Sera za kusimamia maadili "kutumbua majipu" zitafanikiwa zikifanyika kitaasisi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
serikali kwa sasa inatekeleza mkakati mkubwa ambao unaitwa kutumbua majipu ambao umejizolea umaarufu mkubwa.

mkakati huu unaweza kukwama kutokana na utekelezaji wake kusimamiwa na watu na sio taasisi.

upo uwezekano wa majipu haya kutafuta mbinu za kujilinda kwa kuwachafua watumbuaji ili kuwanyamazisha. tunajua tulikotoka na hivyo yawezekana kumpata mtu aliyekuwa kwenye system ambaye ni malaika ni vigumu. hivyo majipu haya yanaweza kuanza kutafuta ushetani wa watumbua majipu hawa na kuuleta ili kulimaliza nguvu zoezi la utumbuaji wa majipu.

lakini pia jamii zetu zinaamini sana habari za mitaani hivyo upo uwezekano wa habari nyingine kupikwa pia na jamii ikazibeba.

wapo watu walikuwa mstari wa mbele kutumbua majipu lakini kwa sasa wako kimya baada ya wao kuhusishwa katika tafrani fulani. kwao yawezekana wanaona kukaa kimya pengine kunaweza kuwa nafuu maana wakiibuka tu ya kwao yanakumbukwa.

yawezekana wapo waliokuwa wakijiadaa kutumbua lakini baada ya kuona upo uwezekano wa yao ya nyuma kuibuliwa wanaanza kusita.

kama shughuli hizi zitasimamiwa na taasisi na sio mtu mmoja itakuwa vigumu kuichafua taasisi kwa kumlenga mtu mmoja na hivyo utumbuaji utakuwa endelevu.
 
Back
Top Bottom