Seneta mmoja wa upinzani amejitangaza kuwa Kaimu Rais wa Bolivia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Siku chache baada ya Rais wa Bolivia, Evo Morales kujiuzulu naibu Spika wa Bunge la Seneti la nchi hiyo, Jeanine Anez amejitangaza kuwa kaimu Rais katika kikao cha Bunge ambacho kilikuwa na idadi ndogo ya wabunge.

Wabunge wa Bolivia walikuwa wameitwa kupitisha uamuzi wa Morales kujiuzulu na kumthibitisha Anez mwenye umri wa miaka 52 kuwa kaimu Rais wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la DW, Bunge hilo lilihudhuriwa na wabunge wengi wanaompinga Morales, hata hivyo katika taarifa yake kwa Bunge hilo, Anez amesema kuwa wanataka kuitisha uchaguzi mpya haraka iwezekanavyo.

Awali, akijitangaza kuwa Rais katika bunge hilo la Seneti, Anez amesema uamuzi huo ni hatua ya kujitolea ambayo amechukua kwa ajili ya nchi hiyo na kwamba ataitimiza kwa kuitisha uchaguzi haraka.

Mwanamke huyo ambaye ni Seneta kutoka eneo la Kaskazini Mashariki mwa Bolivia (Beni) amesema “ipo haja ya kuweka mazingira ya amani ya kijamii” katika nchi hiyo ambayo ilikuwa chini ya ombwe la uongozi wa Morales.

Juzi, umati wa watu waliojawa na furaha waliandamana katika mitaa ya jiji la La Paz nchini humo wakisherehekea kujiuzulu kwa Rais Morales ambaye amelitawala Taifa hilo kwa miaka 14.
 
Back
Top Bottom