Oohh siyo mbaya lakini uzuri wa mwendokasi ni kama hivyo ulivyosema kwamba kwa route ndefu zinasaidia
Lakini inatakiwa waongeze magari maana zilizopo tu bado ni za kugombania
Sisi wengine huku tulipo hakuna mwendokasi na daladala si za kugombania, wala hakuna foleni za kutisha ni mara moja moja tu, kwahiyo hata siku mtu ukiamua kutumia daladala ni raha mustarehe hazina hekaheka
Cha ajabu ukienda pale kivukoni muda huu,utakuta nyomi la watu wamepanga foleni wanasubiri mwendokasi ya kukaa.
Na pale Kuna mwendokasi limeshajaa,hawataki kuliondoa eti wanasubiri watu wa kusimama hadi lijae lote na wakati posta ya zamani,halmashauri,kisutu,fire Kuna watu kibao watapanda.
Kwahiyo mnasimama kwenye foleni na magari mengine yamewekwa tu pembeni,ila wanasubiri wanataka watu wapande lililojaa tayari ,na watu hawataki lililojaa,wanasubiri lenye siti maana mbezi ni parefu.
Aliyewaroga viongozi na wasimamizi Tz alishakufa na vifaa vyake.