Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,422
- 4,730
Katika zoezi la uwekaji wa anuani za makazi, bila shaka kila mmoja wetu ameshuhudia baadhi ya kasoro zilizojitokeza.
Wengi wamelaumu wizara ya habari na mawasiliano kwa kuwa waziri wake alionekana kufuatilia kwa karibu zoezi hilo.
Lakini tuseme ukweli, watekelezaji wa mwisho (watendaji, wenyeviti wa mtaa/vijiji, na mawakala wa sensa ngazi za mtaa) ndio hasa walipaswa kulaumiwa.
Japo na wao pia wangeweza kujitetea.
Kazi ilikuwa ngumu, malipo kidogo. Iliitwa kazi ya KIZALENDO.
Sasa basi, wito wangu ni kwenye zoezi la kukusanya takwimu (sensa) hapa hapahitaji kabisa mzaha. Endapo taifa litashindwa kupata takwimu sahihi za watu wake katika kila kipengele kilichokusudiwa, ni vigumu sana kuweka mipango sahihi (Proper planning).
Zoezi la kupata takwimu sahihi linahitaji uaminifu na uzalendo wa kweli.
Ushauri: kama serikali itaona haina uwezo wa kuwalipa vizuri mawakala wa sensa, ni afadhali kusitisha zoezi hilo au kutafuta mbinu nyingine ya kupata takwimu hata kama itachukua muda mrefu. Mfano kuwatumia mabalozi na wenyeviti wa mtaa. Kuliko kushuhudia kile kilichofanyika kwenye zoezi la anuani za makazi.
Ukweli ni kwamba,( kwa mujibu wa baadhi ya mawakala) 'walipika' taarifa ili kujiongezea malipo kwani walipaswa kulipwa kuanzia kaya 20 kwa siku moja.
Na hii inaweza kuwa kweli kwasababu baadhi ya mawakala hawakutumia simu kujaza taarifa; na wala hawakuchukua taarifa zote. Waliandika taarifa chache kwenye daftari na kisha kuondoka kwa madai kwamba watazi 'upload' baadae kwenye mfumo!
Suala la Takwimu halihitaji mzaha!