Sera ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Inapatikana Wapi?

Sera ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Inapatikana Wapi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,250
Reaction score
44,578
Hali ya Usalama na Ulinzi ya Nchi yetu iko matatani. Matukio ya uhalifu wa kila namna yanaonekana kuwa ya kuthubutu zaidi na vyombo ambavyo vimeundwa kusimamia ulinzi na usalama (law enforcement organs) vinaonekana kuwa nyuma ya wahalifu. Kuanzia kwenye ujangili, ujambazi, uvamizi na utekaji na uhalifu wa kalamu na ufisadi mwingine wahalifu wanaonekana kuwa juu.

Mabadiliko mengi ya sekta mbalimbali nchini yametanguliwa na kupitiwa kwa sera (policy review) ya eneo husika. Hii imekuwa kweli kwenye masuala ya elimu (MMEM zote) na imekuwa kweli kwenye sekta ya afya. Pia imekuwa kweli kwa kiasi kikubwa kwenye sera ya nishati na madini ambayo ilikuwa haijafanyiwa mabadiliko kwa karibu miaka ishirini - tangu Kikwete awe Waziri wa Nishati enzi hizo hadi hivi karibuni. Na hili ni kweli pia kwenye suala la utafiti wa mafuta na gesi ambapo miezi ya karibuni kumekuwa na jaribio la kukamilisha sera mpya ya sekta hiyo nyeti.

Sera ndio msingi wa sheria na ndio msingi wa mfumo wa utendaji kazi na hata naweza kusema ndio msingi wa miundo mbinu ya kiutendaji ya sekta mbalimbali. Kwa sababu, sera ni kama ramani ambayo ina maelezo yote kwa kirefu ya kitu gani taifa linataka katika sekta fulani. Sera huandaliwa na vyama vya siasa na katika Tanzania sera zinazotkelezwa ni zile za Chama cha Mapinduzi - ndicho chama ambacho sera yake ya ulinzi na usalama ambayo siamini kama imepitiwa kwa miongo miwili sasa.

Tunaweza kuwa tunashtushwa na matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani na hata utendaji duni wa baadhi ya vyombo vya usalama lakini ukweli ni kuwa haya yote ni matokeo ya udhaifu wa sera yenyewe. Vyombo vyetu vya usalama viko karne ya ishirini na moja lakini sera yake ilitungwa wakati wa Vita Baridi au Mapema wakati wa mageuzi ya kisiasa (sina uhakika wa hili).

Ni kwa sababu hiyo naomba kutoka kwa mtu yeyote ambaye anayo sera hii katika maandishi mahali popote atutupie hapa ili tuweze kuipitia na kuona kama inaenda na wakati au kama inahitaji mapitio au mabadiliko makubwa. Ikumbukwe sijauliza sera za chama kingine chochote kwani kwa hivi sasa sera zinazotekelezwa ni za CCM. Kwa vyama vingine ni matumaini yetu na wao watakuwa na sera ya eneo hili mapema kabla ya uchaguzi wa serikali za Mitaa mwakani ili kuwapa wananchi nafasi ya kujua mwelekeo wa nini wanataka kufanya kwa taifa kwenye eneo hilo.

Natoa ombi.
 
WanaJamii kuna nyeti ambayo inakuja na inahusiana na mambo ya usalama wa nchi...nadhani media za Tanzania zitaipick tuu quite soon au mnao scan mambo ya nje mtakuwa mshakiona hicho chuma kinachokuja na moja kwa moja hawa watu wa National Security Council ya Tanzania itabidi watoe tamko sasa kabla hatujaenda mbali kuna mtu anajua:

1. Je limeundwa lini?

2. na wajumbe wake wanapatikana vipi?

3. Je Zanzibar wamo au hawamo?

4. Je inabidi wawe na qualifications zipi?

5. wanakutana mara ngapi?

6. mwenyekiti wao ni nani?

7. Katibu wao ni nani?

8. Wanaripoti kwa nani?

9. je washatoa maamuzi yepi zazito yanayohusu nchi hii tangu liundwe?

10. je ripoti zao (gongo la mboto, pirates, meli kuzama zanzibar etc) ziko wapi?

11. je website yao ni ipi?
 
Mzee Mwanakijiji,
Pamoja na kwamba nakubaliana na umuhimu wa sera ya usalama wa taifa lakini bado nchi hii ina matatizo ambayo hata kama tutakuwa na sera mzuri bado matatizo ya usalama yataendelea! Kwanza kabisa, napingana na wewe unaposema: " Vyombo vyetu vya usalama viko karne ya ishirini na moja lakini sera yake ilitungwa..." Vyombo vyetu vya usalama bado vipo karne ya ishirini na wala sio ya ishirini na moja! Wanausalama na makachero wengi bado wapo karne ya 20 na wala sio karne ya 21! Na hivi ndivyo Watanzania wengi tulivyo! Nenda pale CRDB Azikiwe Branch(te largest branch in the country) kisha muulize ofisa wa benki juu ya jambo dogo sana, say how you can link your account with a Paypal! Utashangaa, anakuuliza ni nini hiyo....ofisa wa benki toka benki kubwa kabisa iliyo kwenye jiji kubwa kabisa! Hawa nao bado wapo karne ya 20!

