Serengeti: Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu azindua Jeshi jipya nchini

Maendeleo yanakuja kwa kasi mno;
Wanyamapori na misitu ni sehemu muhimu ya kuchangia pato laTaifa ni muhimu kulilinda kwa gharama yoyote Ile.
 
Inabidii watumie vifaa vya kisasa kama spy drones zitakazorushwa hifadhani na kupiga picha ili kuwanasa kirahisi majangili.
 
Na sisi tuliopitia jkt tunaweza pata ajira huko, tumehenya vya kutosha!!

Juzi tu zilitolewa nafasi za askari zaidi ya 100, sifa moja wapo ilikuwa ni form four mwenye mafunzo ya JKT. Kwa hiyo askari toka JKT wataweza kuajiriwa kama kawa.
 
Wajuzi tafadhali naomba mwenye ufahamu juu ya Muundo wa jeshi usu LA Wanyamapori/Misitu lililozinduliwa juzi name Makamo wa Rais ukoje, na je Wahifadhi wengine wa Wanyamapori na Misitu waliopo Halmashauri za Miji/Majiji/ Manispaa na Wilaya watajuishwa ktk Jeshi hili? Kama ndivyo ni kwa namna gani, je nalo litakuwa na Kamanda Mkuu mmoja Kama yalivyo yalivyo majeshi mengine? (Polisi, Magereza, JWTZ, Zimamoto na Uokoaji kwa uchache) Vyeo/ Kamisheni kwa Askari vitatolewa na Nani kwa utaratibu upi? Naomba tuelimishane bac kidogo wadau
 
Nadhani muundo na karibu kila kitu wameshakiweka mtandaoni.
Huku ukisubiri majibu humu pitia na mtandaoni pia.
 
Back
Top Bottom