Mkuu unasema ni newbie ila kwenye signature yako umetoa namba ya simu watu wakucontact kuhusu software development, kama unajua programming angalau mwaka moja hizo systems ilitakiwa uwe angalau na idea zinavyofanya kazi.
In simple terms kabisa, system zote hizo zinakua na server, Vodacom wanachofanya ni kuset tu SSID fulani mfano hiyo *150*33 ukibonyeza inaomba data kutoka kwenye server zao, wanachofanya ni kukutumia hizo data tu, sema in this case wanatumia normal GSM (2G) networks, transmission ya data ni sawa na internet ya kawaida tu.
Ukitaka kudeal na GSM ufanye practice kidogo, nunua GSM modem hata AliExpress zipo hadi $15, connect kwenye computer yako, jifunze language kama python, JavaScript(node.js) au C, utengeneze webserver, fikiria unataka kufanya nini then anza kutengeneza, unaweza anza na apps ndogo ndogo mfano a simple news reporting service ambayo inakutumia habari mpya kwa kutumia sms, mtu akitaka kuregister na service yako labda anatuma message yenye ujumbe fulani kwenda kwenye namba yako ambayo line yake ipo kwenye hiyo gsm modem, unaparse ile message na kumuweka kwenye database, then kila habari mpya ikitokea unaiforward kwa subscribers wote, unaweka na option pia ya ku~unsubscribe, ukipenda unazidi kuiongezea manjonjo ili ujifunze zaidi. Unaweza ona ngumu ila ungekua na mentor mfano ungeshangaa sana ilivyo process rahisi once ukizoea.
Sema unlike softwares running through the internet, anything to do with SSIDs itabidi upate ruhusa kutoka kwenye mtandao husika, so kama unataka namba labda *22*22 iwe assigned kwako itabidi uombe mtandao husika, watakupa details zote kama kuna API, unahitaji kufanya nini, data wanazokupa mfano mtu akituma request vitu kama phone number, au kama haihitajiki njia nyingine utakayotumia kufanya authentication, vitu kama hivyo.
Na kuhusu mobile money, hiki ni kitu kipo hata nje, tena nje its more convenient zaidi ya waafrika mnavyofikiria, so hapo Mark alikua anapasha tu macho, kaja anajipendekeza kidogo na kuwapa moyo mnazidi kumpenda ila ni njia ya kutafuta wateja na kupenetrate kuingia kwenye market zetu hizi za Africa, ndiyo M-Pesa and the likes zimerahisisha sana maisha lakini bado hazifikii systems za nje hata kidogo, unlike bongo hadi utafute agent akujazie pesa kama hutumii banks huku unatoka nje ya mlango wako kuna atm karibu unaenda unatuma pesa kwenye mobile phone, internet, au popote pale unapotaka, hatuhitaji kutumia GSM wakati fast internet is all over ambapo kuna GSM na ni affordable, banking ni rahisi sana hata nje ya nyumba huitaji kutoka kama kila kitu unakifanyia hewani, mshahara unaingia kwenye account tayari una notification kwenye simu, mtu anakudai anakupa account namba unaforward hapohapo ulipo, unaenda dukani almost maduka yote unalipa kwa kadi, au unagusisha hata saa yako au simu hela inatoka kwenye bank moja kwa moja, wanaotumia cash wachache sana. Yote haya Tanzania yanawezekana sana tu hata kwa current situation sema ma~bank yetu yanapenda kuona sura zetu zimepanga foleni kuweka pesa hata ATM hawataki kutuletea zinazoweka pesa kila kona, nilitoa proposal ya virtual accounts nikatupiliwa mbali sana ka vile kila.za, sina hamu ya kurudi tena.