Selemani Semunyu kipindi dakika 45 ITV hautendi haki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Selemani Semunyu kipindi dakika 45 ITV hautendi haki!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gamba Jipya, Jan 7, 2012.

 1. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa jijini kuwasabahi ndugu na jamaa baada ya muda mrefu, nimebahatika kuona kipindi cha Q&A cha ITV kinachoenda kwa jina la dakika 45 kinachoongozwa na mtangazaji kijana kabisa bwana Suleiman Semunye.

  Kipindi hiki kina idea kama ya Hard Talk cha BBC kuanzia setting mpaka background music kwa hiyo nachelea kusema kuwa hii ni idea ya Semunyu na ITV, lakini kwa ujumla ni kipindi kizuri endapo kitatumika vema.

  Tatizo nililoliona ni upeo mdogo sana wa mambo wa Bw. Semunye, huyu mtangazaji anaonekana kuwa na matatizo ya umakini na ufuatiliaji wa mambo, inaonekana dhahili huwa anafanya kipindi akiwa haja jitayarisha, hafanyi research na vilevile anamaswali yasiyokuwa na mashiko wala tija, mara nyingi wageni wake huwa wanamtumia na ku drive mijadala kutokana na ufahamu wake finyu wa baadhi ya mada zinazojadiliwa.

  Vilevile costume designer wa ITV awe anamtayarishia huyu jamaa suti na mashati yanayo mtosha (look good, feel good), mara zote amekuwa akivaa suti mbili na zote oversized, na kiatu pair hiyo hiyo kwa vipindi vyote vitatu nilivyoangalia.

  Najua expose ni tatizo kubwa sana kwa waandishi wengi wa habari wa Tanzania, lakini jaribuni kusoma magazeti ya nje na kuangalia tv za nje ili kupata exposure zaidi.

  Nakutakia kazi njema kijana mwenzetu natumaini utajifunza na kuchukua changamoto, kazi njema.

  Tuendelee kumkoma nyani giladi, moko moko!
   
 2. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  Maskini, juzi mzee Sumaye aligusia suala la uchapishaji fedha kwa nchi zenye uchumi mbaya au ulioshuka akisema kuwa kipindi wanachukua madaraka uchumi ulikuwa mbaya lakini wakajitahidi kuupandisha bila kuchapisha fedha, yeye akauliza sasa inamaana nchi yetu hali ni mbaya sana, kwa kuwa wamechapisha noti(banknote)mpya...lol!, hakuelewa chochote kabisa, maskini.
   
 3. k

  karichuba Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Naam, nadhani pia wajifunze kutoka kwa yule babu wa TBC1, this week,in perspective anavyotawala kipindi chake na hasa pale anapomalizia kwa majumuisho, unaona alivyojiaandaa na anajua kile alichotaka watazamaji wake wajue.
   
 4. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kazi ipo
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mkuu specify sehemu angalau chache ambazo umeona amekosa umakini au hakuzifanyia utafti. Kumbuka kwamba huyu siyo mtangazaji wa siku nyingi, lakini nionavyo mimi pamoja na uchanga wake anajitahidi sana na he has what it takes to be a wonderful mtangazaji in the near future.
   
 6. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nilibahatika kuona kpindi alichomuhoji Sumaye nilipata wasiwasi na upeo wake wa mambo ya kisiasa na uchumi..................Kipindi kizuri ila jamaa anatakiwa awe mdadisi wa mambo na ache kufanya kazi kwa mazoea
   
 7. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  kwenye Red hapo: HA HA HA maneno kuntu hayo..
  umeongea vizuuriii lakini mwisho hapo umekunya kwenye blue..ngoja nikuulize
  "kwani wewe ni WM @NY ?? maana hapo mwisho ye ndo hua anaandikaga ushuzi huo wa kitoto FB

