Separation VS new relationship is it right?

Huyo mdada anafikiri kuanza mahusino ni swala rahis na watoto wake wawili!! utachemsha, rudi kwa mumeo muishi kama zamani.
 
mleta mada tayari ana maamuzi yake...umeshaamua..we amua tu..watoto si unaweza kuwatunza!!!...endelea tu....amani si unayo moyoni!, uwezo si unao!?..si yupo uliyempenda na ndio maana unataka talaka haraka haraka....sasa kama unajiamini na unasema ndoa yako ni kama haipo na wewe unaishi kivyako na watoto..sasa unataka kujificha nini..si unajiamini we fanya tu hata mchana kweupe....fanya tu...mpaka wakati unavunja ndoa na unaenda kuishi kivyako hili ulikuwa unalijua...ndoa huwa haivunjwi na mtu yeyote wa nje zaidi ya wanandoa wenyewe....wewe umeshaamua fanya..viatu vyako vya plastic ulivyovaa usivivue ni vyako endelea navyo...
 
Dada piga moyo konde urudiane na mumeo, hali ya street ni mbaya sana. Watakuja na mbwembwe nyingi za kukupenda na kukuhudumia; mind you they will never be him. Ila ukitaka upate experience na exposure kwenye stress, welcome to the world!

Labda tujue sababu hasa ya kutaka kuachana.
Inaonekana yeye ndo anataka divorce lakini mume hataki.
Ina inawezekana mume hataki ndoa kuvunjika kwa sababu fulani au kum-trick mleta hoja.
Si bado ndoa haijavujwa kisheria?
 
.....Assume kama sababu ya kuvunjika kwa ndoa ni adultery halafu unaenda kuanzisha mahusiano mapya hata kabla divorce process haijamalizika.

......assume kwenye kesi hii mkorofi na mwanaume, tena maudhi kero na visa vyake vimemkinaisha kabisa huyu mama, halafu huyo mume HATAKI kuitoa talaka...

Huyo mke akae tu? MwanajamiiOne, huyu dada asiendelee na maisha kwakuwa tu huyo baba hayupo tayari kumuacha? ....mnh, haijaniingia bado akilini.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna k2 kipya utakachopata kwny huo uhusiano mpya. Km ni mkristu na umeshaolewa, hauruhusiwi kutengana na mmeo mpk kifo. Jitahidi myasuluhishe
 
Kuanzisha mahusiano sasa hivi ni 'risk' kama yakija gundulika utaonekana unataka divorse kwa ajili ya mchuchu mpya.

Umeshakaa miezi 8, basi vumilia hadi process ya kutengana iende mahakamani.
 
hizi sheria ni kabla ya kuanza kuchumbiwa upya ama ni kwa ajili ya kufunga ndoa upya?

Niliona mtu anataka kuunganisha sherehe ya ndoa mpya na arobaini ya marehemu mkewe.....:photo:

Sheria za kiserikali ni miezi 24. sheria za ki Islam ni miezi minne na siku kumi.
 
  • Thanks
Reactions: LD
......assume kwenye kesi hii mkorofi na mwanaume, tena maudhi kero na visa vyake vimemkinaisha kabisa huyu mama, halafu huyo mume HATAKI kuitoa talaka...

Huyo mke akae tu? MwanajamiiOne, huyu dada asiendelee na maisha kwakuwa tu huyo baba hayupo tayari kumuacha? ....mnh, haijaniingia bado akilini.

mkubwa Mbu....ukisoma hiyo thread ya huyu mleta mada ni kwamba tayari ana mnara wa kiburi...anaweza kuwatuna watoto wake na anasem wako vizuri na hana tatizo na hilo....
umri wake anasema yuko kwenye early 30...na ana watot wawili...kisa cha ndoa kuvunjika mimi na wewe hatukijui ila ukisoma hiyo thread vizuri utagundua tu mkorofi ni nani....Roho y siri huwa inalia sana na huwa haiachi kama mtu unafanya jambo lisilo jema..lazima ilie.....huyu dada ameshindwa kutumia utashi wake na ndio maana roho inalia ..we si unaona tu ...emeondoka na anaishi kivyake lakini anataka afnaye kwa kujificha!!!..hayupo nyumbani kwa mumewe lakini anataka kujificha...shetani siku zote akitaka kukuaabisha huwa anakuvuruga, anakutia mashaka, anakutia woga..kisha unaanza kujiachanganya na kuanza kusema mambo ya ajabu......hivi unafikiri hapo alipo hajafanya maamuzi ila anasubiri ushauri wa hapa jf?
 
