Sera za CCM dhidi ya Sera za CHADEMA

Sadock Kabuko

JF-Expert Member
Mar 26, 2013
1,171
1,080
Nimekuwa nikifuatilia kampeni za CCM na CHADEMA, kuna utofauti mkubwa sana wa sera kati ya CHADEMA na CCM,

Sera za CCM imejikita kueleza yafuatayo kwa wananchi

1. Kujenga miundo mbinu wezeshi kumrahisishia mwananchi kufanya shughuli zake kwa urahisi mfano. barabara, ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege, ununuzi wa meli, upanuzi na ujenzi wa bandari
2. Kuboresha huduma za afya na maji i.e kujenga vituo vya afya, zahanati, hospitali, kununua madawa na kuhakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika
3. Kufanya mapinduzi ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu
4. kutengeneza ajira n.k
5. Kusambaza umeme vijijini kwa 100%
6. kutatua kero za wananchi

Sera za CHADEMA na vyama vingine
1. Magufuli amejenga madaraja, SGR na amenunua ndege, barabara,madaraja atachaguliwa na vitu sio watu
2. Magufuli amajenga uwanja wa ndege Chato
3. Magufuli hana cheti cha kuzaliwa
4. CCM watatuibia kura na uzushi mwingine
5. CCM inatumia wasani kujaza viwanja-mikutano yao

NB: CHADEMA, ACT n.k wanajikita sana kushambulia mambo mema yaliyofanywa na CCM wamesahau mpaka kunadi sera zao nawakumbusha tu October sio mbali ule mchezo wa kulialia kwamba mmeibiwa kura, Wananchi wanaangalia na kusikiliza sera na sio makanjanja mengine.
 
Umeiona 'Chopa' ya CCM lakini? Hivi ile 'Chopa' kabisa wana CCM hasa akina Bashiru na Polepole wamekubali JPM aitumie? Ngoja 'nijinyamazie' tu.
 
Umeegemea upande mmoja sana kiasi cha kukera na kutia kinyaa sana. kwa ufupi hii mada haina hadhi ya kujadiliwa kwa hoja hata kidogo. Kitu pekee unachokistahili kwenye huu uzi wako ni matusi mazito mazito.

Umesahau sera za CDM ambazo Magufuli anaishia kuzitusi na kuzipiga vijembe kwamba 'hazitowezekana'?
 
Magufuli amesema ".wananchi msiwapigie kura wabunge wa upinzani hata kama ni wazuri".

MAGUFULI 2020.
 
Kifupi CCM tunanadi tuliyofanya ambavyo wananchi walitutma tufanye kama kujenga barabara shule vituo vya afya umeme elimu bure nk wakati Chadema wananadi vitu hewa ambavyo wananchi hawakuwatuma wabunge au madiwani wao walioiwachagua uchaguzi uliopita
 
Tunataka cheti X3..nilisikia walevi kilabuni wakiimba hiko kibwagizo
 
Kuna maccm kama Polepole yana DHAMBI. Unafunga MIRIJA ya UCHUMI Nchi nzima. Wananchi wanalia NJA.

Wakisema vyuma vimekaza eti unawafunga badala kufungua mirija ya Uchumi.

Huu ujinga wote unafanywa ili uweze kuwaDHIBITI siku ya UCHAGUZI kwa kuwapa buku mbili wajaze viwanja.
 
Wakipata asilimia 12 ya kura watasema tume inaundwa na watu wa CCM hawatakumbuka kuwa kampeni zao ni “mashudu” matupu.
 
Wakipata asilimia 12 ya kura watasema tume inaundwa na watu wa CCM hawatakumbuka kuwa kampeni zao ni “mashudu” matupu.
Ukipiga kura ya rais kwa Tundu Lissu, ujue unapiga kura ya katiba mpya, ujue unapiga kura kwa rais ambaye atarudisha uhuru na haki za wananchi, ujue unapiga kura kwa rais ambaye hatawasimanga..".Tundu Lissu. #Uchaguzi2020

Achana na takataka za ccm
 
Kwanini nimpigie kura mtu aliyemdhihaki mwasisi wa taifa hili ndani ya bunge wakati naweza kumpigia kura mtu anayemuenzi kwa vitendo?.
 
Sera za CHADEMA na vyama vingine
1. Magufuli amejenga madaraja, SGR na amenunua ndege, barabara,madaraja atachaguliwa na vitu sio watu
2. Magufuli amajenga uwanja wa ndege Chato
3. Magufuli hana cheti cha kuzaliwa
4. CCM watatuibia kura na uzushi mwingine
5. CCM inatumia wasani kujaza viwanja-mikutano yao
Unamasikio lakini husikii na una macho lakini huoni. Mwisho kabisa una ubongo lakini umekataa kuufikirisha. Tumekuelewa.
 
Back
Top Bottom