Semina ya wake za watu...

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,413
Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono. Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho umemwambia mumeo nakupenda lini?. Majibu mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema Leo, wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha akawaambia, kila mtu achukue simu yake halafu amtumie mumewe text yenye maneno. NAKUPENDA MPENZI, kisha wabadilishane simu. Wakaambiwa kila moja asome majibu kwenye simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama ifuatavyo;


Simu 1- Samahani nani mwenzangu?


Simu 2- He Mama Joji unaumwa?


Simu 3- Nami pia daima


Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?


Simu 5- Sijakuelewa una maana gani


Simu 7- Umefanya nini tena? Leo sitakusamehe


Simu 8-Chukua taim yako


Simu 9-?!?


Simu 10- Acha kuzunguka unataka shilingi ngapi?


Simu 11 – Hivi naota?


Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii meseji ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu shenzi mkubwa


Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na mimi
 
Bofloooooooooooo happy valentines day
 
Last edited by a moderator:
Haya cjui leo watajibiwa nn wakiwambia happy Valentine!
 
Dah aisee ni kweli maisha mengi ya ndoa ni kutimiza wajibu tuu...ndoa nyingi hazina upendo mkuu.....
 
Bofloooooooooooooooooooooooo.

Naona umeuwa ya valentino.
 
Boflo samahani lakini wewe ni mtu kama wa tano unapost hii mada.please refee the JF database .
 
Last edited by a moderator:
Usaniii kwenye mapenzi na mahusiano. kila kitu fake, fake,fake.....
 
happy velentine boflo hii ndo hali halisi kwenye mahusiano mengi.
 
Ukiona mwanamke anajipendekeza sana tu, ujue kaharibu, hii ni kweli kabisa Bofloooo!
 
Dah! Hii story yako Boflo imenifurahisha sana. Thanks a lot.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…