Sera ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Rais Magufuli

Sera ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Rais Magufuli

Kwa upande mwingine, kama mtu anaweza kusema hadharani Libya ilikuwa inaongozwa na Sadam Hussein halafu katika kujirekebisha anakosea tena na kusema alikuwa rais wa Quwait!!! mtu huyu anatakiwa kuandaliwa kwa muda mrefu zaidi kabla hajaanza kuhudhuria mikutano ya aina hii. Asije akamwabia Netanyahu "ukirudi wasalimie sana wapiga kura wako kule Palestina" (Just kidding)
Unamkumbuka yule kiongozi wenu aliyewahi kwenda Thailand kutununulia mvua
 
Ina wezekana hapati viza, au anaogopa kupanda ndege!!!
 
Mleta Uzi unakosa kauelewa fulani juu ya uhusiano wa kimataifa, Sera ya nje ama Foreign Policy haijawahi kuwa sera ya rais n sera ya Taifa na sera yetu ya mambo ya nje ya TZ kwasasa ni ECONOMIC DIPLOMACY, sasa hyo yako sijuwi umeiibuwa wapi thinker wetu??
You mean ECONOMIC DIPLOMACY ya kutembea na bakuli na kuombaomba.
 
Economic diplomacy ndio Sera ya nchi yetu kwa sasa
 
Unamkumbuka yule kiongozi wenu aliyewahi kwenda Thailand kutununulia mvua

Inafananaje na post yako hii? Au unaandaka kuhusu diplomasia na hujui hata mambo ya diplomasia ni yepi?
 
Tulisema mwache kumlinganisha huyu nanilii na Nyerere aisee, Nyerere alikuwa na influence kwenye siasa za dunia na alizijua A to Z, sasa huyu #Uchwara asiyejua Sadam alikuwa Rais wa nchi gani eti ndo aziweze siasa za nje????
 
Sasa wee ngumbaru,,, hujui kuwa anayofanya Magufuli ndo yanakufanya ukalipe VAT uchwara?

Endelea kusifia!!

IPi ni VAT uchwara?
Mfano nchi karibu zote za EU wanalipia TV license, kitendo cha cha kuwa na TV tu ama unaangalia ama umeizima TV license unalipia. Sasa sisi hatuwezi tembea nyumba kwa nyumba kulipisha TV. Phone license ndo inafaa zaidi. Sasa VAT uchwara ni ipi? Nenda nchi za europe zote harafu uone tofauti ya VAT ya Tz ambayo ni uchwara na za europe.
 
Hivi sera ya mambo ya nje ya Magufuli ni ipi?
Sera yak ya nje ni kukimbia safari zote z nje....kumuomba kilaza PM na Waziri Mahiga waende maana hajui lolote kuhusu diplomacy...either ya uchumi au ya siasa....hajui lolote! Tumsamehe tu maana miaka 10 tulisema kuna auto pilot sijui miaka 10 hii tuna nini!! Msomi , PhD hawezi ha kujieleza mistari 2 tu! Kazi tunayo!!!
 
IPi ni VAT uchwara?
Mfano nchi karibu zote za EU wanalipia TV license, kitendo cha cha kuwa na TV tu ama unaangalia ama umeizima TV license unalipia. Sasa sisi hatuwezi tembea nyumba kwa nyumba kulipisha TV. Phone license ndo inafaa zaidi. Sasa VAT uchwara ni ipi? Nenda nchi za europe zote harafu uone tofauti ya VAT ya Tz ambayo ni uchwara na za europe.
Akili mbovu kweli! Kwani mimi silipii king'amuzi? Nenda kalale!!
 
Kwa tegemezi lenu hilo ndio mmeshazoea kuwa na viongozi wanaozunguka dunia nzima kuomba misaada.
Lazima mtarudi vijijini kulima hakuna mchezo na Hapa Kazi Tu.
Mbona zinazotolewa sijaskia zikikataliwamaana tunajiweza?naskia tu tumepokea tumepokea si mlemle hahahahaha acha u le mbebezzzzzzzz
 
Ni sahihi, lakini siasa za sasa siyo kama za wakati ule, hivyo ni lazima uangalie kwa makini na kwa mapana faida ya Raisi kuwepo au kutokuwepo kwenye mikusanyiko ya kimataifa kama hiyo. Kimsingi, kwenye mikosanyiko yenye kujenga mahusiano ya kimataifa yenye hadhi ya taasisi ya URAISI si vyema sana yeye akijiweka nyuma au mbali. Nivizuri aende, ajifunze na kushiriki.
Bado tujifunza kitema yai unataka tukaaibike shekhe?!
 
Sasa wee ngumbaru,,, hujui kuwa anayofanya Magufuli ndo yanakufanya ukalipe VAT uchwara?

Endelea kusifia!!
Tatizo la nyumbu ni peer pressure hawezi kukuelewa mkuu. Njaa mbaya sana
 
Ebu tufikiri kidogo, kati ya Israel a close allies of westerners na TZ nani anaweza kumuhitaji mwezake zaidi??????

Duu hizi fikra za ajabu kweli yaani kutohudhuria vikao ni ni sera ya mambo ya nje ya nchi yetu au hujui maana ya sera? We unajua kwa nini hajaenda?

Hivi sera ya mambo ya nje ya Magufuli ni ipi?
Tuna gesi, mafuta na rasilimia nyingi sana lazima wazungu watufuate. Kama hawaji basi wakae huko kwao na sisi tukae kwetu.
 
Kwa upande mwingine, kama mtu anaweza kusema hadharani Libya ilikuwa inaongozwa na Sadam Hussein halafu katika kujirekebisha anakosea tena na kusema alikuwa rais wa Quwait!!! mtu huyu anatakiwa kuandaliwa kwa muda mrefu zaidi kabla hajaanza kuhudhuria mikutano ya aina hii. Asije akamwabia Netanyahu "ukirudi wasalimie sana wapiga kura wako kule Palestina" (Just kidding)
ki ki ki ki ki mbavu sina.
 
Tuna gesi, mafuta na rasilimia nyingi sana lazima wazungu watufuate. Kama hawaji basi wakae huko kwao na sisi tukae kwetu.
Umeshaona kiongozi yeyote anaenda kutembelea Eritrea ama umeshaona kiongozi wa Eritrea akitembelea nchi yeyote, nenda ukaone maendeleo ya nchi hiyo ndogo Afrika ilivyopiga hatua katika masuala ya huduma kwa jamii. Sio lazima kwa Rais wa nchi ya Tanzania apigie magoti wahisani ama wafadhili wakati Tanzania ni nchi Tajiri bali mfumo wa watawala waliopita haukuwa mzuri. Hapa Kazi Tu.
 
Itabidi siku moja nitoe darsa la sera watu wajue sera ni kitu gani. Sio kila uamuzi au utashi ni sera. Pengine hata ukimuuliza mtoa hoja tofauti ya Ilani ya CCM na Sera za CCM hajui.
 
Back
Top Bottom