Sensa 2012: Yanayojiri

Sensa 2012: Yanayojiri

Mimi tayari nimehesabiwa, lakini la kushangaza kwa sababu ya umbo langu nimehesabiwa kama watu wawili. Madai yao ni kwamba kama serikali inakadiria mipango chakula kwa ajili ya kulisha kila mtanzania, mimi nitahitaji double!!

Hahaaaha
 
Katika hali ya utulivu kabisa majira ya saa 2:36 leo [26/08/2012] asubuhi amekuja karani wa sensa na kujitambulisha kwangu na kueleza kilichomleta.

Bila kusita nimempa ushirikiano mzuri sana na kumwandalia chai ingawa aliktaa ila nimemwambia mchana aje kula chakula cha mchana, yaani yale maswali waliokuwa wanasema mengi kumbe ukianza kuhojiwa hata dakika 7 hazifiki, miongoni mwa maswali hayo ni Unaitwa nani, Nani aliyelala kuamkia usiku wa leo, umri wako na wengine, kuna ulemavu wowote kati yenu, kuna vifo vilivyotokea, kati yenu kuna waliojiunga na mfuko wa jamii ie nssf, pspf, unashinda maeneo gani, na wenzako wanashinda maeneo gani, unajishughusha na ufugaji, elimu yako na wenzako, lugha unazozifahamu, uraia wako, kuna mwanakaya ambaye anaishi nje, n.k
Yule karani ameniambia atarudi tena kwa ajiri vitambulisho, alikuwa hana sare ameniambia sare zimechelewa ila alikuwa na kitambulisho.

Vile vile nimemshuhudia jirani yangu wa imani ya pili naye akitoa ushirikiano huku akiangalia kama kuna watu wa imani yake kama wametumwa kumwangalia anatoa ushirikiano, nikamwambia asiwe na wasi wasi mimi naaangalia kama kuna mtu yeyote atakuja ambaye simfahamu nitamstua.
 
Mie tayari nimesha hesabiwa!Karani aliyekuja ni mstaarabu sana nahisi ni mmoja wa aliye jifunza vizuri shughuli za sensa!kwa taaluma yeye ni mwalimu !
 
Huku tumeambiwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wataanza saa tatu. Nimeambiwa wataanzia nyumba yangu, hapa nipo nawaandalia chai kabisa.

Mdogo wangu una mbwembwe zaidi ya maimamu wanaopinga sensa ....haaa haaa haaa haaa,...nakutakia jpili njema
 
Mi tayari nimehesabiwa,maswali 37 ya dodoso fupi,ni maswali ya kawaida sana tu la msingi ni kuonesha ushirikiano na uvumilivu ili kutoa taarifa sahihi.Kwa bahati nzuri kutokana na mazingira ya njini,maswali mengine yanajibika haraka,kama vile nyumba unayoishi,choo unachotumia,afya yako I.e macho,miguu,usafiri,kipato nk.Tulieni mhesabiwe,uzalendo kwanza.
 
Bahati mbaya hujasema upo maeneo gani. Tutashukuru kama itakuwa hivyo sehemu zote lakini kuna sehemu ambazo nina uhakika kabisa kuwa kama hao unaosema kuwa ni 'jamaa zetu wa Imani nyingine' watakuwa ni wengi, Sensa haitaenda kwa Amani kihiiivyo...!
 
Niece wangu ananiambia nimewa bore na BBC news hivo amebadilisha channel to cartoon network. Nasubiri makarani wa Sensa.
 
Kama sio binti anayekuja kunihesabu sihesabiwi walahi tena...mbona lile kabila kule singida (wanyaturu)wametaka nyama wakapewa ili wahesabiwe !!
 
Mi sihasebiwi!

SOMA HAPA CHINI .... wakati nakutafutia kifungu unachovunja..... The Mayor warned them that whoever would not cooperate will be going against the law and may face the consequences, including serving jail terms of up to six months or more.
 
Mdogo wangu una mbwembwe zaidi ya maimamu wanaopinga sensa ....haaa haaa haaa haaa,...nakutakia jpili njema
Nimetumiwa ujumbe kuwa watachelewa kidogo, okay nawaona hao wanakuja, karani na mwenyekiti wa mtaa.....hahahaah!
 
Nimesikia kwenye vyombo vya habari kwamba kuna tatizo la sare za makarani,pengine aliyepewa tender hana uwezo wa kusupply bidhaa.
 
Back
Top Bottom