Selfika na JF: Snap it. Show it

Kuna jirani yetu walimwajiri mfanyakazi wa ndani, mke anarudi jioni sana,kazi ya mfanya kazi ni kumhudumia mtoto, katoto ka miaka mi 3 katoto ka kike, yule Dada wa kazi alikuwa akitaka kwenda kuzurura anakapa dawa za usingizi, mtoto analala kuanzia mchana mpaka usiku, Dada akitoka kazini yeye ni kuuliza 'mtoto amekula' that's all, mtoto amelishwa sana dawa za usingizi, dogo ana miaka 12 sasa, ni katoto karembo Sana, but now ni kama akili zimeruka, side affects za dawa...
Hata leo huwa nikienda nyumbani nikimwona yule dogo roho inaniuma Sana, lawama zote ziende kwa mama yake...
Fundisho kwa wazazi wote,
 
Boss umeongea vyema sana,nakumbuka kuna kesi ilikuja ya mtoto wa kiume kuingiliwa kinyume na maumbile baada tu ya kupelekwa boarding akiwa na umri wa miaka 7,sababu kubwa mke alimwambia mumewe anachoka sana na majukumu ya kazini hivyo ni vyema mtoto aende boarding. Mume aligoma kabisa,akatoa option ya mama kuacha kazi kusimamia miradi ya familia ili awe na muda mzuri wa kulea familia, mwanamke akagoma.
Anasema umenikuta na kazi yangu.
The rest ni story mbaya,maana dogo alikuwa hata akirudi likizo hachunguzwi wala kupewa upendo wa karibu,na bahatimbaya zaidi baba alikuwa anafanya kazi mkoani, kwahiyo kuonana ni nadra.
Imagine mtoto amegundulika na tatizo na mtu baki kabisa,tena alienda shuleni akamuona yupo abnormal,hachangamani na wenzie vizuri.
Mimi naamini ukengemfu mkubwa wa jamii unatokana na malezi mabovu tunayotoa leo,tunaamini pesa inaweza kuchukua nafasi ya mzazi pale awapo mbali. Na tusipo badilika mapema,tutegemee kizazi tunachokileta kitakuwa cha hovyo sanaa, Mungu atusaidie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…