Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Attachments

  • IMG_7095.jpeg
    IMG_7095.jpeg
    361.5 KB · Views: 1
Mimi nishaumia sana na siasa hizi za bongo, kuna kipindi nilijaribu kuzipotezea lakini nashindwa..!!
Pole sana maa 🫂
Niliumia sana kipindi Lissu kapigwa risasi na kipindi cha uchaguzi wa 2020 Magufuli alivyopora uchaguzi nchi nzima..
Huyu mwenda zake apumzike anapostahili
Kule Zanzibar walikufa watu wengi na wengine kupigwa vibaya mno.
Wale KMKM walikua wanavamia majumbani wanapiga risasi raia..!! (Kile kipindi aisee nilimlaani sana Magufuli na niliomba Mungu kama yupo atuondolee lile balaa) kama ulishuhudia kile kipindi utakubaliana na mimi.
Hili jambo mpaka leo wa zanzabar wamelishikilia na wanalo sana angalia tunapozungumzia mo 29 wao hua wanaweka maoni gani
Maumivu yamekuja kurudi tena baada ya tekateka ya wapinzani na kupotezwa na hakuna maelezo ya kueleweka wala kukemea..!! Kipindi cha Samuya
Pole yetu wote
Na OCT 29 mimi nilitoka kwa hasira kuandamana kukemea, yaliyonikuta sitakuja kusahau! (Ipo siku nitaandika kuhusu ile siku) 😥🥹
Fanya siku uandike please
Kwa Lissu ni muendelezo wa watawala waovu kukanyaga utawala wa sheria.
Na hiyo yote sababu tuna katiba mbovu inayompa mamlaka makubwa mtu mmoja..!!

Tungekua na katiba nzuri ambayo tume na majaji wote haiko chini ya rais, kusingekuwa na uvunjaji wa sheria kama huu.

Fikiria hao majaji wote boss wao mmoja, tume ya kwake. Hivi unategemea kuna haki itakayotendeka?

Tupambanie katiba mpya, huo ndio mzizi wa tiba wa haya yote..!!
Sheria inabakwa kweupe!
Hata wale ambao hatujasomea sheria tunaona jinsi Lissu alivyoonewa
Dunia nzima imeona


Lakini kwa sababu hawa watu wamedhamiria kufanya wanachotaka, hawaoni hata aibu ilimradi mambo yao yanaenda kama walivyopanga

Naunga mkono suala la Katiba mpya.

Jaji Mkuu anateuliwa na Rais
Hapo kuna nini kingine cha ziada zaidi ya kujiuliza kuhusu uhuru wa mahakama na uwezekano wa kupokea maelekezo?

Na hata hukumu ya juzi ni dhahiri yalikua maelekezo ukiangalia namna nduguru alivyokua anazunguka mbuyu kuja na ile hukumu

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi naye vivyo hivyo Anateuliwa na Rais

Hii Katiba mbovu inayompa mtu mmoja madaraka makubwa ya kuamua mambo ndiyo imetufikisha hapa tulipo

Nyerere alifanya mengi mazuri lakini pia alituachia laana na laana yenyewe ni hii Katiba

Ndiyo maana hata Lema aliposema kwamba Katiba mpya haitabadilisha kitu, nikajua basi hakuna kitu!

Kigumu zaidi ni kwamba kuna baadhi ya wapinzani au tuseme baadhi ya wana CHADEMA ambao wanazunguka mlango wa nyuma na kurudisha harakati nyuma siku hizi wanaitwa madalali

Inasikitisha sana lakini ngoja tuendelee, tutaona mwisho wake

Pole baby girl Lamomy 🧡
 
Back
Top Bottom