Last edited by a moderator:
......hapa Soulmate naungana na King'asti kukushangaa aisee....lol

soulmate hapana nilichokuwa nimemwelewa mleta mada ni kuwa kuwa muwazi kwenye mahusiano mapya katika wakati huu. Mie bado nasisitiza ni muda mfupi sana ila naungana na wewe kwenye USIRI kwanza. Mbona tunawaona wengi tu wanaingia kwenye mahusiano ya siri ya nje kutokana na mateso na manyanyaso wanayoyapata ndani ya ndoa zao? lakini bado hata wakiachika/achana huvuta subra kwanza kabla ya kuonyesha wazi mahusiano yao mapya?

Nilikosea kumwelewa mtoa mada nikifikiri anataka kuonyesha wazi kuwa anaye mpenzi mpya tayari.
 
  • Thanks
Reactions: LD
......assume kwenye kesi hii mkorofi na mwanaume, tena maudhi kero na visa vyake vimemkinaisha kabisa huyu mama, halafu huyo mume HATAKI kuitoa talaka...

Huyo mke akae tu? MwanajamiiOne, huyu dada asiendelee na maisha kwakuwa tu huyo baba hayupo tayari kumuacha? ....mnh, haijaniingia bado akilini.

That will be the reason for divorce: unreasonable behavior. Hapo hapo hakuna ndoa isiyokuwa na ukorofi (depending how you define it), maudhi, kero, visa, n.k. Ndoa maana ingekuwa vizuri kujua sababu hasa ya mleta mada kutaka kuvunja ndoa. Pia na sababu iliyomfanya afunge ndoa na huyo mwanaume. People get married and divorce for different reasons.
 
  • Thanks
Reactions: LD
mleta mada tayari ana maamuzi yake...umeshaamua..we amua tu..watoto si unaweza kuwatunza!!!...endelea tu....amani si unayo moyoni!, uwezo si unao!?..si yupo uliyempenda na ndio maana unataka talaka haraka haraka....sasa kama unajiamini na unasema ndoa yako ni kama haipo na wewe unaishi kivyako na watoto..sasa unataka kujificha nini..si unajiamini we fanya tu hata mchana kweupe....fanya tu...mpaka wakati unavunja ndoa na unaenda kuishi kivyako hili ulikuwa unalijua...ndoa huwa haivunjwi na mtu yeyote wa nje zaidi ya wanandoa wenyewe....wewe umeshaamua fanya..viatu vyako vya plastic ulivyovaa usivivue ni vyako endelea navyo...

Huyu mdada anachotafuta atakiona.
 
  • Thanks
Reactions: LD
Mbu, wakati mwingine waweza pima faida na hasara ya kuachana na mme.

Kuachana kunaweza na faida ya mama kutafuta furaha yake anayoikosa ndani ya ndoa hiyo.

Hasara inaweza kuwa kuwalea watoto kama 'single parent' au kujiweka kwenye risk ya kuolewa na mtu mwingine ambaye huna uhakika atawapenda vipi watoto wake.

Mie nadhani furaha ya mama si kigezo pekee cha kuangalia hasa mnapokuwa na watoto angekuwa hana watoto ningemshauri kukimbia mara moja.

Na hao watoto wana umri gani? Ujue malezi si pesa tu.
 
Last edited by a moderator:
MwanajamiiOne hiyo inaweza kuwa ni sababu mojawapo ya kutaka kuvunja ndoa lakini sio kuwa ndo imevunjika. Kunahitajika divorce order ya mahakama ku-annul hiyo ndoa.

Aksante sana kaka yangu kwa kuniweka sawa. Na hapa nadhani ndipo nilipokuwa nachanganya mie. So hiyo miaka 2 ni kuwa inatoa go ahead ya kuvunja ndoa na si kwamba ndoa ishavunjika si ndio?

Naombeni msaada wa mwanasheria aisee!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Takes two mamii. Bible inasema 'isipokuwa kwa habari ya uzinzi', na mie nasema 'ukiongezea na physical and emotional abuse'.
unajitahidi kuvuta kamba mwenzio anakoroma, unaishia kuvuta mzigo na yeye, kha! Bora uikate uburure alone

Km ni mkristu na umeshaolewa, hauruhusiwi kutengana na mmeo mpk kifo. Jitahidi myasuluhishe
 
  • Thanks
Reactions: LD
Mbu, wakati mwingine waweza pima faida na hasara ya kuachana na mme.

Kuachana kunaweza na faida ya mama kutafuta furaha yake anayoikosa ndani ya ndoa hiyo.

Hasara inaweza kuwa kuwalea watoto kama 'single parent' au kujiweka kwenye risk ya kuolewa na mtu mwingine ambaye huna uhakika atawapenda vipi watoto wake.

Mie nadhani furaha ya mama si kigezo pekee cha kuangalia hasa mnapokuwa na watoto angekuwa hana watoto ningemshauri kukimbia mara moja.

