Sera ya elimu bure imedumaza ubora wa elimu yetu. Turudi kulipa ada

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,946
2,929
Sera hii ya elimu bure haitufai watanzania eidha hatujafikia hatua hiyo kutoa elimu bure au elimu haipewi kipaumbele.

Taaluma imekufa watoto wamrundikana madarasani Tena wamekaa chini, mwanzo wa mwaka 100000 ya dawati kwa Kila mzazi anayemwanzisha mtoto shule au forme one.

Ni vema turudi kwenye ada ili shule ziweze kupata vitendea kazi na kujenga miundombinu Wengine najua mtakuja na kekejeli lakini wapo watakao nielewa.
 
Nchi inatakiwa iendelee kutokea hapo.

Kama tatizo ni kujazana madarasani na vitendea kazi basi serikali ifanye namna ya kuboresha hivyo na sio tena kurudi nyuma. Sasa hivi serikali inatakiwa kufikiri namna ya kufanya hata elimu ya juu kuwa bure na sio mikopo mikubwa ambayo hailipiki kiurahisi Wenzetu mnawaza kwa kutumia nini? Sio kawaida hii.

Kumbuka wanaosoma shule za serikali kwa Sasa hivi wengi wao masikini Sana, wenye kipato kidogo huwa wanawapeleka Watoto wao shule za English medium ambazo Sasa hivi zimejaa kila Kona.

ACHENI ubinafsi, huku tulipo wenzenu suala la elimu bure walilipita miaka karibu 50 nyuma
 
Unaonekana kuwa na point,, lakini vp kuhusu watoto wa masikini wasiokuwa na uwezo wa kulipa hio ada,, Je, wasisome ?
Ada ikiwa rafiki wataweza kulipa, hao unaowaita masikini, ukiishi nao utaona maisha wanayoishi. Anachoma mkaa, anauza hela anaenda nywea pombe.

Chukulia ada sh 30000 kwa mwaka, kuku wa kienyeji jike sh10000,huyo masikini atashindwaje?

Kipi kizuri tuifanye elimu yetu kuwa Bora liende au tuipie watoto hao wa masikini wapate elimu Bora iwainue kimaisha?
 
Unaonekana kuwa na point,, lakini vp kuhusu watoto wa masikini wasiokuwa na uwezo wa kulipa hio ada,, Je, wasisome ?
Hata wewe una pointi lakini pia tafakari, kwenye hizi shule za kata zilizo nyingi watoto ambao ndo wengi ni wamasikini hawasomi masomo ya Sayansi kisa walimu hawapo au waliopo whawatoshi na wamerundikana sana madarasani huku wakikaa chini.

Je, hii aina ya elimu ni kweli inamkomboa huyu mtoto wa masikini?
 
Nchi inatakiwa iendelee kutokea hapo.
Kama tatizo ni kujazana madarasani na vitendea kazi basi serikali ifanye namna ya kuboresha hivyo na sio tena kurudi nyuma..
Umeelewa post yangu au umechuku kakifungu tu?

Tuna miaka zaidi ya hamsini, unaípimaje elimu yetu, inapanda au inazidi kushuka na je umewahi kutafakari hili kwa kina?

Kusoma post ni Jambo moja na kuelewa no Jambo la pili
 
Naona makuwadi wa samia mpo mitandaoni mkijaribu kupindisha mambo.

Mmeshindwa kuendesha mashule kodi hazitoshi eeeh???
 
Nchi inatakiwa iendelee kutokea hapo.
Kama tatizo ni kujazana madarasani na vitendea kazi basi serikali ifanye namna ya kuboresha
Kwanini iwe serikali tu? Kwanini usiwe wewe unayesaidia shule zilizo jirani yako? Ulishawahi kununua hata box moja la chaki ukawapelekea walimu wakakataa kuchukua? Ustawi wa nchi unaanza na wewe hapo hapo mtaani kwako na kila mmoja akifanya hivyo Tanzania itakuwa mbali sana.
 
Ni wachache wanaoweza kuelewa hali halisi, watajitetea "wasio na uwezo wasisomeshe"

Acha elimu ibaki hivo hivo kama simu za kichina mwenye elf 10 atapata ya saizi yake mwenye laki 5 atapata ya saizi yake.... Hadi hapo tutakapokuja kushtuka usingizini.
 
Mbona zipo shule za kulipia. Hebu achana kutaka watoto wa wengine wasisome. Mpelekee hata mwanao uk USA Norway Finland Austria hujakatazwa ni hela yako tu ndugu
 
Neno masikini linatajwa sana humu, utadhani ni kitu kizuri mno!

Je, umaskini ni fahari?

Kama sivyo, mbona msihamasishane kuupiga vita badala ya kuusifia na kuufurahia ili kupata huruma!
Moja ya njia ya kuupiga vita umasikini ni Elimu mkuu...

Rejea notes za Civics form 3 ( ways to combat poverty )
 
Moja ya njia ya kuupiga vita umasikini ni Elimu mkuu...

Rejea notes za Civics form 3 ( ways to combat poverty)

Kama ni hivyo, hamasishaneni kusomesha... kama elimu bure haifai basi mlipie mtoto bila kisingizio cha umaskini wenu kana kwamba mnajivunia!
 
Back
Top Bottom