudumu kibao ambao mabwana zao huja kula chakula hicho,kwahyo kama kitakuwa ni kibaya wale wafanyakaz wake lazima wavujishe siri na wasingeweza kukila wao pia

Hilo haliwezekani,bali litawezekana kwenye vyakula vinavyoweza kuandaliwa na mtu mmoja au wawili kama chips na mishikaki
 
Nguruwe?????????
Soma huu uzi, mafuta ya nguruwe yamekuwa ni bei rahisi mno,

Wenye migahawa wakishawishika kuyatumia nani wa kuwazuia ??

Vingine wanashindwa kuvifanya maana hakuna siri chini ya jua,kumbuka ana wahudumu kibao ambao mabwana zao huja kula chakula hicho,kwahyo kama kitakuwa ni kibaya wale wafanyakaz wake lazima wavujishe siri na wasingeweza kukila wao pia

Hilo haliwezekani,bali litawezekana kwenye vyakula vinavyoweza kuandaliwa na mtu mmoja au wawili kama chips na mishikaki
wengi wanaofanya kazi migahawani ni familia au ndugu wa karibu,,,,,, damu nzito kuliko maji.
 
Swala la mlo ni kitu muhimu sana lakini ajabu ni kwamba serikali imekuwa haina chombo kinachoenda kukagua ubora wa chakula kinachouzwa mitaani na hata mahotelini, yawezekana chombo kipo ila wanakaa tu ofisini.

Hali hii inawazuiaje mama ntilie, wenye migahawa, wenye hoteli, n.k. wasishawishike

-kuweka hamira kwenye wali
-kupika nyama zilizokaa mda mrefu (kuna namna ya kukata harufu),
-kupika mizoga (zipo tetesi kuku wanaotupwa hukaangwa na kuuzwa buku kipande)
-viungo kama nyanya na nazi za kwenye makopo zilizo kwisha mda wake
-kutumia mafuta ya transfoma ama ya nguruwe ambayo ni bei rahisi
-kupika mchele wa plastiki
-n.k.

Hali hii inaenda mbali zaidi, kwenye migahawa ya mtaani unaweza kuta mwenye mgahawa hali chakula anachowapikia wateja, hii huwa inatia mashaka.

Binafsi nimewahi kuona video kuna mchele ulikuwa umeharibika ulienda kumwagwa lakini kuna wamama wanaodaiwa ni mama ntilie wakaenda kuufukuana kuupepeta upya, sasa sijajua kama ulirudi mtaani ama walienda kulisha kuku zao.

Huenda hali hii ndiyo inayosababisha hata vijana wengi kupata matatizo mazito ya kiafya.

Serikali inalinda vipi wanachi wasilishwe vitu dhaifu kwa tamaa za wenye migahawa
Mabwana afya wenyewe corrupt vibaya mno siku hizi
 
Vingine wanashindwa kuvifanya maana hakuna siri chini ya jua,kumbuka ana wahudumu kibao ambao mabwana zao huja kula chakula hicho,kwahyo kama kitakuwa ni kibaya wale wafanyakaz wake lazima wavujishe siri na wasingeweza kukila wao pia

Hilo haliwezekani,bali litawezekana kwenye vyakula vinavyoweza kuandaliwa na mtu mmoja au wawili kama chips na mishikaki
👍
 
Uzalendo ni somo la lazima kwa kila raia....lifundwishwe vyema na kuhubiriwa vyema ndani ya familia ,misikitini na makanisani.....

Ila mwisho wa yote ni MOYO....moyo wake huyo aliyefundishwa huo uzalendo.....

#Siempre JMT🙏
 
Huo uzalendo kwa sasa unakuwa taabu sana.

wanasiasa wamekuwa wakidanganya sana wananchi, huo uzalendo utoke wapi?
 
Serikali tangu lini ilifanya biashara ya Mama ntilie?

Uliza hivyo wateja hautapata na automatic biashara itakushinda na kuchafua jina lako,
Hata uje Kupika vyakula halali na vizuri hautauza
 
Huo uzalendo kwa sasa unakuwa taabu sana.

wanasiasa wamekuwa wakidanganya sana wananchi, huo uzalendo utoke wapi?
Mwananchi asiposoma ALAMA ZA NYAKATI kutani.....

Mwanasiasa/wanasiasa wasipozisoma ALAMA ZA NYAKATI kutani......

Basi....
Basi....
Basi....

#Siempre JMT🙏
 
Ukitaka kujua kuwa Tanzania ni pagumu anza kufanya hayo mambo. Ndani ya miezi 3 tu usipokamatwa basi biashara inakufa. Labda kama ufanye hayo yote bila mwingine yoyote kujua.
 
Ukitaka kujua kuwa Tanzania ni pagumu anza kufanya hayo mambo. Ndani ya miezi 3 tu usipokamatwa basi biashara inakufa. Labda kama ufanye hayo yote bila mwingine yoyote kujua.
Haya mambo labda ni mpaka uwe unafanya wazi wazi na hapo wateja watakukumbia ila sio kukamatwa maana vitu hivi vishazoeleka, umewahi kusikia kesi ya mgahawa unaofanya haya mambo mahakamani ?

wengine washakua wazee kabisa wanafanya biashara kwa mtindo huu mpaka sasa.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Haya mambo labda ni mpaka uwe unafanya wazi wazi na hapo wateja watakukumbia ila sip kukamatwa maana vitu hivi vishazoeleka.

wapo washakua wazee kabisa wanafanya biashara kwa mtindp huu mpaka sasa.
Ni ngumu japo hii nchi ni kubwa hivyo inawezekana.
 
Back
Top Bottom