Serikali awamu ya Sita ni butu? Makampuni ya simu yameipuuza

Nafikiri baadhi ya mitandandao wanafanya price discrimination, kwangu mimi offer ziko vizuri 1000tsh napata 1gb, dk 100, na sms 1000, laini zangu zote tigo na voda napata hii offer.
Ila kuna mtu kwa buku hapati kifurushi hicho.
Uko sahihi, it seems kila mtu anapewa price ya bando kivyakevyake tofauti na mwenzake
If that is the case kwanini serikali isitoe bei elekezi? kuna haja gani kuwaambia washushe gharama zao kama mwisho wa siku kila mmoja ataamua ashushe kwa kiasi gani? au asishushe kabisa?

Hii issue imekaa kisanii sana, inawezekana serikali na makampuni ya simu wanaijua siri kati yao ndio maana serikali iko kimya, hasa ikizingatiwa kodi kubwa hayo makampuni ya simu yanayolipa kwa serikali.
 
Moja kati ya udhaifu mkubwa sana wa Watanzania ni upotezaji wa kumbukumbu hata kwa jambo ambalo halina hata miezi 6; kwani ile issue ya kuongeza bei za vifushi vya internet ilitamkwa lini na nani? Sio waziri muhusika tena enzi za mwendazake? Tusiisingizie awamu ya sita, tusiyasingizie makampuni ya simu. Lawama au pongezi ziende kwa muhisika
Lakini mkuu mama alitoa maagizo kwenye kampuni zote za cm zi angalie upya ziache kuumiza wanainchi au wewe hukumsikia,sasa hivi tunataka kuona utendaji wake hayo mambo ya mwendazake amesha enda maisha lazima yaendelee. Kwa sababu yeye ndio kashika usukani,mbona wateule wa mwendazake kawapangua hili linamshindaje?
 
Kabisa mkuu, yaani huyu mama hakuna kitu kabisa naona tunarudi kwenye enzi za MSOGA na wale watu wa kauli mbio ya UNANIJUA MIMI? wameanza kurudi mjini, tena kwa kasi ya ajabu kuliko mwanzo
Endeleeni kupiga kelele, ila kampeni zenu zitafeli. Hizo bei kubwa za bando zilipandishwa na huyo mnayemsifia. Wanafiq tu nyinyi. Wakati Zantel kwa 1500 unapata gb 1.5 kwa wiki. Uchawi sio lazima mbebe tunguri.
 
Lakini mkuu mama alitoa maagizo kwenye kampuni zote za cm zi angalie upya ziache kuumiza wanainchi au wewe hukumsikia,sasa hivi tunataka kuona utendaji wake hayo mambo ya mwendazake amesha enda maisha lazima yaendelee. Kwa sababu yeye ndio kashika usukani,mbona wateule wa mwendazake kawapangua hili linamshindaje?
Nashukuru mkuu kwa kuja tena, binafsi sikumsikia mama but kupitia maneno yako mwenyewe,) kama umemnukuu vizuri), kwamba mama alisema "kampuni za cm ziangalie upya, ziache kuumiza wananchi". Hilo neno/sentesi ziangalie upya lina maana gani kwako? Huwezi kujua, huenda wameangalia upya kweli na wakaishawishi serikali (ambayo of course kwa msimamo wangu, ni serikali ndio iliopandisha kupitia Ndungulile) na serikali ikaamini na mambo yanaendelea. Sipendi bei hizi mpya cause hata mimi zinaniumiza but ukifanya utafiti mdogo, bado Tanzania tuna unafuu wa bei za internet kulinganisha na nchi nyingi.
 
Natafakari sana haya makampuni ya simu kuigomea serikali kupunguza bei ya vifurushi. Katika awamu ya tano tulijionea, serikali ilikuwa ikiamua jambo lake, watendaji waliwajibika kwa wakat na kwa speed mujarabu. Tunajionea kwa macho na kwa vitendo awamu hii ya Sita ipo slow sana inaenda sawia na sauti ya upole na ya taratibu ya rais mama yetu Samia.

Takiriban miezi miwili sasa Wananchi tunapigwa punch za uso na makampuni ya simu kwenye bei ya vifurushi kuwa juu, hatimaye Wwnanchi wameanza kuizoea hali hii.

Huko mbele Kuna hatari tutakuja kujionea kila taasis za binafs zitoazo huduma kujipandishia bei watakavyo, mfano shule binafsi zitapandisha ada na kuongeza michango na kwani serikali ni butu, hii ni mfano Michache. mapovu ruksa.
Mbona Makampuni yote wameshusha waliambiwa waachane na bei mpya(elekezi)na waendelee na bei zao za zamani na wamefanya hivyo sasa kelele zinatoka wapi tena?
 
Endeleeni kupiga kelele, ila kampeni zenu zitafeli. Hizo bei kubwa za bando zilipandishwa na huyo mnayemsifia. Wanafiq tu nyinyi. Wakati Zantel kwa 1500 unapata gb 1.5 kwa wiki. Uchawi sio lazima mbebe tunguri.
WAPIGAJI mnakuja kwa nguvu zote kutetea upuuzi!
 
Hawajutii chochote mkuu, wamefanya usanii hapa na pale - lakini either way wame-peg major/popular bundles predominantly kwenye 500Mb, wanacho ongeza ni muda wa maongezi wakati wateja wanacho gomba ni bundle za data sio voice.