Hivyo basi, tatizo kubwa ninaloona mimi ni wahusika kuwa lagged behind! Makachero wetu they don't think behind the box! Hata kama tunakuwa na sera mzuri namna gani, uhalifu utakuwepo tu; kinachokera ni pale inaposhindikana kupatikana kwa wahalifu hao! Tuchukulie mauaji ya Dr. Mvungi....huyu ni wakili wa muda mrefu ambae si ajabu ameshawahi kuathiri maslahi ya watu mbalimbali ambao pia ni wazito kwa namna moja au nyingine!! Lakini pamoja na yote hayo, Makachero wetu wanaweza ku-conclude kirahisi rahisi tu kwamba lilikuwa ni tukio la ujambazi simply because kuna vitu viliibiwa! Hawawezi kuweka option nyingine kwamba inaweza pia kuwa ni cover up(undercover) incident/operation! Hili ni tatizo!

So, kama ipo hiyo sera nami pia ningependa niione lakini bado tuna safari ndefu hata kama tunafanya policy review!
 
Last edited by a moderator:
Kamanda Kova anaifahamu zaidi ngaja aje kutujuza na kutuelimisha. Karibu kamanda mchapa kazi kwakutumia tv.
 
Mzee Mwanakijiji Eti "sera" ya ulinzi! Wewe Mzee una matatizo ya kufikiri. Hivi unajuwa maana ya sera?
 
Last edited by a moderator:
The main thing that makes me hate ccm the most,siyo kwasababu ya lack of good policy,bali governance na utekelezaji wa policies hizo.Sasa hivyo vyama vingine vitueleze,hatuwezi kujuwa hadi tubadilishe utawala halafu tuwasimamie hao wengine kwenye utekelezaji wa sera.
 
Ukitaka kuwachanganya CCM we waulize SERA - Mimi nina wasiwasi kama tumeshawahi kuwa na sera hizi katika taifa letu!!
1. Sera ya Kilimo
2. Sera ya Elimu
3. Sera ya Ulinzi na Usalama wa taifa - anayoitaka kuiona MM
4. Sera ya Afya
5. Sera ya Raslimali asilia za taifa letu - eg Madini, Misitu nk

Hii ya Elimu ndiyo ilileta mshike-mshike pale bungeni mwisho wa yote - tumemwachia mola kama kawaida yetu.
 
Mods: naomba mnisaidie jambo moja.... hivi hakuna uwezekano wa kuzuia au kufuta kabisa contributions za kipuuzi kama zilizotolewa na faiza na simiyuyetu hapo juu kwenye jambo la muhimu na nyeti kama hili la mzee mwanakijiji..... maana wakati mwingine huwa nahisi hata kulia ninapoona mtu kaanzisha mjadala muhimu kwa taifa letu halafu watu wengine wanaanza kuleta masikhara yao..... kama hilo litafanyiwa kazi itatusaidia sana kupata contributions za maana....... kwenye mambo yao ya vyama mnaweza kuwaachia wanyukane wanavyoweza maana wengine hatuna vyama kwa hiyo inakuwa inatuumiza tu kuona vitu muhimu vinachangiwa kwa ujinga ujinga...
 
Eti "sera" ya ulinzi! Wewe Mzee una matatizo ya kufikiri. Hivi unajuwa maana ya sera?

Ungeonyesha kwamba hajuhi kwa kueleza sera ni nini? Upo kwenye MP nini mbona unaropoka tu kama Maghufuli?
 
Mzee Mwanakijiji,
Pamoja na kwamba nakubaliana na umuhimu wa sera ya usalama wa taifa lakini bado nchi hii ina matatizo ambayo hata kama tutakuwa na sera mzuri bado matatizo ya usalama yataendelea! Kwanza kabisa, napingana na wewe unaposema: " Vyombo vyetu vya usalama viko karne ya ishirini na moja lakini sera yake ilitungwa..." Vyombo vyetu vya usalama bado vipo karne ya ishirini na wala sio ya ishirini na moja!

Hapo kwa kweli hata mimi umenitisha kwa kweli na kunikatisha tamaa.. na hapa ndio suala la sera linapokuja. Kwa sababu sera ndiyo ambayo ingetoa uongozi wa kuwatoa hawa jamaa kutoka karne ya 19 (had to make it look worse). Tatizo la vyombo vya serikali haviendi vyenyewe na mara nyingi ndio tabia ya karibu taasisi zote za kimifumo. Lengo la kuulizia hili la sera ni ili tuone kwa jinsi gani tunaweza kuvileta vyombo hivi katika ulimwengu wa kisasa ambao uhalifu ni wa kisasa kama vile utatuzi wake ulivyo wa kisasa. Hatuwezi kutegemea initiative ya mtu mmoja mmoja.

Chukulia mfano wa hilo la kulink paypal na benki; well kama sera na mfumo haujaweka wazi umuhimu na ulazima wa kwenda na teknolojia ya kisasa ni wazi kuwa watu bado watakuwa wanatumia kompyuta bila kutumia teknolojia ya kimtandao.
 
Mzee,nasikia hii sera anayo mkuu wa mkoa anaitwa mwambungu jaribu kuwasiliana naye mkuu.

Mkuu wa mkoa wapi? ina maana hakuna mwana CCM hata mmoja ambaye anayo au hata kwenye tovuti ya CCM ambapo tumeweza kupata nyaraka nyingine nyingi tu?
 
Naona "simple minded virus" wamevamia hapo juu ili kuvuruga mjadala..IGNORE THEM,they've been paid to do it.
 
Back
Top Bottom