Selemani Semunyu kipindi dakika 45 ITV hautendi haki!

Hiv bado kuna magreat thinker toka jf wanafuatulia hicho kipindi na mijutani ya ccm jamani km mnakuwa mmekosa vya kuangalia muwe mnajipumzisha vitandani
 
Huyo mwendesha kipindi hana interview skills. Hajui kuuliza maswali magumu. Kazi yake ni kutabasamu na kumsaidia anayemhoji. Namwomba amwige Steven Sucker wa BBC.
 

Simple, huyu anatafuta ukuu wa wilaya! same like marini hassan marine, Ukuu wa wilaya mongers!!!
 
yule jamaa ninapomwangalia akiwa amekoncentrate kusikiliza anavyoburuzwa, huwa napata hasira ya kuvunja tv.

Kuna hilo likipindi na lile amani yetu tbc1, la mwanamboka.
Yanatumaliziaga umeme bure tu.

mkuu hawa jamaa wanaboa kishenji wa kina membe wanarudi mala 3 sasa hv hakuna wengine!
 
Tutaongea sana humu jf! Tatizo hatuungani pamoja kwenye harakati kwa action! (tukisema tuiname pamoja na tuinuke pamoja, chakushangaza tunainama wote,afu wanainuka wachache).
 
Tatizo kubwa la Selemani ni kwamba anakuwa kama shabiki badala ya kuwa muuliza maswali! Kwa kimombo he gets carried away by the answers given by his guests! Nimemwangalia mara nyingi wahojiwa wakisha jibu anaridhika kirahisi mno. Angalaie kipindi kama cha Jenerali Ulimwengu au Je tutafika au hata Hard Talk ajifunze. Kwa mfano mahojiano ya kina Wasira, Membe na Hosea zile zilikuwa ni tambo zaidi na yeye akawa anaduhaa!
 
Hivi wewe bado unakifuatilia? mimi nilisha kisahau kumbe bado kipo?
 
hivi kumbe bado kipo, yaani mimi huwa nabadilishaga chanell nikikiona kwa kweli kinakera. yaani jamaa utafikiri anawasindikiza badala ya kuwapiga maswali magumu. kingeitwa Safisha Njia CCM Ipite
 
Huyo mwendesha kipindi hana interview skills. Hajui kuuliza maswali magumu. Kazi yake ni kutabasamu na kumsaidia anayemhoji. Namwomba amwige Steven Sucker wa BBC.



Dah jamaa anaboa sana, utadhani yeye ndo anahojiwa bwana, maswali kibao yanaibuka katika mahojiano sijui anayapotezea au haelewi, utamuona anacheka tuuuuu, dah sasa hatasielewi kile kipindi kina dhima ipi?

Semunyu kabla hujafanya mahojiano, THINK BIG, THINK CRITICALLY, JARIBU KU-CONSULT WATU, angalau m -brainstorm uelewe mambo kwa mapana yake bro, tunatarajia changes bana.
 
Atapataje ukuu wa wilaya?? Anavyojichekesha utadhani hajielewi. Kila kitu wanaiga, wakiona wenzao wenye ujuzi wanaendesha vipindi hadi unatamani kisiishe! Lile likipindi halina tija zaidi ya kunadi chama!!
 
Kweli ukuu wa wilaya unatafutwa kwa fitna nyingi sana bado tu ndugu yetu Kibonde maana naona jina lake halifikishwi au hawamuoni atawasaidia sana kuwapigia mikelele ya hovyo na kuwa hadaa na danganya wadanganyika wilayani na vijijini!!hata Semunyu anaota ukuu wilaya siku moja!hajui kuwa katiba inabadilika na kuanzaia 2015?
 
J3, 06[SUP]th[/SUP] August, nafungua ITV, nakuta na Mh. January Makamba anaongea kwa upoleeee na maelezo ya kuzunguka zungukaaa (mf. "hakuna haja ya kukasirikiana…" n.k) nikadhani pengine tena amejiingiza kwenye sanaa (kwa ajili ya fundraising) kama vile anamwomba radhi mtu wake warudiane n.k au kama yuko msibani vile anatoa neno moja moja kwa umakini wakati wa rambirambi kumbe ni dakika 45 za kuhojiwa?

Yaani kweli ungeweza sinzia kwa kusikiliza majibu na kulala kabisa ungesikiliza maswali na namna ya uulizaji wa Selemani.