TCRA wakumbuke kwamba wananchi karibu wote wanajifunza mengi kupitia kwenye mitandao na sio kwenye maongezi na simu - hilo wala Serikali yetu ilioni wana wachia makampuni ya simu yafanye yapendalo bila wasi wasi wowote - we fikiria kampuni hizi zilivyo za ajabu kidogo - mfano Airtel bundle ya UNI wameifanyia usanii na mamlaka husika wako kimya kabisa, mamlaka hii hii iliahidi wananchi pamoja na Rais kwamba wata hakikisha charges zitarudishwa kama zilivyo kuwa tangu mwanzo - sasa huu mwezi wa ngapi tangu TCRA itoe ahadi?
Hapana hapa mwenye kosa ni TCRA sio VODA au TIGO..... muongozo unataka MB moja iuzwe mpaka Tsh 9 max. Kwa mahesabu hayo hizo 500 MB wakisema wauze bei halali ndio mkaanza lalamika MB 500 kwa elfu 4 and so on.

JPM alitaka kodi zaidi so akapandisha bei elekezi so lazima mitandao ya simu nao iweke cha juu ipate faida. Kwa ssa Halotel anauza chini kabisa ya bei Elekezi yaani Tsh 2 mpaka 1.8 kwa kila MB ila watu bado wanalia. Kwenye zile bei mpya Voda ilifanya 4.5 Tsh kwa 1 MB lakini kelele zikazidi na ilikua nusu tu.

Wa kulaumiwa ni TCRA wakishusha madai na bundle zitashuka tu automatically
 
Bando bei zake zilipanda kipindi cha hilo jiwe lako, au umesahau? Jiwe was nothing and curse for this nation. Let him die again where he is.
Nawe utakufa tu. Utamkuta jiwe ni kiongozi wa malaika huko mbinguni
 
If that is the case kwanini serikali isitoe bei elekezi? kuna haja gani kuwaambia washushe gharama zao kama mwisho wa siku kila mmoja ataamua ashushe kwa kiasi gani? au asishushe kabisa?

Hii issue imekaa kisanii sana, inawezekana serikali na makampuni ya simu wanaijua siri kati yao ndio maana serikali iko kimya, hasa ikizingatiwa kodi kubwa hayo makampuni ya simu yanayolipa kwa serikali.
Kuna tatizo hapo, mimi naona wanafanya bei tofauti kwa kila mteja, kuna rafiki yangu bila 3000 hawezi pata hizo offer mimi ninazo.
 
Natafakari sana haya makampuni ya simu kuigomea serikali kupunguza bei ya vifurushi. Katika awamu ya tano tulijionea, serikali ilikuwa ikiamua jambo lake, watendaji waliwajibika kwa wakat na kwa speed mujarabu.

Tunajionea kwa macho na kwa vitendo awamu hii ya Sita ipo slow sana inaenda sawia na sauti ya upole na ya taratibu ya rais mama yetu Samia.

Takiriban miezi miwili sasa Wananchi tunapigwa punch za uso na makampuni ya simu kwenye bei ya vifurushi kuwa juu, hatimaye Wwnanchi wameanza kuizoea hali hii.

Huko mbele Kuna hatari tutakuja kujionea kila taasis za binafs zitoazo huduma kujipandishia bei watakavyo, mfano shule binafsi zitapandisha ada na kuongeza michango na kwani serikali ni butu, hii ni mfano Michache. Mapovu ruksa.
Mzee watu wakiongea wananyamazishwa kwa neno la SUKUMA GANG,wacha tunyamaze kimyaaa maana serikali ya sasa ni kwa hisani Ya Team Msoga na Chadema
 
Ni butu haswaaaa!!

Suala la umeme ni kero kubwa sasa, huku kwetu umeme unakata kila wanapojisikia tu, iwe Asubuhi, mchana, jioni na hata usiku mmelala unastukia tu tayari hakuna umeme, na hata huu muda navoandika hivi, washakata umeme, na hawatoi tarifa

Tutaachaje kusema ni serikali butu?
 
Kwa sababu mnasoma humu ombi letu ni kurudisha pia vile vifurushi vya usiku vya Data kama Amsha popo cha Airtel, Voda, Tigo, Zantel, TTCL pia Halotel waongeze ukubwa irudi Unlimited. Hii inasaidia wale wanaopakua vitu vikubwa kwa kuacha kifaa on kisha kulala ikifika asubuhi mambo safi. Please tunawaomba.
 
Tanzania ni nchi yeye raia wanaolalamika kupita kiasi dunia nzima.

Yaani vifurushi hivi bado kuna watu wanataka vishushwe zaidi..Haya makampuni yataendelea kweli?.

Kodi serikali inataka kubwa na nyie mnataka muuziwe 1gb kwa jero.

Wabongo bhana.
 
Nafikiri baadhi ya mitandandao wanafanya price discrimination, kwangu mimi offer ziko vizuri 1000tsh napata 1gb, dk 100, na sms 1000, laini zangu zote tigo na voda napata hii offer.
Ila kuna mtu kwa buku hapati kifurushi hicho.

Hiyo inaitwa ‘Ya kwako tu’ unapewa offer kulingana na profile lako, cha ajabu mtumiaji mzuri ndiye anabanwa kwenye offer!
 
Back
Top Bottom