Na hao watoto wana umri gani? Ujue malezi si pesa tu.

kongosho umenena sawa. Sometimes wengi huwa tunaangalia satisfaction zetu sie kama wenzi tunasahau interest za watoto wetu. Lakini sometimes hata hizo interest za watoto hakuna. Mahusiano ni vururuvururu yanachanganya mpaka watoto.........no matter umri wa mtoto ikiwa mazingira si condusive kwa malezi na makuzi ya mtoto sidhani inawezashaurika kuvumilia for the sake ya watoto aisee.

Tunaharibu psychologies za wenetu in the name ya ..."For their sake".
 
Hivi kwani ukiachana na mwenza ndo lazma uoe ama kuolewa tena jamani? tusijekujiskia kama nyani, ukiachia tawi hili shurti udake lingine! Kongosho, trust me watoto wanaokulia kwenye familia isiyo na furaha na upendo ni mara chache sana wanakuwa watu wema. Mtu anaempiga mkewe ama mumewe muulize atakuambia the same ilikuwa inafanyika kwao! Ushaona kitoto wageni wakifika kwao kinawakata majicho ama kinasengenya live "mama kasema wewe unapenda kukaa kwa watu, ni kweli?''

Kama ikishindikana tuite tu beleshi bana!
Mbu, wakati mwingine waweza pima faida na hasara ya kuachana na mme.

Kuachana kunaweza na faida ya mama kutafuta furaha yake anayoikosa ndani ya ndoa hiyo.

Hasara inaweza kuwa kuwalea watoto kama 'single parent' au kujiweka kwenye risk ya kuolewa na mtu mwingine ambaye huna uhakika atawapenda vipi watoto wake.

Mie nadhani furaha ya mama si kigezo pekee cha kuangalia hasa mnapokuwa na watoto angekuwa hana watoto ningemshauri kukimbia mara moja.

Na hao watoto wana umri gani? Ujue malezi si pesa tu.
 
Last edited by a moderator:
Mbu, wakati mwingine waweza pima faida na hasara ya kuachana na mme.

Kuachana kunaweza na faida ya mama kutafuta furaha yake anayoikosa ndani ya ndoa hiyo.

Hasara inaweza kuwa kuwalea watoto kama 'single parent' au kujiweka kwenye risk ya kuolewa na mtu mwingine ambaye huna uhakika atawapenda vipi watoto wake.

Mie nadhani furaha ya mama si kigezo pekee cha kuangalia hasa mnapokuwa na watoto angekuwa hana watoto ningemshauri kukimbia mara moja.

Na hao watoto wana umri gani? Ujue malezi si pesa tu.

Kongosho heri umeghusia hilo. Linapokuja suala la divorce watoto huwa hawafikiriwi kabisa. Kwa mfano kwa mleta mada amesema "Tuna watoto 2 naishi nao na kuwatunza kwa kila kitu they are fine and I dont have problem with that." Yupo confident hapo kuwa "they are fine" na hana "problem with that". It may sound OK lakini ame-take into account the likely impact of the intended new relationship kwa hao watoto? Halafu anaposema "new relationship" ana maana gani?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: LD
King'asti na MwanajamiiOne.

Ndio maana nikasema lazima kipima faida na hasara za kuachana vs uleaji wa watoto.

Kuna wakati kuachana wanandoa inakuwa kwa faida ya watoto pia. Mfano baba mbakaji wa watoto wake mweyewe.

Lakini si kila divorse ina faida kwa watoto sababu unaweza kuta wakati mwingine ugomvi umejikita katika kuta nne za chumba chao. Mfano, niliwahi ona mke kamkimbia mme sababu alikuwa ananusa pichu yake kila akitoka kazini for more that 15 years. Lakini alikuwa baba mzuri kwa watoto na mwishowe walidivorse.

Sababu za kuachana Vs faida kwa watoto majibu yake hayako straight forward sababu kila case inakuwa unique.

Kuna wakati mwanamke anashauriwa kabisa kuachana lakini anashindwa na kubaki kwenye ndoa sababu hawezi kulea watoto peke yake kwa kutokuwa na kazi. Anabaki kwenye ndoa ambayo inamuumiza yeye na watoto pia.
 
Last edited by a moderator:
EMT, hapo wengi huwa hatukumbuki kabisa.

Tunadhani utayari wa akili zetu unalingana na utayari wa watoto kitu ambacho si kweli.

Kumletea mtotot baba mpya zaidi ya yule aliyemzoea na anayemjua unaweza dhani haimuathiri lakini inamuathiri sana. Tunakuja jikuta tumetengeneza kizazi ambacho kubadili wapenzi haoni kama ni shida halafu baadae tuanza kuwalaumu huyu mtoto 'mhuni', not fair.

Na bora hayo mahusiano mapya yadumu, lakini leo una juma kesho john, kesho kutwa bakari hapo ni tatizo kubwa.

Na kwa uzoefu, hakuna watu wenye wivu na mama zao kama watoto wa kiume bora wa kike kidogo.

Back
Top Bottom