Semina elekezi na ziara za chadema

Semina elekezi na ziara za chadema

Felixonfellix

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
1,672
Reaction score
184
Rafiki yangu kaniletea haya. Naomba kuwashirikisha.
CCM: Semina unakutana na watawala wenzako - wachache
Chadema:Ziara mikoani unakutana na umma
CCM: Semina unafundisha ujanja, ghiliba
Chadema:Ziara unaleta uamsho; unafumbua macho na masikio - akili
CCM: Semina unakumbusha udhibiti wa umma
Chadema: Ziara unaeneza ufahamu wa haki na jinsi ya kuipigania
CCM: Semina unaunda mikakati ya kuendelea kutawala - halali au haramu
Chadema:Ziara unatafuta kushirikiana na umma kuweka utawala wake
CCM: Semina unalisha wachache mamilioni ya shilingi
Chadema:Ziara unaelewa vema nchi yako, watu wake ma natatizo yao
CCM: Semina unabaki na mawazo yaleyale
Chadema:Ziara unapata mawazo mapya kutoka kwa wananchi
CCM: Semina unakutana na waliofeli kazi; ulioteua kwa "mapenzi"
Chadema:Ziara unasimika wenye ari kutumikia umma
CCM: Semina unatoa amri na kukemea wateule wako
Chadema:Ziara unapata mawazo mapya yasiyochakachuliwa
CCM: Semina unajenga umimi wa watawala
Chadema:Ziara unatafuta ukaribu na wananchi - shavu kwa shavu
CCM: Semina unalenga kutisha
Chadema:Ziara unalenga kuelewana, kushirikiana na muwafaka
CCM: Semina unakumbushana mliyosahau au mliyodharau
Chadema:Ziara unachanja mbuga, unafyeka, unalima na kupanda mbegu huru
CCM: Semina unaendeleza "Hewallah"
Chadema:Ziara unatafuta kilichoko nyoyoni mwa wengi; halisi na kweli
CCM: Semina unazalisha semina nyingine aghali mikoani bila tija yoyote
Chadema:Mkutano mmoja unainua maelfu na kuwakomboa kifikra
CCM: Semina unalenga kuimarisha utawala wa walioko madarakani
Chadema: Ziara unalenga kuasisi utawala wa umma uliosahauliwa
Bila kujali nani anatumia nini, nani hasa anafanya kazi inayostahli kugharimiwa na umma: Walioshindwa kwa miaka yote na sasa wanajifungia ili kuandaa mbinu za kujibakiza madarakani; au wenye mawazo mapya na wanaoshirikisha umma kuasisi utawala unaowajali?
Tufikiri sawasawa!
 
Back
Top Bottom