Kwa mujibu wa tovuti ya serikali Sera ya Ulinzi ya Taifa ni seti ndogo ya Sera ya Serikali inayohusika na kukabili vitisho vya kijeshi na maendeleo, utunzaji, matayarisho na ajira ya wanajeshi. Tovuti hiyo inaendelea kusema kuwa Sera ya Ulinzi inahitaji kuwa na majeshi yenye kiwango cha juu cha tija ya jeshi, utayari wa kutosha, na kuwa na madhumuni yanayoeleweka kwa kuzuia migogoro, udhibiti wa migogoro, na shughuli za mapambano.
Aidha tovuti hiyo inaendelea kusema kuwa Lengo la jumla la ulinzi wa taifa linazingatia kulinda maslahi na maadili makuu ya Taifa, yanayojumuisha kulinda uhuru wa taifa, dola na uadilifu wa taifa, kulinda Muungano, kudumisha amani na utulivu, kuhimiza demokrasia na utawala bora, kuhimiza ustawi wa kiuchumi na maendeleo ya uchumi na jamii, kudumisha amani na utengamano wa kanda, kudumisha haki katika jamii na kulinda maliasili.
Ukisoma tafsiri ya Kiingereza iliyowekwa kwenye tofuti hiyo inatafsiri Sera ya Ulinzi kama National Defence Policy na kui-define kama the subset of government policy concerned with countering military threats and with development, maintenance, preparation and employment of the armed forces. Hivyo basi inaonekana kwama sera inayozungumzwa kwenye tovuti hiyo ya taifa imejikita zaidi kwenye masuala ya kujilinda dhidi ya maadui kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wa kujilinda na maadui wa nje wengi wanaweza kusema wazi kuwa Tanzania inafahamika kwa kuwa na jeshi zuri la kulinda mipaka yake. Hata hivyo, linapokuja suala la ulinzi na usalama wa raia ndani ya nchi kuna walakini. Whether or not hii imesabishwa na ukosefu wa sera ya ulinzi na usalama wa raia sijui, lakini ukosefu wa sera kama hiyo unaweza kusababisha kusiwe na basis ya actions zinazochukuliwa na serikali katika kulinda raia wake.
Wizara ya Mambo ya Ndani, ambayo kwa kawaida ndiyo imepewa jukumu la ulinzi na usalama wa raia, ina idara inayoitwa Policy and Planning Division. Moja ya objectives za idara hii ni pamoja na "to provide expertise and services in policy formulation, implementation, monitoring and evaluation. Idara hii ambayo inaongozwa na Mkurugenzi inamegawanywa katika vitengo mbalimbali, mojawapo kikiwa kitengo cha Policy Section.
Kazi za Policy Section, ambacho kinaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi, ni kama zifuatazo:
- Coordinate formulation, review, implementation and monitoring of Ministrys policies; and ensure they are consistent with national policies, frameworks and strategies;
- Review and advise on policy papers prepared by other ministries;
- Carry out research and impact studies of ministerial policies and provide a basis for making informed decisions on the future direction of the Ministry; and
- Compile implementation reports on Ruling Party Manifesto and Parliamentary Committee reports.
So far kwenye tovuti ya Wizara ya mambo ya Ndani, sehemu ya Policies kuna sera moja tuu imewekwa pale ambayo ni National Refugee Policy. Labda sera nyingine hazijawekwa kwenye soft copy. Kwa upande mwingine, inawezekana labda Tanzania ilikuwa haina au bado haina sera ya ulinzi na usalama unayozungumzia kwa sababu mwaka jana mwishoni, Chama cha Sekta ya Ulinzi Binafsi nchini kiliiomba serikali, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, kuendelea kusimamia na kukamilisha mchakato wa Sera ya Taifa ya Ulinzi na Usalama wa Raia. Bado sijui kama mchakato huo umekamilika na kama bado haujakamilika utakamilika lini.