Black Empowement is long due in Tanzania. Sera za uzawa sio ubaguzi bali kujenga mfumo kwa rasilimali zote zimilikiwe na wazawa halafu wawekezaji wote lazima waingie ubia na wazawa katika kila sekta ili baadhi ya net profit ya hii miradi ya uwekezaji ibakie nyumbani.
Niko hapa India, Ardhi yote ni mali ya koo fulani fulani. Kama umezaliwa kwenye landless family, kwa hakika utakufa landless. Hakuna namna yoyote ya mwekezaji toka ndani ama nje anayeweza kuwekeza India bila kushirikisha wazawa. Tatizo la India wana Caste System ambao ni ubaguzi wa wazi wazi yaani kama umezaliwa ukoo wa hali ya chini wewe ni mtu duni maisha yako yote, na kama umezaliwa familia bora wewe ni bora. Hawa wahindi walioletwa Tanzania, walitoka low caste na walikuja kama vibarua wakati wa ujenzi wa reli ya kati. Ndipo wakapata fedha na kukuta Bongo ardhi bure, ndio wakajitwalia na kujenga maghorofa karibu miji yote mikuu na hatimaye kulowea na kupata uzao wao hapa. Tangu baada ya kutaifishwa kwa majengo ya, wameishia kupanga nyumba za Shirika la Nyumba, hawaweki tena witegauchumi vya infrastrucure, kazi yao ni kuvuna pesa na kuzihamishia India kuangalia namna ya kuinua hali za maisha ya low caste za jamaa zao walioko huku ambao kutokana na mfumo huo wa caste, hao jamaa zao huku ni masikini kweli kweli, hata wale ombaomba wa Dar ni afadhali!.
Umoja wa Falme za Kiarabu pia umeweka sheria kali za uwekezaji kwanza ardhi yote ni ya ukoo wa Kifalme, wananchi wanagaiwa bure ila haiuzwi, pili kila mwekezaji lazima aingie ubia na wazawa. Matokeo yake waarabu ni matajiri, kazi yao kula na kulala huku wakilipwa gawio la uwekezaji hivyo kubaki wakifanya ziara za utalii mwaka mzima na kuwinda wanyama
Baada ya burudani za kuua binadamu kupigwa marufuku.
Tanzania tunashindwa nini kumillikisha maeneo yenye madini kwa wazawa waliolizunguka. Wakina Barrick wakija, lazima waingie ubia na wamiliki ili hiyo dhahabu iwafaidie wote.
Maeneo yote yenye vivutio vya utalii kumilikiwa na waliopo. Ingawa lengo la Nyerere kukataamfumo huu lilikuwa zuri la kuzuia matabaka ya wenye nacho na wasionacho, lengo hili sasa limepitwa na wakati kwa sababu wenye nacho ni wageni na wasionacho ni wazawa, afadhali wazawa wa maeneo yenye nacho wamilikishwe na serikali iwatoze kodi hao wenyenacho na kuwagawia wasionacho.
Kariakoo wengi waliomiliki zile nyumba ni wanawake wa Kizaramo na Kimanyema baada ya waume zao waliokuwa makuli bandarini kufariki. Leo nyumba zote wameuza, wamehamia Tabata, wamiliki wapya ni waarabu. Kama kungekuwa na sera ya uzawa, hawa wazawa wangeendelea kumiliki ardhi na mwekezaji angejenga kitega uchumi na kumiliki kwa ubia na wawekezaji.
Kilio cha kijana Nape kuhusu mkataba wa Jengo la Umoja wa Vijana-CCM, kimedondokea 'sikio la kufa' maana ule ni mkataba wa Maisha!.Kwa lugha rahili hilo jengo jipya linalojengwa litakuwa ni mali ya mwekezaji ila Umoja wa Vijana watakaa bure na tujisenti kidogo twa kununulia soda za wageni!.
Kwa waliiona movie ya 'Trading Places' watakubaliana na mimi kuwa wazawa weusi wana uwezo wa biashara kama wakiwezeshwa. Kuwezeshwa kwenyewe ni pamoja na kujengewe uwezo, capacity building ya kuja kuendesha hizi biashara kubwa kubwa ama- miradi mingi ya uwekezaji.
Ukiisoma vizuri ile sera ya Ubinafsishaji, utaona lengo lilikuwa tuuze yale mashirika na fedha zitakazo patikana ziwekwe kwenye mfuko maalum ambao ungetumiwa kuwagawiya wazawa mtaji katika ununuzi wa hisa mbalimbali. Sijui kama hilo lilitimizwa hivyo kwa lugha nyingine, zoezi lote la ubifsishaji pamoja na umasikini wetu, ni kile kidogo tulichonacho ndio tumekigawa bure kwa wenyenacho ili litimie lile neno, 'mwenenacho anaongezewa, na asiyenacho ananyang'anywa hata kile kidogo alichonacho.
Japo hayo yote yameshafanyika, thank God, Tanzania bado hatujachelewa kwa sababu japo mbele hatusongi, ila tumesimama hapa hapa tulipo na wakati mwingine tunapiga hatua kwa kurudi nyuma tungali tumesimama. Ushauri ni utekelezaji wa msemo huu 'anayejidhania amesimama, na aangalie usianguke'. Njia pekee ya kuzuia tusianguke ni kuwawezesha wazawa weusi kukamata usukani wa uchumi wetu.