Mpaka dakika 45 zinaisha, Mtangazaji (na Umma) unaambulia kupata tu hisia za Naibu Waziri kuishia KUSIKITIKA kutokana na yaliyosemwa juu ya Kamati aliyokuwa anaisimamia kipindi cha nyuma lakini hakutoa tamko lolote KULAANI NA KUTAKA HATUA ZICHUKULIWE kama kweli kuna Mbunge aliye jiingiza katika kupokea rushwa au kutaka kumlinda Mtendaji Mkuu wa TANESCO (akionekana na hatia)!

Sikubaliani na wale wanosema eti Dakika 45 ni kipindi cha kuijenga CCM maana kwa mwendo huu kusudio hilo halitafiwa kamwe! Hii ni karne nyingine, watu wanasikiliza, wanachambua na kutoa hukumu!:israel:
 
Sasa si hao wanasiasa uchwara wangetengeza yao magumu na kuyajibu kiufasaha, pengine wangeleta maswali yanayoulizwa na raia,pamoja na kuibua mawazo mapya katika nchi. Mimi katika darasa langu tulishawai pewa nafasi ya kujitungia maswali+ kujibu+ kujisahihisha. Na maxi zilikuwa zinatolewa katika hizo block na maxi zilikuwa na mchango katika Mjumuisho wa muhula.

Na game halikuwa rahisi kama watu walivyodhani.Kwanza kujitungia mrahisi sana, hakumaanishi kuwa utazidi 1/3 ya test, pia kama maswali nayo hayajawekwa clear neno hadi neno,jibu linaweza lisiwe hilo mjiibuji anfikiri ingawa katunga yeye, na pia kujipendeleakatika kujipa majibu kunakupa adhabu ya kutolewa marks huku , yale makosa nayo yanapoteza marks .Yaani unaweza jikuta unadaia Maxi katik kipengele cha 3(Yaani kama huna marks, halafu ukapewa adhabu kwa kutolewa marks zilizoahinishwa kabla ya paper inakuwa 0-X%= -X%).
 


tatizo hilo ni kwa sekta na taaluma zote hapa nchini si waandishi wa habari pekee yao hata wanasheria ndiyo maana wanaingia mikataba mibovu,wafanyabiashara na wote wakiwemo wanaokosoa hivi sasa tatizo kwa sekta ya habari ipo hadharani zaidi na hivyo ni rahisi kufahamu
 
Kwa ujumla kijana anajitahidi sana..anajua kuuliza maswali magumu, yuko focused na anatoa muda wa kutosha kwa anayeuliza kufafanua mada. In really akikaza buti atafika mbali sana. CNN wanamsubiria kwa hamu sana.

Chunya News Network!
 
mkuu hawa jamaa wanaboa kishenji wa kina membe wanarudi mala 3 sasa hv hakuna wengine!

Haya ndo madhumuni ya thread hii and nothing else. Mbona hamjawahi hata siku moja kusema kuhusu Makwaia wa Kuhenga ambaye huwa ana-feign ignorance kwa kila kitu. Wamekuja na idea nzuri na kipindi kinaendelea ku-improve kila wakati and it is much better today than when it started. Tatizo mnataka kulinganisha BBC, chombo kilichoanzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, na waandishi mahiri mfananishe na ITV. Huko ni kutotenda haki. Sasa kama anatafuta ukuu wa wilaya kama Marine, mbona Marine hajawa?

Ni discretion ya wenye kipindi kujua ni nani wamuite na aeleze nini. Hiyo demokrasia yenu ifanyeni kwenye TBC ya walipa kodi. Sijawasikia mkilaumu Channel 10 ambayo kila siku huwaita Butiku, Kitine, Kaduma na Lwaitama! Nampongeza Semunyu, anajitahidi.
 
ila hichi kipindi kusema kweli hakitoi haki kwa wanasiasa wapinzani maana kipindi kililenga kuonesha uwajibikaji na challenge za serikali lakini viongozi wa serikali wamekuwa wakitumia kipindi hiki kutangaza siasa ya chama chao tawala na kuwapondea wenzao wapinzani kwakuwa wanajua hawawezi kupata fulsa za kujibu hoja kwenye kipindi hicho. napendekeza, muongozaji anapaswa awalimit kwenye hoja za kiserikali tu na ajue kutofautisha kati ya userikali na uchama. NAWASILISHA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…