SENSA inafaida gani kwa watu wa wilaya ya KONDOA? miaka 50 sasa hakuna High school, hakuna Hospitali, hakuna maji, hakuna Umeme,hakuna barabara n.k. Binafsi yangu sioni faida ya sensa, kama hata maji bado watu wanachota mtoni, highschool mpaka twende moshi, songea, mwanza nk. KAMA BUDGET YA TAIFA HILI inazingatia idadi ya watu mbona kila mwaka budget haikidhi mahitaji ya wananchi?? na bado sehemu kibao zimesahaulika. NINI FAIDA YA SENSA KTK WILAYA YA KONDO??/
Tuache ushabiki wa kisiasa...sio kwa sababu unashabikia upinzani au kwa sababu unachukia CCM ndio upinge kila kitu kinacholetwa na CCM. Kwenye masuala muhimu yanayohusu maslahi ya kitaifa ninaomba tuache ushabiki na chuki. Mimi nadhani ni sahihi kama mtu atakuja na hoja kuhusu namna sensa inavyofanywa na sio hoja ya kuipinga sensa pasipo sababu za msingi.
we upo kondoa gani? maana kuna kondoa ya ovada usandawe hadi kurio wao wanajijengea sekondari na kuchimba visima,na kujenga zahanati HALAFU kuna kondoa ya farkwa ,babayu , kondoa mjini na kule kwa kina nkamia juma wao kipaumbele chao ni kujenga madrasa! wewe upo kondoa ipi mkuu?
Hospitali ipo hapo pembeni ya ofisi za halmashauri na huko kwingine vijijini kuna vituo vya afya na zahanati labda useme habari ya uchache.............Umeme nao upo mjini, na vijiji vyote inakopita barabara ya kuelekea Kiteto. Barabara inajengwa toka babati mpaka dodoma tatizo ni kasi ya mkandarasi ama labda serikali haimlipi kwa wakati............Mengine ya maji na high school sina la kusema!SENSA inafaida gani kwa watu wa wilaya ya KONDOA? miaka 50 sasa hakuna High school, hakuna Hospitali, hakuna maji, hakuna Umeme,hakuna barabara n.k. Binafsi yangu sioni faida ya sensa, kama hata maji bado watu wanachota mtoni, highschool mpaka twende moshi, songea, mwanza nk. KAMA BUDGET YA TAIFA HILI inazingatia idadi ya watu mbona kila mwaka budget haikidhi mahitaji ya wananchi?? na bado sehemu kibao zimesahaulika. NINI FAIDA YA SENSA KTK WILAYA YA KONDO??/
Hospitali ipo hapo pembeni ya ofisi za halmashauri na huko kwingine vijijini kuna vituo vya afya na zahanati labda useme habari ya uchache.............Umeme nao upo mjini, na vijiji vyote inakopita barabara ya kuelekea Kiteto. Barabara inajengwa toka babati mpaka dodoma tatizo ni kasi ya mkandarasi ama labda serikali haimlipi kwa wakati............Mengine ya maji na high school sina la kusema!
Uchawi mwingi sana pale.......huwezi pata maendeleo wakati uchawi umeshamiri!