Serikali boresheni huduma ya M-KILIMO

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari za wakati huu wanajukwaa wenzangu.

Kwanza napenda kuipongeza serikali kupitia wizara ya kilimo hasa kwa kuanzisha huduma ya M-kilimo ambayo kwa kiasi kikubwa ni mkombozi kwa wakulima hasa vijijini ambako ni vigumu mabwana na mabibi shamba kufika huko.

Tatizo kubwa la huduma hii ni kuchelewa kupata mrejesho au majibu kuhusu maswali unayouliza licha ya kwamba majibu yake huja vizuri.

Siku moja nilijiunga na huduma hiyo ya M-kilimo nikakaa taarifa zangu lakini cha ajabu majibu nikaja kupata baada ya wiki moja na zaidi licha ya kuunganishwa na afisa ugani pia kwenda ofisini kwake kwenye shamba darasa kila Jumatano ili kwenda kujifunza.

Natamani majibu yangekuwa yanatoka isizidi siku 3

Jinsi ya kujisajili na m-kilimo kwa watakao hitaji

~Piga *152*00#
~Chagua kilimo uvuvi na mifugo
~Chagua M-kilimo kisha kuna machaguzi mengi hapo kutokana na hitaji lako
~Jaza taarifa zako hasa eneo unaloishi
~Baada ya muda watakuunganisha na Afisa Ugani wa eneo lako kwa upande wangu alinipigia simu kabisa

Ni huduma nzuri ila inachelewa kuleta majibu ya maswali yetu wananchi

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Habari za wakati huu wanajukwaa wenzangu.

Kwanza napenda kuipongeza serikali kupitia wizara ya kilimo hasa kwa kuanzisha huduma ya M-kilimo ambayo kwa kiasi kikubwa ni mkombozi kwa wakulima hasa vijijini ambako ni vigumu mabwana na mabibi shamba kufika huko.
Wawe na app kwenye android ambayo itakuwa ina live chat kwa muda wa kazi pia hii itapunguza urasimu na uzembe kama upo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom