Sera ya viwanda ikitimia 2020 nitahamia CCM

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kwa mwendo ninaouona, kupitia maaamuzi ninayoyaona yakifanywa na utawala wangu wa Serikali ya sasa sina budi kusema ahadi ya Tanzania ya viwanda ikitimia kabla ya 2020 nitavaa kofia,viatu,T-Shirt,koti na socks zenye nembo ya CCM.Sitahitaji maswali mengi kwasababu nitakuja nimetimiza nilichoahidi leo.

Tuombeane uzima kufikia muda huo maana kuna baadhi ambao hawataweza kuiona Tanzania ya viwanda.Nisipoiona Tanzania ya viwanda nitaamini kua mabadiliko chini ya CCM ni ndoto labda upinzani ambao haujawahi kutawala.Wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu 2020 CCM wajiandae kwa moyo mweupe kukabidhi Dola maana watakua wameshindwa kazi.
 
Hapa mtazamo wa elimu nao utazamwe upya,maana wanaoenda kufanya kazi kwenye hivyo viwanda ni watu.Watu wasome hasa ufundi.Wanafunzi waanze kufundishwa stadi za ufundi wakiwa ngazi za chini za elimu.
 
Ni kawaida sana wagombea kutoa ahadi nyingi na kuzitekeleza hawawezi..
 
Kwani wewe unamsada gani na ccm kwaujumla hahaha mbona vituko
Wewe kama nani ukihamia ccm ione kuna manufaa !!!
Mmeishiwa
 
Kwani wewe unamsada gani na ccm kwaujumla hahaha mbona vituko
Wewe kama nani ukihamia ccm ione kuna manufaa !!!
Mmeishiwa
Soma argument yake uielewe kwanza ndio ubwabwaje. Wewe eleza unadhani kwa nini sera ya viwanda itawezekana kabla ya mwaka huo, hiyo ndio namna bora ya kujadiliana.
Hivi tatizo lako ni elimu au kwa sababu unetoka kabila lenye asili ya ubishi tuu?
 
Kiwanda cha helikopta na gari aina ya kaparata tayar vimeishaonesha ni nchi ya viwanda!!!hahhahaaha yaaan kweli hii ndo tanzania ya maigizo full kukurupuka,,ngoja tuone mwisho wapicha
 
Kwani wewe unamsada gani na ccm kwaujumla hahaha mbona vituko
Wewe kama nani ukihamia ccm ione kuna manufaa !!!
Mmeishiwa
Kwa nini mashoga wanaongezeka mjini hiyo tabia sio nzuri ya kuchezewa tope iache mkuu
 
Haitokuja itokee mkuu. Kwa kigoma imeshakuwa Dubai au viwanja vya ndege alivyosema jk au meli kubwa nne kwenyw miji yote inayotegemea meli walishapat. Ukifikiria hivyo tu. Hutokuja.ukakaa uiamini ccm hata mwaka moja.
 
Mwaka unakaribia kwisha Mukulu wa Mukulu bado anaunda serikali,kumbuka bado makatibu taarafa,vijiji na mitaa
. Akimaliza tutaanza kujenga viwanda
 
Mkuu Mahanju
Usitake kunichekesha nimetoka kushuhudia mahoka ya DRT na UDA wanavyofanya biashara kwa mazoea. Kama kuendesha mabasi yaani kusimamia tumeshindwa unaota viwanda by 2020? Baada ya vita vya Uganda Mwalimu alitudanganya tufunge mikanda kwa miezi 18 lakini baada ya miaka 20 yaani 1999 tulikua bado tumefunga mikanda na Mwalimu alipotutoka October 1999 alituacha tumefunga mikanda! Hawa jamaa wa kijani huwa kila uchao wanawadanganya Watanzania / Watanganyika na misamiati kuanzia "uhuru na Kazi" siasa ni kilimo " Ruksa" mtaji wa "Masikini ni nguvu zake" Mkukuta" , Maisha bora kwa kila mtanzania " Ari mpya nguvu mpya" , Kilimo Kwanza" Hapa KaZi Tu" Dai risiti" "Tanzania ya Viwanda " na mingineyo mingi. Nakuhakikishia utakuwa umeshatutoka kabla Tanzania haijawa ya Viwnda. Hizo nguo hitavaa! Kila kukicha utazuka Msemo na Watanzania kwa Uzuzu wao wanaambiwa na kukubali Mara Elimu bure na kadhalika!
 
Hilo suala halitatokea kamwe. Ngoz nyeusi hatujiamin na pia tunapenda kuwatukuza ngoz nyeupe.
Hapa tz watu weng sana weny ujuz wa kila aina, serikali ikaamua kuwasupport tutafika mbali sana km china. Tunachungu nzima ya watu weny ujuzi lkn tunawaangalia tu halafu leo tunataka nchi ya viwanda mbona hainingii akilini kbsa
mfano. Mtu aliyetengeneza gari na helicopta akiendelezwa mbona hiv vitakuwa vingi sana hapa tz.
Mbali na hapo kuna watu wamebobea kweny masuala ya IT lkn tunataka rwanda ndio itusaidie. Ha ha ha ha
tz tunachungu nzima ya watu weny kutengeneza vitu mbali kias kwamba wakipewa support tz yetu itakuwa kila mtaa ina kiwanda lkn cha kushangaza tunategemea watu weupe waje wawekeze tz ktk sector ya viwanda ha ha ha ha ha ha. Inachekesha na pia inahuzunisha
muhindi anateknolojia gani huyu?!!! Tz tunajichanganya sana, ktk watu ambao huwa siwakubali mpaka keshokutwa ni wahindi, hawa hawana lolote zaid ya unyonyaji tu. Kule kwao maskini km nn halaf waje kuwekeza hapa. Walio fanya kaz au wanaofanya kaz kweny mashirika ya wahind watanielewa ni bora hata uwe boda boda utapata hela na sio hawa washenzy.
Mtoa mada naungana na ww, kwa tz yangu hiyo kitu haitatokea hata ikifika mwaka 2050 na kuendelea.
Angalia nchi zote zenye viwanda km marekan, china n.k walithamini vya nyumban na kuviendeleza.
Mtoa uzi hata mm nitavaa nguo za ccm na kuchukua kadi kbsa ikiwa nchi viwanda 2020.
 
Back
Top Bottom