Jamani wadau wa MMU,mwenzenu nasumbuliwa na mafua balaa,nimeshndwa hadi kuhudhuria pindi leo.niombeeni nipone haraka,pia anae jua dawa ya mafua anisaidie,maana yananinyima raha mwenzenu.
mkuu piga konyagi yatayeyuka yenyewe.....bora wewe,mwenzio nimebanwa na tumbo la kuhara.yaani kila nikiona mgonjwa mmoja tumbo linabana inabd nitafute toilet ya haraka otherwise ntachafua mazingira
C. MAFUA (FLU NA COMMON COLD). HAYA ni maradhi maarufu, ambayo huambukiza kwa urahisi kutoka kwa mgonjwa hadi kwa mtu mwingine. TIBA: Chukua asali robo lita, unga wa tangawizi vijiko viwili vikubwa, unga wa mdalasini kijiko kimoja kikubwa na unga wa habasoda vijiko viwili vikubwa. Changanya zote pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara tatu.