   
 8. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni mtangazaji mzuri ndo maana vipindi vyake vingi akishafanya kesho yake kina make headlines kwny magazeti kwa mfano alivyofanya juzi na Sumaye na kile kipindi alivyofanya S. Sitta
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jana Yahya M wa star t.v alipewa dongo kama hli,akang'aka huyo,
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu kazi kweli kweli..
   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Bado ni mbunifu pamoja na mapungufu yote yanayoonekana. Kumbuka wanahabari wa TZ wengi wao hawana background ya yale wanayoyaandikia ..mhandishi wa habari za mahakamani unaweza kukuta ni yule aliyezoea kutangaza taarabu nk..hii ni changamoto kwani vijana wetu ngawila zinawafanya wahame taaluma. Waandishi wengi wa Habari hapa kwetu waliingia kwenye fani kufuatia ugumu wa maisha wakaanza kujifunza kuandika na baadae kujisomea kidogo kidogo mpaka wengine sasa ni maarufu
   
 12. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndo ameanza ujira,usijali atazoea na pia atabadili nguo
   
 13. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Kwa ujumla kijana anajitahidi sana..anajua kuuliza maswali magumu, yuko focused na anatoa muda wa kutosha kwa anayeuliza kufafanua mada. In really akikaza buti atafika mbali sana. CNN wanamsubiria kwa hamu sana.
   
 14. Mmasihiya

  Mmasihiya JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 368
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hapa umeongea nadhani kawapunguzia kazi baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari....ya Sumaye ilikuwa ktk kila gazeti na soure ITV.
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwa hli,
  indebt television(I.t.v)wameonesha ubunifu
   
 16. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada ume-base kwenye lawama bila kuangalia hata chembe ya jitihada ambazo kijana ameonesha, mfano imeonekana dhahiri kuwa yeye ndiye aliyekuja na hiyo idea coz baada ya yeye kuanza ndipo muda mfupi kipindi kikawa established, that means kuwa bila yeye ITV isingekuwa na kipindi hico kwa hilo tu NAMPONGEZA!

  Hayo mambo mengine atakomaa kadri ambavyo atazidi kufanya vipindi hivyo na kujifunza zaidil naamini hata Larry King hakuwa mzuri kwenye kipindi chake tangu siku ya kwanza ilichukua muda kuwa mtangazaji mahiri kwenye vipindi vyake!

  Asante.
   
 17. T

  TUMY JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunarudi pale pale tatizo letu wabongo ni kulaumu tu, tunasahau kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, toa maoni yako nini unafikiri kiboreshwe nafikiri ungekuwa umemsaidia sana kuliko kukimbilia kulaumu. Kwanza rudi ulipotoka sikukuu zimeshaisha nenda kafanye kazi ukirudi tena mwakani kuja kuwasabahi jamaa zako utakuta mabadiliko chanya. wasalimie ukifika.
   
 18. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #18
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Acha uzushi na ufinyu wa kufikiri.Mbona ameelezea vyema ,kasifia ,kabainisha mapungufu na katoa njia za kuboresha hayo mapungufu...Usikurupuke kuchangia mambo ili uonekane umechangia hoja ama uonekane unajua kukosoa.
   
 19. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo wapi wakati watu tunalia kazi (ajira) hakuna kaka??!!!
   
 20. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ndugu yangu Selemani Semunyu,

  Kwanini huelewi, tumeshakushauri mara nyingi kuhusu hicho kipindi chako, kwamba kuhoji hao viongozi wa kiserikali inatosha, jaribu kuwapa watu wengine nafasi ili ku-balance stories na kupata taarifa zingine.

  Kila siku ni Wassira na hali ya kisiasa nchini, mara Nagu na Wawekezaji, mara Joka la mdimu na harakati zake za Urais, 2015, INATOSHA... Leta makundi mengine sasa mfano Mawaziri vivuli wa CHADEMA, NGO za kisiasa na kiuchumi na hata wachumi....
   
Loading...